MTEI: Nililipwa Mshahara sawa na Nyerere

MTEI: Nililipwa Mshahara sawa na Nyerere

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Edwin Mtei akiwa gavana anasema alilipwa mshahara sawa na Nyerere akiwa Rais ili kupunguza tabaka la wenye kipato cha juu kutokana na uadilifu wa mwl. Nyerere ambapo kwa sasa ni vigumu sana.
==================================

mtei+px.gif

Arusha. Inawezekana likawa jambo nadra kutokea kwa sasa, lakini enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere lilitokea.

Ni baada ya mwasisi huyo wa Taifa kuamua kwa hiari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 10 ili kupunguza pengo baina ya maskini na wale wenye kipato cha juu, uamuzi ambao ulifuatwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati huo, Edwin Mtei.

Mwaka 1968, Mwalimu Nyerere aliyekuwa akilipwa mshahara wa Sh5,000 kwa mwezi alikiona ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na wengi wa watumishi na hivyo kuamua kukipunguza.

Mshahara huo wa Mwalimu Nyerere ni sawa na ambao alikuwa akilipwa pia Gavana Mtei. Kutokana na punguzo hilo, mishahara yao ilishuka hadi Sh4,500 kwa mwezi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Tengeru, nje kidogo ya Mji wa Arusha Jumatatu iliyopita, Mtei alisema alifikia uamuzi huo wa kupunguza mshahara wake baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza kupunguza mshahara wake.

Alisema: "Nilipunguza mshahara wangu tena kwa hiari yangu baada ya kuona Mwalimu Nyerere amepunguza wa kwake."

Alisema wakati ule mshahara wa Gavana ulikuwa ukipangwa na Serikali na kwamba ulikuwa na kipengele katika mkataba kikionyesha kuwa hauwezi kupunguzwa na mamlaka yoyote, labda atakapotaka mwenyewe.

Mtei ambaye pia ni mwasisi wa Chadema alisema sababu nyingine iliyomsukuma kupunguza mshahara wake ni kuona kwamba kama asingefanya hivyo, basi angemzidi mshahara Rais (Nyerere), kitu ambacho kwake hakukipenda.

Alisema, ingawa Mwalimu Nyerere alipunguza mshahara, lakini yeye kisheria hakuwa akibanwa kufanya hivyo kutokana na mkataba wake ambao ulikuwa ukiibana Serikali kutokuugusa mshahara wake.

Alieleza kuwa ukimwondoa yeye na Mwalimu Nyerere, Serikali iliamua kuwapunguzia mishahara watumishi wengine wa kada nyingine serikalini ili kubana matumizi.

"Watu wote walipunguziwa mishahara kuanzia vigogo wote (wa wakati ule)," alisema Mtei ambaye Jumamosi iliyopita alitimiza miaka 82 tangu kuzaliwa kwake.

Sababu za punguzo hilo

Alisema Serikali ya Mwalimu Nyerere iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona kuwa kulikuwa na pengo kubwa la kipato kati ya watumishi wa ngazi za chini na wale wa juu.

Mwanasiasa huyo ambaye aliteuliwa kuwa Gavana wa BoT akiwa na umri wa miaka 32, jambo ambalo ni mara chache kufanyika kwa vijana kuaminiwa na hata kupewa madaraka makubwa kiasi kile, alisema Mwalimu Nyerere alimwamini kwa kiasi kikubwa.

Kuhusu Mwalimu Nyerere, Mtei alisema alikuwa kiongozi mwadilifu, ndiyo maana akafanya uamuzi mgumu kama huo wa kugusa mshahara wake mwenyewe.

Alisema kwa kizazi cha sasa ni watumishi wachache wa kuweza kuwalinganisha naye.

Alisema baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka katika uongozi wa nchi, watumishi na hata viongozi walibadilika na kujiingiza katika mambo mengi yakiwamo yale ambayo yanakwenda kinyume na maadili.

Uongozi wa sasa

Mtei ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kabla ya kuteuliwa kuwa Gavana wa BoT alisema katika mazingira ya sasa hakuna kiongozi yeyote ambaye anaweza kukubali au kupunguza mshahara wake.

"Katika mazingira ya sasa, jambo hilo haliwezekani kabisa," alisema. Aliongeza: "Hivi sasa viongozi wengi wanashindana kupeleka na kuficha fedha Uswisi, wengi wao wanakimbilia kwenye utajiri, si utumishi."

Alisema hivi sasa viongozi wengi wametanguliza mbele masilahi yao na wengine kujiingiza kwenye ufisadi na hivyo kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo.

Mtei alisema viongozi wote lazima waongozwe na uzalendo na kuwahurumia wananchi wengi ambao ni maskini.

Alisema uamuzi walioufanya yeye na Mwalimu Nyerere hivi sasa unaweza kufanyika katika chama kingine kinachojali wananchi endapo kitaingia madarakani, ambacho hata hivyo alisema siyo CCM.

Chanzo;
Mwananchi
 
Edwin Mtei akiwa gavana anasema alilipwa mshahara sawa na Nyerere akiwa Rais ili kupunguza tabaka la wenye kipato cha juu kutokana na uadilifu wa mwl. Nyerere ambapo kwa sasa ni vigumu sana.
==================================

Chanzo;
Mwananchi

Mzee umechoka pumzika, Maelezo yako yanadhihirisha ulivyo na hata Chama chako pia. Bila aibu unawaambia watz Kuwa ulipunguza mshahara wako kwa Kuwa Mwalimu Nyerere alipunguza wa kwake na kwa kuona Kuwa usingefanya hivyo mshahara wako ungekuwa mkubwa kuliko was Mwalimu, kumbe hukusukumwa na uzalendo wala huruma kwa wananchi wa kipato cha chini, una tofauti gani na wale waliopunguziwa kwa nguvu? Huu ni unafiki usiovumilika kusikika masikioni. Eti Huyu ndio mwasisi wa Chama mbadala! Tumekusikia Mzee hatutafanya makosa kamwe.
 
Ujinga mwingine unatisha sana,

Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.

Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.
 
Uwe unasoma na kuelewa kabla Ya kupost, Mshahara wake ulikuepo kisheria na sheria ilikua inamlinda asiguswe na mamlaka yoyote ile juu mshahara wake. Hivyo uamuzi wa kupunguza kipato chake ilikua ni heshima kwa mkuu wake na kwa wananchi.

Je, kwenye CCM Ya sasa nani anaweza kupunguza mshahara wake kwa hiyari achilia mbali kwa lazima.?
 
Huyo mzee hakutaka kabisa kutumikia wa-Tz, hakushiriki kabisa hata kutafuta uhuru japo tayari alikuwa ana kaelimu kake. Na hata kuja kufanya kazi Tz ilikuwa ni kwa masharti ya kulipwa pesa nyingi sana. Hana hata chembe ya uzalendo.

Uwe unasoma na kuelewa kabla
Ya kupost, Mshahara wake ulikuepo kisheria na sheria ilikua inamlinda
asiguswe na mamlaka yoyote ile juu mshahara wake. Hivyo uamuzi wa
kupunguza kipato chake ilikua ni heshima kwa mkuu wake na kwa wananchi.

Je, kwenye CCM Ya sasa nani anaweza kupunguza mshahara wake kwa hiyari
achilia mbali kwa lazima.?
 
Viongozi na wana siasa wetu wapunguze mishahara yao?Thubutu
 
Inaonekana una chuki kubwa sana na mwl nyerere
Ujinga mwingine unatisha !sana,

Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.

Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.
 
Huyu mzee hakuwa na moyo wa kutumikia watanzania kabisa, ndio maana wakati anakula ajira alitaka hata sheria za kulinda mshahara wake ziwepo.

Nani anayeweza akatuambia mzee Mtei amefanya nn nchi hii zaidi ya kuanzisha CHADEMA SACCOS?

Big up jembe letu la moshi mtei
 
Ujinga mwingine unatisha sana,

Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.

Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.

Jamani lini tutaacha ushabiki? Wakati mwingine tutumie akili ya kawaida kubishana wakati aliyoyasema Mtei ni mambo ya msingi na hayagusi vyama kabisa. Yana akisi utaifa mbele na si vinginevyo.

Kuhusu Nyerere hata asipochukua mshahara alikuwa na shida ipi? Jamani! Kama rais hana shida kwa vile anapewa kila kwa nini wanalipwa mshahara wa zaidi ya mil.30?
 
kipind hcho naona huyu mze alikuwa bado na akili kichwani. Sasa amebaki vacum tu
 
Huyo mzee hakutaka kabisa kutumikia wa-Tz, hakushiriki kabisa hata kutafuta uhuru japo tayari alikuwa ana kaelimu kake. Na hata kuja kufanya kazi Tz ilikuwa ni kwa masharti ya kulipwa pesa nyingi sana. Hana hata chembe ya uzalendo.

mtei atueleze kwanini alikataa kupigania uhuru na nyerere?
Kwa nini alitaka kuiuza nchi kwa wazungu?
 
Angalia kuongea bila kufikiri kunaonesha uwezo wa akili uliyonayo kwamba bado changa. Nyerere alijitahidi sana, kuongoza nchi kwa wakati ule ilikuwa kazi ngumu sana ukizingatia na idadi ya uchache wa wanataaluma na Ukabila ambao ulikuwepo. Lakini katika yote aliweza kuwaunganisha watanzania wakaacha ukabila wao, na Serikali kwa wakati ule ilikuwa inatatua mambo ya msingi tofauti na ilivyo kwa sasa. Viongozi wanapenda kuendeshwa kwenye V8 wakati hospital hazina dawa na vifaa vya kutosha, kuuwa viwanda na ukosefu wa ajira, ufisadi.

Hatusemi kuwa Nyerere hana mapungufu ila kwa kiasi chake alifanya zaidi kuliko inavyostahili, kwa hiyo ni miongoni mwa viongozi Bora AFRIKA tena sio Tanzania.

Ujinga mwingine unatisha sana,

Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.

Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.
 
Mkweo mbona anatafuna ruzuku kama hana Akili nzuri kwenye Saccoss yenu?

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Nyerere hakuwa mhuni, wanaogombea urais hivi sasa wote ni wahuni na wanawekwa na wahuni wenzao, Mtu kama Rage au Kinana eti ni viongozi tegemea watachagua viongozi aina gani?

ni kweli mkuu,ukiwaangalia kinana na rage,sidhani km wana hadhi ya vyeo walivyonabyo,uaani ni wahuni wahuni tu,km ilivo kina membe na bos wake
 
Back
Top Bottom