Uelewa wako unatia shaka. Mzee mtei anamlinganisha Nyerere katika nafasi yake na maraisi wengine wa siku hizi katika nafasi ile ile. Kama Nyerere hakuwa na shida ni vivyo hivyo kwa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Jakaya. Hata hawa wasipochukuwa mishahara yao haina tofauti na Marehemu Nyerere asingalichukua. Sasa kama vile haitoshi hawa viongozi wa sasa sio hawapunguzi mishahara kwa kuwahurumia masikini bali pia huwaibia zaidi masikini na kujilimbikizia wao wenyewe na jamaa zao. Inashangaza kama huelewi mantiki ya Mzee Mtei, basi una safari ndefu sana kuweza kuchambua mambo. Mtei hamlinganishi Marehemu Nyerere na mtu kama wewe anamlinganisha na viongozi walioshika au kupata kushika nafasi kama yake. Upo hapo? Ua umejianda kutetea tu jambo lolote ili mradi uonekane umechangia? Hivi kweli unaweza kulinganisha uadilifu wa Marehemu Nyerere na kiongozi yupi wa sasa Tanzania ya leo? Mtei ingawaje haikuwa dhamira yake kupunguza mshahara wake lakini kwa kuona Boss wake amepunguza alipunguza pia mshahara wake, ina maana Mzee Mtei aliona aibu Boss wake apunguze halafu yeye apate zaidi ya Boss wake. Angalao Mtei aliona aibu, viongozi wa sasa hata HAYA hawana.
Ujinga mwingine unatisha sana,
Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.
Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.