Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

Kwanini shutuma za ufisadi hazikutumika kuwaengua Chenge na Rostam kwenye kugombea Ubunge?

Mhimili wa mahakama upo bias,hao watu wapo ndani ya mfumo wa chamadola,kwa mahakama yetu corrupt huwezi mtia hatiani mtu kama Chenge na Rostam.
Rejea kesi ya ajali ya Chenge.
Mkuu wewe hujui kuwa selikali ya CCM inaingilia utendaji kazi wa mhimili wa mahakama? Pinda kashtakiwa kuvunja katiba,subiri uone uamuzi wa kesi.
 
Shutuma? Kwa chama kipi, endapo mtumishi wa Mungu alisema shutuma tu zingeweza kumtoa mtu kazini, ni nani mwenye unyoofu wa Mwinyi na mrema ambao walukubali kujiuzulu nyadhifa zao? Post za kitoto ndizo zitaua kabisa usalama wetu

Umenikumbusha Dr. Slaa alivyokataa kujiuzuru baada ya kuvujisha barua ya siri aliyoandikiwa na kiongozi mwandamizi wa chama chake.

By the way, Dr. Slaa ni mwanasiasa ambaye hajawahi kuomba msamaha hata siku moja, anajiona yeye yuko perfect wakati wote...
 
kwa udaku wako huu, inabidi twende kotekote mkuu, unaunganishaunganisha vijistori vya vijiweni halafu unatuletea hapa jamvini! Mtahangaika sana lakini kamanda mbowe atazidi kudunda mkuu...

Wabadhilifu wengi wa mali ya umma wanadunda mitaani.
 
Umenikumbusha Dr. Slaa alivyokataa kujiuzuru baada ya kuvujisha barua ya siri aliyoandikiwa na kiongozi mwandamizi wa chama chake.

By the way, Dr. Slaa ni mwanasiasa ambaye hajawahi kuomba msamaha hata siku moja, anajiona yeye yuko perfect wakati wote...
kama kujiuzulu walipaswa kuanza viongozi wa ccm, mbona jk hajawahi kujiuzulu? Lini jk aliwahi kuomba msamaha watanzania kwa uhuni na mateso anayowafanyia?
 
Mzee Edwin I. Mtei, alikuwa Gavana wa Benki kuu kwa kipindi cha miaka minane kuanzia 1966 hadi 1974.

Aidha umedhamiria kudanganya au hauna taarifa sahihi, lakini hiki ulichoandika hapa si kweli.
 
Utajiri halali unaonekana kwenye kiasi cha kodi anacholipa mtu na idadi ya watu aliowaajiri.

Mbowe ameajiri watu wangapi? Mention 5 degree holders walioajiriwa na Mbowe.

Usilete story za vijiweni za "ubilionea" wa Arusha.

Kule juu kwenye bandiko umesema "anamiliki mali zisizohamishika" tutajie hizo mali na mimi nitakutajia anazitumia vipi hapo utajua aina za watu walioajiliwa katika mali hizo.
 
Mwenyekti wa kwanza wa Chadema, Mzee Edwin Mtei, alikuwa Gavana wa BoT.

Mwenyeti wa sasa wa Chadema, Mh. Freeman Mbowe, alikuwa mwajiriwa wa BoT.

Kabla ya kupata uenyeti wa Chadema, Mh. Freeman Mbowe, alimuoa mtoto wa Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, Mzee Edwin Mtei.

Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, amekiri kwa maandishi kuwa anamiliki mabilioni ya shilingi pesa tasilimu na mali zisizohamishika yenye thamani ya mabilioni ya shilingi.

Hesabu za kiasi cha kodi alicholipa Mh. Freeman Mbowe kwa miaka kumi iliyopita hakiendani na utajiri huo mkubwa alio nao.

Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema Mzee Edwin Mtei, hupenda kujitambulisha kama mkulima. Hata hivyo, utajiri wake ni mkubwa sana kuliko kiasi cha uzalishaji wa shamba lake lililopo Tengeru, Arusha.

Mzee Mtei amekuwa akitumia pesa zake binafsi kuendesha shughuli zote za Chadema tangu ilipoanzishwa mpaka ilipofikia hatua ya kupata wabunge na ruzuku. Huu ni utajiri wa hali ya juu. Sio mbaya kuwa tajiri, lakini utajiri wa mtu ni lazima uendane na kiasi cha kodi anacholipa. Mtu akiwa tajiri sana lakini katika orodha ya walipa kodi haonekani, ni ishara ya ufisadi.

Ukwasi huu wa wanasiasa hawa wawili walioitumikia BoT na kuamua kuunganisha familia zao kwa njia ya ndoa ya binti wa mmoja wao unatokana na chanzo gani?

Je, kuunganisha familia hizi ni njia ya kuongeza uaminifu wa "ushirikiano" waliokuwa nao tangu BoT? Je, "ushirikiano" wao waliouanza BoT unaendelea ndani ya Chadema? Je, hii ndio sababu ya Mzee Mtei kulazimisha Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti na kukataza wagombea "who are from nowhere"?.

Je, biashara ya ukumbi wa muziki inamuwezesha mtu kumiliki mabilioni nje ya nchi? Kiingilio bilicanas ni shilingi ngapi kila mtu? Kwa siku wanaingia watu wangapi? Je, zinatosha kununua nyumba Uingereza, Marekani, Afrika Kusini na Dubai?

Its too early to go to bed, wake up. Connect the dots...
Umeishapewa ngumi za uso hapa chini!! Huna hoja tena!! Muongo mkubwa!! Hebu soma hii:
Mzee Edwin I. Mtei, alikuwa Gavana wa Benki kuu kwa kipindi cha miaka minane kuanzia 1966 hadi 1974. Wakati anateuliwa kuwa Gavana mtoto Freeman Aikaeli Mbowe alikuwa na umri wa miaka mitano (alizaliwa mwaka wa uhuru 1961) na wakati Mzee Mtei anaacha kazi Benki Kuu Kijana Mbowe alikuwa na umri wa miaka 13!
 
Wewe ni mlaghaika.

Hizo taarifa ulizoandika sio sahihi.

Connect the dots...
 
Si kosa langu, serikali iliyoko madarakani ni ya CCM...ni ya serikali dhaifu, serikali tapeli na serikali ya wauaji. Bonyeza hapa;

Dont blame the book, blame your lack of curiosity...
 
Mkuu Marco,
Pale juu,unejaribu kuunganisha dhana ya Mbowe kuoa mtoto wa Mtei.
Ulitaka kutuambia nini? Je,unataka kutuaminisha kwamba mtoto wa Mtei kamtajirisha Mbowe?
Kama ndivyo,hivi leo mtu akioa binti yako,wakatafuta hela wao,wakazipata,utatembea kifua mbele kuwa wewe (mkwe) ndio umewapa utajiri huo?
 
Biashara zote za Mbowe zinasimamiwa na mtoto wa Mtei.

Connect the dots...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom