Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

Mwaka 1979 Mwalimu Julius Nyerere alipomsimamisha kazi Edwin Mtei(gavana wa BoT wakati huo),kinyongo kiliendelea.Ulikuwepo msuguano mkubwa kati ya Mwalimu na Mtei kuhusu utekelezaji wa sera za IMF nchini Tanzania na katika moja ya mambo ambayo Mwalimu hakutaka hata kuyasikia lilikuwa suala la kushusha thamani shilingi yetu dhidi ya fedha za nchi za kigeni (devaluation) tulizokuwa tunafanya nazo biashara.Katika moja ya hotuba za Mwalimu alishaliongelea hili.1979 haukuwa mwaka mzuri kwa Edwin Mtei ila alipata kazi katika shirika la fedha IMF na kuhamia Marekani ambapo wanawe walipata elimu yao huku akiwepo Lilian Mtei ambaye baadaye alikuja kuolewa na Freeman Aikaeli Mbowe.

Nimekuwekea haka kastori kafupi lakini kana maana kubwa sana
- Edwin Mtei ameishafanya kazi katika Shirika la IMF je huko hakupata fedha ambazo anaweza kuwa ameziendeleza na kuongezeka maradufu?
- Wakati wa Nyerere kulikuwa na uwezekano wa kiongozi kuiba fedha kama unavyojiaminisha sasa?

Ukimtaja mtuhumiwa mmoja tu wa ufisadi wa mali ya umma ambaye ni jobless basi kauli yako hii itakuwa na mashiko.
 
Lailaa hailalaa... Mohamad rasululaah x5
 
Mkuu huo ni udaku! Kuna kada moja maarufu ndani ya ccm aliwahi kuniambia kuwa baba ake mbowe alikuwa akimdhamini mzee nyerere wakati wa kudai uhuru wa tanganyika! Sasa nimeamini yale maneno. Pia kinachonishangaza propaganda za huko lumumba ni kwamba mara zote mnadai mbowe alipata zero form six, je aliajiriwa vipi pale BoT? Je nchi hii mwenye mabilioni ni mbowe pekee? Wapi kina chenge? Wapi kina lowasa?. Ccm haitapona kwa majungu haya!
 
Mbowe alifanya kazi BOT mwaka gani na Mtei aliacha kufanya kazi BOT mwaka gani?? Miaka ikiwekwa wazi ndo tutakua na hoja ya kujadili hapa.

Mkuu haya maCCM ni majinga sana ebu soma stori hii hapa chini utaelewa jinsi yalivyo kwani yanaandika na kuanzisha mambo pasipo kuwa na kumbukumbu vizuri.

Mwaka 1979 Mwalimu Julius Nyerere alipomsimamisha kazi Edwin Mtei(gavana wa BoT wakati huo),kinyongo kiliendelea.Ulikuwepo msuguano mkubwa kati ya Mwalimu na Mtei kuhusu utekelezaji wa sera za IMF nchini Tanzania na katika moja ya mambo ambayo Mwalimu hakutaka hata kuyasikia lilikuwa suala la kushusha thamani shilingi yetu dhidi ya fedha za nchi za kigeni (devaluation) tulizokuwa tunafanya nazo biashara.Katika moja ya hotuba za Mwalimu alishaliongelea hili.1979 haukuwa mwaka mzuri kwa Edwin Mtei ila alipata kazi katika shirika la fedha IMF na kuhamia Marekani ambapo wanawe walipata elimu yao huku akiwepo Lilian Mtei ambaye baadaye alikuja kuolewa na Freeman Aikaeli Mbowe.

Mkuu Marco,wewe si ndio unasema kila siku Mbowe hana elimu!! Sasa tuambie BOT aliajiliwa lini na kwa post gani?
Pia kupigia mahesabu pesa ya Mbowe kwa kigezo cha ukumbi,umechemka vibaya bwana Mkunga.
Jaribu anzia kudadafua pesa alioichuma mzee wake Mbowe,tueleze uhalali wake,ndipo uje kwa Mbowe.
Pesa ya Mbowe ni ya kurithi mkuu,alichokifanya kaiendeleza kama ilivyo kwa Uhuru Kenyatta au Prezzo mwanamuziki wa Kenya.
 
mwambie mkuu: kule uchagani hakuna nyumba ya nyasi hata moja...!!!!!

hivi nyumba ya nyasi nikipimo cha umaskini mbona hotel kibao za utalii wanazo au jamii za wafugaji wanazo coz wanahamahama na huku wana mifugo ya ml
 
Mkuu huo ni udaku! Kuna kada moja maarufu ndani ya ccm aliwahi kuniambia kuwa baba ake mbowe alikuwa akimdhamini mzee nyerere wakati wa kudai uhuru wa tanganyika! Sasa nimeamini yale maneno. Pia kinachonishangaza propaganda za huko lumumba ni kwamba mara zote mnadai mbowe alipata zero form six, je aliajiriwa vipi pale BoT? Je nchi hii mwenye mabilioni ni mbowe pekee? Wapi kina chenge? Wapi kina lowasa?. Ccm haitapona kwa majungu haya!

Unataka orodha ya watu waliopata zero ambao wako BoT?
 
Mkuu Marco,wewe si ndio unasema kila siku Mbowe hana elimu!! Sasa tuambie BOT aliajiliwa lini na kwa post gani?
Pia kupigia mahesabu pesa ya Mbowe kwa kigezo cha ukumbi,umechemka vibaya bwana Mkunga.
Jaribu anzia kudadafua pesa alioichuma mzee wake Mbowe,tueleze uhalali wake,ndipo uje kwa Mbowe.
Pesa ya Mbowe ni ya kurithi mkuu,alichokifanya kaiendeleza kama ilivyo kwa Uhuru Kenyatta au Prezzo mwanamuziki wa Kenya.

Umeshawahi kujiuliza kiasi cha pesa cha baba yake Chenge?
 
Lailaa hailalaa... Mohamad rasululaah x5

Mkuu Tuko,

Usishtuke sana. Ndio wanasiasa wetu walivyo. Maneno mengi majukwaani, kumbe nyuma ya pazia wana agenda za siri...
 
ZeMarcopolo, nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini pamoja na kujiunga JF tarehe 11/5/2008 (ukiwa umenitangulia kwa siku 20) na baada ya kuwa na posts zaidi ya 10,000 (mimi nikiwa na posts chini ya 4,000), kwa nini rep power yako ni 0 (sufuri). Kwa mara ya kwanza naweza kusema nimepata jibu la swali langu hilo kutokana na post zako ambazo kila siku zinazidi kukufichua uwezo wako kifikra na kiakili. Thread yako ya kwanza jamvini lilikuwa ni la kupongeza jitihada zilizokuwa zikifanyika mjini Moshi kuwasaida watu wenye matatizo ya akili. Wakati huo sikuweza kuunganisha dots hizo juhudi zako zilitokana na msukumo gani hasa?...kwa nini nauliza hivi?

Mzee Edwin I. Mtei, alikuwa Gavana wa Benki kuu kwa kipindi cha miaka minane kuanzia 1966 hadi 1974. Wakati anateuliwa kuwa Gavana mtoto Freeman Aikaeli Mbowe alikuwa na umri wa miaka mitano (alizaliwa mwaka wa uhuru 1961) na wakati Mzee Mtei anaacha kazi Benki Kuu Kijana Mbowe alikuwa na umri wa miaka 13! ZeMarcopolo, umeanza mada yako kwa kusema nanukuu;

Hukuishia hapo ukaanza kuunganisha dots kwa kudai, nanukuu;
ZeMarcopolo, kama asemavyo Invisible, Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!:coffee:
mkuu hizi zinaitwa za uso mkuu! Hongera sana!
 
Maswali, sio lazima lazima yajibiwe, lakini lazima yaulizwe, kama kweli wahusika wanaweza kuyajibu poa, ila hata sie tunashangaa......
Kuoa kwenye mkondo wa mapesa, habari iliyopo, kwamba huwezi oa kwa akina Kida, Mareale n.k kama huna pesa au damu ya uchifu...Sijahakikisha.....
Ila kama kweli basi hawa hawana tofauti na CCM, wanarusha mawe kwenye majengo ya glasi, wakijua nao wanaishi kwenye majengo kama hayo...
Kama Mh. Mbowe angeoa demu wa kawaida tu, aliyesoma, mzuri, mwenye tabia safi...Twauliza, je angekua mwenyekiti wa CHADEMA leo??????????????
 
Umeshawahi kujiuliza kiasi cha pesa cha baba yake Chenge?

Historia ya Chenge na Mbowe vitu viwili tofauti mkuu. Chenge anahistoria ya kuwa AG wa nchi yetu,tuambie Mbowe BOT aliserve kama nani?
Twende taratibu ninachokijua nitakueleza.
 
Naomba kwanza unijibu maswali yangu ya msingi nitauliza moja moja.
Mosi,unaweza kunipa japo kwa aya mbili namna unavyomfahamu Baba yake Mbowe mzee Aikaeli,hususani biashara zake kwa wakati huo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom