Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

Mkuu Tuko,

Usishtuke sana. Ndio wanasiasa wetu walivyo. Maneno mengi majukwaani, kumbe nyuma ya pazia wana agenda za siri...

Sikushtuka... ila niliona niendeleze tu bla bla kama zako. Ningeshtuka kama ungeweka figures mzee. Unajua unapoongelea hela inabidi utaje figures ku make sense. Kwa mfano tukiongelea mabilioni ya uswis haileti maana hadi tuseme bilioni 334 huko uswis. Hebu weka figures za mabilioni ya Mbowe figures za kodi, nk tuone...
 
Naomba kwanza unijibu maswali yangu ya msingi nitauliza moja moja.
Mosi,unaweza kunipa japo kwa aya mbili namna unavyomfahamu Baba yake Mbowe mzee Aikaeli,hususani biashara zake kwa wakati huo?

Umeanza hadithi za vijiweni za "mabilionea" wa Arusha...
 
Umeanza hadithi za vijiweni za "mabilionea" wa Arusha...

Ha ha mkuu Marco,stori za vijiweni zinatoka wapi? Tunataka tukusaidie kuelewa connection ya utajiri wa Mbowe huyu mtoto wa Aikael.
Tuambie unamjua vipi hata kwa kuambiwa tuu.
 
Sikushtuka... ila niliona niendeleze tu bla bla kama zako. Ningeshtuka kama ungeweka figures mzee. Unajua unapoongelea hela inabidi utaje figures ku make sense. Kwa mfano tukiongelea mabilioni ya uswis haileti maana hadi tuseme bilioni 334 huko uswis. Hebu weka figures za mabilioni ya Mbowe figures za kodi, nk tuone...

Connect the dots...

Mtei alipoulizwa kuhusu tenda ya magari ya M4C alijibu hivi:

niliachia ngazi Chadema 1998 na tangia hapo sishiriki ktk mambo ya uendeshaji wa Chama ambapo ningeweza kukujibu juu ya zabuni iliyohusu magari ya M4C.

Je wewe unaamini kuwa Mtei hajui kuhusu taratibu za kununua magari ya Chadema.

Pitia hapa kwa kumbukumbu...
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...m4c-na-pikipiki-kufisadi-ruzuku-ya-chama.html
 
Umesema "hesabu za kodi za biashara ua Mbowe haziendani mapato yake kwa miaka kumi iliyopita".
Mwaka 2005 Mbowe aligombea uraisi,kwanini kigezo cha kutokulipa kodi hakikutumika kumuengua kwa mujibu wa katiba? Marco wewe ni mzima mkuu tena unakisomo.
 
Mwenyekti wa kwanza wa Chadema, Mzee Edwin Mtei, alikuwa Gavana wa BoT.

Mwenyeti wa sasa wa Chadema, Mh. Freeman Mbowe, alikuwa mwajiriwa wa BoT.

Kabla ya kupata uenyeti wa Chadema, Mh. Freeman Mbowe, alimuoa mtoto wa Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, Mzee Edwin Mtei.

Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, amekiri kwa maandishi kuwa anamiliki mabilioni ya shilingi pesa tasilimu na mali zisizohamishika yenye thamani ya mabilioni ya shilingi.

Hesabu za kiasi cha kodi alicholipa Mh. Freeman Mbowe kwa miaka kumi iliyopita hakiendani na utajiri huo mkubwa alio nao.

Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema Mzee Edwin Mtei, hupenda kujitambulisha kama mkulima. Hata hivyo, utajiri wake ni mkubwa sana kuliko kiasi cha uzalishaji wa shamba lake lililopo Tengeru, Arusha.

Mzee Mtei amekuwa akitumia pesa zake binafsi kuendesha shughuli zote za Chadema tangu ilipoanzishwa mpaka ilipofikia hatua ya kupata wabunge na ruzuku. Huu ni utajiri wa hali ya juu. Sio mbaya kuwa tajiri, lakini utajiri wa mtu ni lazima uendane na kiasi cha kodi anacholipa. Mtu akiwa tajiri sana lakini katika orodha ya walipa kodi haonekani, ni ishara ya ufisadi.

Ukwasi huu wa wanasiasa hawa wawili walioitumikia BoT na kuamua kuunganisha familia zao kwa njia ya ndoa ya binti wa mmoja wao unatokana na chanzo gani?

Je, kuunganisha familia hizi ni njia ya kuongeza uaminifu wa "ushirikiano" waliokuwa nao tangu BoT? Je, "ushirikiano" wao waliouanza BoT unaendelea ndani ya Chadema? Je, hii ndio sababu ya Mzee Mtei kulazimisha Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti na kukataza wagombea "who are from nowhere"?.

Je, biashara ya ukumbi wa muziki inamuwezesha mtu kumiliki mabilioni nje ya nchi? Kiingilio bilicanas ni shilingi ngapi kila mtu? Kwa siku wanaingia watu wangapi? Je, zinatosha kununua nyumba Uingereza, Marekani, Afrika Kusini na Dubai?

Its too early to go to bed, wake up. Connect the dots...
Niwajuavyo CCM walivo na wivu kwa wafanya biashara wasio wanachama wao wangeshamtumia TRA kumfilisi lakini hilo limewashinda kwa vile MBOWE nimfanyabiashara halali sikama hao wengine LAKAIRO ET AL! wakwepa kodi sasa we polo unavosema anakwepa kodi nani alaumiwe? ilaumu serikali yako dhaifu basi!
 
Ha ha mkuu Marco,stori za vijiweni zinatoka wapi? Tunataka tukusaidie kuelewa connection ya utajiri wa Mbowe huyu mtoto wa Aikael.
Tuambie unamjua vipi hata kwa kuambiwa tuu.

Utajiri halali unaonekana kwenye kiasi cha kodi anacholipa mtu na idadi ya watu aliowaajiri.

Mbowe ameajiri watu wangapi? Mention 5 degree holders walioajiriwa na Mbowe.

Usilete story za vijiweni za "ubilionea" wa Arusha.
 
Niwajuavyo CCM walivo na wivu kwa wafanya biashara wasio wanachama wao wangeshamtumia TRA kumfilisi lakini hilo limewashinda kwa vile MBOWE nimfanyabiashara halali sikama hao wengine LAKAIRO ET AL! wakwepa kodi sasa we polo unavosema anakwepa kodi nani alaumiwe? ilaumu serikali yako dhaifu basi!

Hata wale wanaotumia pesa za ada za watoto wao kunywa pombe hawako mstari wa nyuma kuilaumu serikali kwa kile walichofanya...
 
Umesema "hesabu za kodi za biashara ua Mbowe haziendani mapato yake kwa miaka kumi iliyopita".
Mwaka 2005 Mbowe aligombea uraisi,kwanini kigezo cha kutokulipa kodi hakikutumika kumuengua kwa mujibu wa katiba? Marco wewe ni mzima mkuu tena unakisomo.

Kwanini shutuma za ufisadi hazikutumika kuwaengua Chenge na Rostam kwenye kugombea Ubunge?
 
Wakishindwa kuhalamisha pesa ya Mbowe,watahamia kwa Ndesamburo,napo watagonga mwamba. Wanaume wana pesa safi hawa.
 
Utajiri halali unaonekana kwenye kiasi cha kodi anacholipa mtu na idadi ya watu aliowaajiri.

Mbowe ameajiri watu wangapi? Mention 5 degree holders walioajiriwa na Mbowe.

Usilete story za vijiweni za "ubilionea" wa Arusha.
mbowe analipa kodi kiasi gani? Na ana mali kiasi gani? Acha blah blah mkuu!
 
Kwanini shutuma za ufisadi hazikutumika kuwaengua Chenge na Rostam kwenye kugombea Ubunge?
tuanze kukuuliza wewe wa lumumba mkuu, pia tuulize hiyo serikali yako ya ccm, kwa nini iliwaacha hawa mafisadi kuendelea kugombea uongozi tena kwa kupeperusha bendera ya chama chao?
 
Kwanini shutuma za ufisadi hazikutumika kuwaengua Chenge na Rostam kwenye kugombea Ubunge?
Shutuma? Kwa chama kipi, endapo mtumishi wa Mungu alisema shutuma tu zingeweza kumtoa mtu kazini, ni nani mwenye unyoofu wa Mwinyi na mrema ambao walukubali kujiuzulu nyadhifa zao? Post za kitoto ndizo zitaua kabisa usalama wetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom