Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...



Kahawa ni biashara yake anayofanya miaka mingi. Hapo alikuwa anapigania biashara yake!

Mtei yuko kimaslahi zaidi...
 

ZEMarcopolo,

Nimeeleza kwamba nikiwa Gavana BoT (1965-74), Freeman Mbowe na binti yangu Lillian walikuwa watoto wachanga, na singeweza kuwashirikisha katika miradi. Freeman alikuwa na miaka 4, na Lillian alikuwa na mwaka mmoja!!

Licha ya kwamba hizi zilikuwa enzi za Ujamaa, babake Freeman alikuwa mjasiriamali mzito, akimiliki Mbowe Hotels Dar es Salaam na Moshi, na ni wakati huu alijenga Aishi Hotel huko Machame. Nakumbuka nikihudhuria uzinduzi rasmi wa Aishi Hotel uliofanywa na Rais Mwalimu Nyerere aliyekuwa rafiki wa Aikaeli Mbowe. Wakati huu sikuwa mzazi mwenza na Freeman labda alikuwa shule ya sekondari.

Freeman Mbowe amerithi hii miradi baada ya kifo cha babake, na ameiendeleza na kuipanua kwa umahiri sana, e.g. kama kuongeza Club Billicanas huko Dar, na Conference Centre pale Aishi. Umahiri na umakini wa Freeman katika business na sawa na ule anaodhihirisha kama mwanasiasa.

Kuhusu mimi binafsi, umesema ukweli kwamba shamba langu la kahawa si kubwa. Gharama za uendeshaji ni kubwa. na mimi nasema nalima kahawa kama "hobby" tu. Ni wakulima wachache sana wanaopata faida kwa kulima kahawa. Soko lake linamilikiwa na wanywaji wa kahawa nchi za nje na hii ndiyo sababu ya kusuasua kwa zao hili hapa Tanzania.

Hata hivyo mara baada ya kununua hili shamba 1980, nilihamia Washington D.C. kama Executive Director wa IMF (end 1982) kwa kupendekezwa na Rais wangu, Mwalimu Nyerere. Nilibahatika kuhama na wanangu waliokwenda kumalizia shule za sekondari huko, pamoja na University kabla ya kurudi nyumbani. Binti yangu Lillian alirudi nyumbani baada ya High School na kujiunga na Muhimbili Medical, akawa daktari. Ni wakati huu walifahamiana na Freeman, wakaoana August 1991 kabla hata ya harakati za siasa ya vyama vingi.

Nimesema nilibahatika kuteuliwa IMF Executive Director 1982, na nilipofika huko nilijiunga na pension scheme ya IMF, ambapo mara baada ya kurudi nyumbani na kuwa na umri wa miaka 60, nikaanza kulipwa pension. Pamoja na savings zangu za huko Washington niliweza kukamilisha masomo ya wanangu na IMF sasa inanilipa pension ambayo ni kidogo kutokana na muda mfupi (miaka 4 tu) niliyotumikia shirika hili la kimataifa.

Kutokana na pension yangu na mapato mengine e.g. house rent tumeweza kuishi na kuendeleza maisha yetu bila kuwa ombaomba. Ukulima wetu sasa unabadilika taratibu kuwa pia na mahindi pamoja na kuongeza nyumba hapa shambani kadri kipato kinavyoruhusu au mikopo inavyopatikana.
 
Mtei kwa tunaokufahamu tutaendelea kukupa heshima yako kama mmoja wa watanzania walioitumikia hii nchi kwa uaminifu mkubwa. Siasa itaendelea lakini pia tuwaenzi wale waliotukuka.

Tuongee kuhusu kahawa kidogo............... kuna miche ya kahawa inapandwa kule nyumbani kwa utafiti wangu inazaa mara moja au mbili halafu inakauka .... ni kwa nini hasa. Kwanini isiboreshwe tukapata kahawa kama ile ya zamani ya kuzaa hadi miaka kumi na zaidi?
 

Dada Mamndenyi,

Nashauri wasiliana na Profesa James Teri, Mkurugenzi wa TaCRI ambaye ataweza hata kupeleka wataalamu hapo shambani kwako wakatambua tatizo na kukushauri la kufanya. Simu yake ya kiganjani ni 0754 473895.
 
Haika mnu mbee;

Nitamtafuta hasa nitakapokuwa maeneo ya kule kule shambani;

Kazi njema sana mzee wetu.

Dada Mamndenyi,

Nashauri wasiliana na Profesa James Teri, Mkurugenzi wa TaCRI ambaye ataweza hata kupeleka wataalamu hapo shambani kwako wakatambua tatizo na kukushauri la kufanya. Simu yake ya kiganjani ni 0754 473895.
 
Ukimtaja mtuhumiwa mmoja tu wa ufisadi wa mali ya umma ambaye ni jobless basi kauli yako hii itakuwa na mashiko.

ZeMarcopolo,
Kibogo,


Nimekwisha sema awali katika michango yangu humu jamvini, kwamba sifurahii kujibizana na wanaJF, hasa wale wanaotumia majina ya kificho (pseudonyms).

Lakini naona nj vema nimweleze Ndugu Kibogo kwamba mwaka 1979, Rais Nyerere hakunisimamisha kama Gavana wa BoT. U-Gavana niliachia April, 1974, Charles Nyirabu akanirithi, mimi nikaenda EAC kuwa Katibu Mkuu. EAC(Phase I) ilipovunyika 1977, Mwalimu akaniita Dar na kuniteua Waziri wa Fedha na Mipango. Baada ya vita vya Idi Amin, uchumi wa Tanzania ulivurugika sana, na Rais alipokataa ushauri wangu wa jinsi ya kuushughulikia, nilijiuzulu mwisho wa Novemba, 1979.

Ni kweli Rais alitangaza kuwa hakupenda sera za Benki ya Dunia au za IMF, ambazo nilizichambua na kurekebisha ili tutatue matatizo yaliyokabili nchi yetu. Lakini siyo sahihi kusema kulikuwa na kinyongo baina yangu na Mwalimu:

Miezi minne tu baada ya kuacha Uwaziri wa Fedha, Serikali ya Mwalimu iliniteua kuongoza Tanzania Development Finance Company Ltd (TDFL) kama Board Chairman. Inavyofahamika Septemba, 1982, Mwalimu mwenyewe alipendekeza niwakilishe Tanzania na Anglophone Africa katika IMF. Hizo siyo dalili za kinyongo kati ya Mwalimu na mimi!!! Nadiriki kujivuna kwamba Mwalimu alikuwa anapenda sana mienendo yangu, na mimi nilikuwa namheshimu na kupenda sana misimamo yake kwa jumla.

Kuhusu sera na misimamo yangu juu ya uchumi na fedha wakati ule, historia ya Tanzania imedhihirisha kwamba kama sera zile zingekubaliwa na kutekelezwa kuanzia 1980, labda hatungekumbana na zahama na matatizo yaliyotukabili karibu kwa miongo miwili baadae. Ni ukweli usiopingika kwamba ni baada ya mwaka 1986 ndipo tulianza kutekeleza baadhi ya zile sera. Wengi wa watekelezaji wakawa ni watu waliozipinga au wasioziamini au waliodandia tu ili wakwapue mali ya umma kwa maslahi binafsi. Kwa lugha ya kisasa tunawaita ni mafisadi.

Nimalizie kwa kudokeza kwamba nimejaribu kuandika katika kitabu cha Wasifu Binafsi (Autobiography) sababu zilizonifanya kujiuzulu; na pia kutoa muhstasari wa sera za Mwalimu Nyerere alipoiongoza nchi yetu. Nimekiita "From Goatherd to Governor" na kinachapishwa na kampuni ya Mkuki na Nyota ya Dar es Salaam.
 
Afadhali umejitokeza kutoa ufafanuzi Mzee wetu kipenzi. Pia Marco naimani ukweli wote ataupata kupitia kitabu,akisubiri tuu.
Cc: ZeMarcopolo
 

Asante Mzee Mtei, maelezo yako yametufungua na sisi wengine na yamejibu hoja
 
Afadhali umejitokeza kutoa ufafanuzi Mzee wetu kipenzi. Pia Marco naimani ukweli wote ataupata kupitia kitabu,akisubiri tuu.
Cc: ZeMarcopolo
 
Afadhali umejitokeza kutoa ufafanuzi Mzee wetu kipenzi. Pia Marco naimani ukweli wote ataupata kupitia kitabu,akisubiri tuu.
Cc: ZeMarcopolo

Kitabu changu From Goatherd to Governor kilichapishwa mwaka 2009 na Mkuki na Nyota Publishers, na kinapatikana katika maduka ya Bookshop Tanzania.
 
sasa mzee wetu mtei,embu tuambie baada ya mkwe wako ni mchaga gn mwingne atakuw mwenyekit?eti sikweli sis wachaga hatutaruhusu mwenyikit wa chama kuwa kabila tofaut na mchaga?wambie wajue,akitoka mbowe tunamuweka liliani mtei
 
sasa mzee wetu mtei,embu tuambie baada ya mkwe wako ni mchaga gn mwingne atakuw mwenyekit?eti sikweli sis wachaga hatutaruhusu mwenyikit wa chama kuwa kabila tofaut na mchaga?wambie wajue,akitoka mbowe tunamuweka liliani mtei

Unafukua mada zilizopitwa na wakati ili kujaribu kuondoa watu kwenye mjadala wa Kapuya ehhhh.....Pile sana...
 
Salaam JF ! Ni muda mrefu sana ndani ya chama chetu pendwa(CHADEMA)Kimekuwa kikipata kashfa nyingi sana ambazo kiukweli sisi kama wanachama tumejitahidi sana kukisafisha na kuonesha yako shwari tu hususani hapa JF iwe kwa matusi amma vyovyote vile.Binafsi nimekaa LEO nikajiuliza hivi ni kweli CHADEMA ni chama amma ni KITEGA UCHUMI cha watu FULANI."Yafuatayo ni mambo yanayonitatiza na kama kuna mtu ajuaye anitoe WASIWASI "!! 1.Mzee Edwin Mtei na Bob Makani baada ya kuondoka BOT walianzisha CHADEMA(Bob Makani alimuoa dada yake MTEI.Pia ndiye aliyekuwa M/KITI wa chama baada ya MTEI.2.Bob Makani alimuachia uenyekiti MBOWE.Mbowe kamuoa Mtoto wa MTEI. 3.Manunuzi yoyote ya Chama anafanya MBOWE akishirikiana na MTEI. 4.Fedha za msaada kwa chama zilijokua kutoka "Conservative" zilitumika kuanzisha Gazeti la Tanzania Daima-Leo hili ni Gazeti la MBOWE ! 5.Ruzuku,Misaada,michango ya wanachama na wadau(ROSTAM,SABODO na MKONO)Zinaishia makao makuu. 6.Viti maalumu wanagawana tu 7.Ofisi(Jengo La MTEI).WHY..?????
 
Porojo hizi saa nyingine zinachosha , eti Jengo la Mtei Makao makuu ya Chadema ? nafikiri kuna haja ya Chadema kuweha hati ya umiliki wa jengolao na jinsi wanavyolipia kodi ya jengo.

Kuna watu watakufa shinikizo la damu kwani waliyokuwawakielezwa na wasaliti sio ambayo leo wanayaona yakijitokeza kiuhalisia huko mitaani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…