Elections 2010 Mtei amwonya Kikwete

Mzee Mtei,
Kwa sisi tunaokufahamu hatukuhitaji maelezo yako. Hao wanaokusema wewe ni fisadi ama wanasema hivyo kwa kutokujua au kwa ajenda zao binafsi, au labda wanapotosha makusudi maana ya neno fisadi. Asante pia kwa kitabu chako kimeweka kumbukumbu za historia ambayo wengine
tulikuwa hatuifahamu. Mungu akubariki.
 
Kwa muda mrefu sikusoma/sikufungua kompyuta na kusoma yanayosemwa juu yangu binafsi. Leo ndiyo naona hii ripoti ya Asha Abdalla baada ya kuzungumza nami hapa nyumbani kwangu.

Nashukuru wanaJF wengi kwa kukubaliana nami kwamba nilikuwa mnyofu na muwazi ktk kutoa ushauri kwa Rais wangu. Nakubaliana na wale wanaodhani kwamba ni vema wazee walio na uzoefu wakachangia nao ktk mijadala.

Nikiri kwamba nimesikitishwa sana na matamshi ya wanaJF, kama William Malecela, kwamba mimi pia nilifanya mambo ya kifisadi.

Kwanza niseme kwamba mimi si tajiri. Hata katika kitabu nilichoandika na kuchapisha hivi karibuni "From Goatherd to Governor" nimeeleza jinsi nilivyoweza kununua shamba la Ogaden baada ya kujiuzulu Uwaziri wa Fedha mwishoni mwa mwaka1979. Shamba hili lenye ekari 52 tu lilibadilishwa na nyumba yangu ya Mzinga Way, OysterBay baada Mkadiriaji (Valuer) kukadiria thamani ya hiyo nyumba. Nimeeleza pia kwamba kwa miaka minne nilikuwa Executive Director wa IMF kwa kuteuliwa na Mwalimu Nyerere; na kwamba napokea pensheni toka Shirika hilo tangu nilipotimiza miaka 55; pamoja na ya Serikali ya Tanzania kutokana na utumishi wangu kama Permanent Secretary to the Treasury nilikostaafu kutokana na kuteuliwa Gavana wa Benki Kuu Januari 1966.

Najivunia kwamba siishi kwa kujititimua, na mke wangu pia hana makuu. Kwa hiyo tumeweza kusomesha watoto wetu waweze kujitegemea; na sasa sisi wenyewe tunaweza kuendesha maisha bila matatizo ya fedha.

Nieleze pia ni jambo la kusikitisha kwamba Watanzania tumedidimia kimaadili kiasi kwamba vijana wetu wengi, kama William , wana dhana kwamba mtu yeyote mwenye fedha ni lazima awe fisadi. Tunahitaji Mabadiliko ya kweli. Fursa ya kubadili imejitokeza sasa kutokana na CHADEMA, kumteua Dr. Slaa kugombea u-Rais. Ni excitement hii ya kwamba INAWEZEKANA KULETA MABADIKO YA KWELI yamenifanya kama Muasisi wa hiki chama nikose kusoma thread hii mapema.

Mzee Mtei achana William Malecela kwani tangu baba yake alipopigwa kura za maoni haonekani tena JF lakini rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa badala yake kwa sababu ya aibu kakimbilia facebook. Msamehe kwani hajui alitendalo kwa kukutukana mzee wetu.
 
Kwa yoyote anayependa kumwelewa Mzee Mtei vizuri, na mchango wake Tanzania, asome kitabu chake "From Gotherd to Governor". I highly recomend it. It is extremely readable, and moving. I shed tears many times as I read it.

Laiti Mwalimu angesikiliza ushauri wa Mzee Mtei kwamba tukubaliane na IMF wakati ule kabla hatujawa mahututi. Tulikaidi (kwa madai kwamba hatuwezi kuwa jiwe) na tukalazimika kukubaliana nao baada ya kuwa mahututi. Yaani ni kama mgonjwa anayekaidi dawa mpaka afike kwanza ICU.
 
hivi kikwete tatizo ni yeye au wasaidizi, rjea mfano wa Sadam husein selikali ilikuwa ni yeye, kutokana na ukali wake mambo yalienda,rejea baba wa taifa yeye kama mkuu wa nchi ndo alifanya mabo yaende. sasa kwa kikwete mbona tunapindisha lawama? kama wasidizi ni wabovu mbona hawachukulii hatua? maji na mafuta daima huwa havikai pamoja, vinavyokaa pamoja ni vitu vyenye asili moja so kikwete na wasaidizi wake wote wabovu na lao ni moja. huamini rejelea tuhuma za EPA alizozitoa marando
 
[
Fursa ya kubadili imejitokeza sasa kutokana na CHADEMA, kumteua Dr. Slaa kugombea u-Rais. Ni excitement hii ya kwamba INAWEZEKANA KULETA MABADIKO YA KWELI ifikapo Oktoba 2010 yamenifanya, kama Muasisi wa hiki chama, nikose kusoma thread hii mapema. WanaJF nawaomba radhi kwa ku-comment so late.

Mzee Mtei,

Kwa heshima zote inatia moyo kuona unaongelea suala la maadili na pia inawezekana kuleta mabadiliko ya kweli. Lakini ni kweli unaamini kwa dhati kuwa kumchagua Dr Slaa ndio utakuwa ufunguo wa mabadiliko ya kweli haswa katika upande wa maadili?

omarilyas
 
Laiti Mwalimu angesikiliza ushauri wa Mzee Mtei kwamba tukubaliane na IMF wakati ule kabla hatujawa mahututi. Tulikaidi (kwa madai kwamba hatuwezi kuwa jiwe) na tukalazimika kukubaliana nao baada ya kuwa mahututi. Yaani ni kama mgonjwa anayekaidi dawa mpaka afike kwanza ICU.

Hivi kati ya nchi zilizokubali kuwapigia magoti hao proxies wa Washington Consesus ni ipi ambayo iliepuka huo umahututi?

Mwalimu aliamini kwa dhati katika ujamaa, iweje mtegemee akubaliane na ushauri wa kuwapigia magoti the very people ambao walifanya wazi kuwa nia yao kuu ni kuhakikisha kuwa ujamaa haufanikiwi.......Hivi hadi sasa baada ya kukubali kufakamia huo ubepari ni nini kimeongezeka zaidi ya ulimbukeni wa tabaka tawala?

omarilyas
 
Mzee Mtei,

Kwa heshima zote inatia moyo kuona unaongelea suala la maadili na pia inawezekana kuleta mabadiliko ya kweli. Lakini ni kweli unaamini kwa dhati kuwa kumchagua Dr Slaa ndio utakuwa ufunguo wa mabadiliko ya kweli haswa katika upande wa maadili?

omarilyas

Mkuu sidhani kama mtu mmoja anaweza kuleta mabadiliko peke yake. CHADEMA as political party naamini inaweza kurudisha maadili kwenye utawala. Inaweza kufanya kazi hiyo vizuri zaidi ikiwa serikalini.

Sasa hivi kila mtu anajua kuwa serikali ni kama haina msemaji, chama cha mapinduzi ni kama hakina msemaji. Katibu mkuu wa chama ambaye ni kiongozi mkubwa anaonekana kuwa mwongo (issue ya Bashe), at keast ujinga kama huu CHADEMA haupo. Hata kama upo basi si mkubwa.
 
Hivi kati ya nchi zilizokubali kuwapigia magoti hao proxies wa Washington Consesus ni ipi ambayo iliepuka huo umahututi?

Mwalimu aliamini kwa dhati katika ujamaa, iweje mtegemee akubaliane na ushauri wa kuwaigia magoti the very pople ambao walifanya wazi kuwa nia yao kuu ni kuhakikisha kuwa ujamaa haufanikiwi.......Hivi hadi sasa baada ya kukubali kufakamia huo ubepari ni nini kimeongezeka zaidi ya ulimbukeni wa tabaka tawala?

omarilyas

classic! kuna watu wanataka tuamini tu bila hata kuhoji kuwa endapo tungefanya kila kitu ambacho IMF imetushauri kufanya tusingekuwa hapa tulipo. Well.. miaka 25 iliyopita tumefanya kila kitu ambacho WB, IMF, UNDP, UNICEF, ADB na wenzake wanayotaka tufanye je tunaweza kusema kweli hali yetu ni bora zaidi? Kufanya yote ambayo Mtei alishauri isingekuwa a panacea ya matatizo yetu kama taifa. Ingekuwa just that - tumefanya tuliyoambiwa na wakubwa kufanya hata kama hayakubaliani na misingi yetu kama taifa. Pamoja na heshima yangu yote niliyonayo kwa Mzee Mtei leo hii mapendekezo yake yamefanyiwa kazi kuanzia Mwinyi hadi Kikwete, ameridhika?
 
Mzee Mtei,

Kwa heshima zote inatia moyo kuona unaongelea suala la maadili na pia inawezekana kuleta mabadiliko ya kweli. Lakini ni kweli unaamini kwa dhati kuwa kumchagua Dr Slaa ndio utakuwa ufunguo wa mabadiliko ya kweli haswa katika upande wa maadili?

omarilyas

Inategemea bila ya shaka tunazungumzia "maadili" gani. Kwani kuna maadili kama miiko na misimamo ya kiuongozi yenye kuzingatia nini ni bora, cha haki, na cha usawa katika utumishi yaani tunakijua kama "ethics" na kuna maadili tunayoyazungumzia kama masuala yanayotokana na uelewa wa kidini na maisha kuhusu uovu na wema yaani "morality". Hivi vitu viwili japo vyote kwenye kiswahili tunaviita ni "maadili" kimsingi siyo kitu kimoja.

Maadili (ethics) za kiungozi siyo lazima zifanane na kulingana kabisa na maadili (morality) ya maisha au kiimani. Hapa ndipo wengi wanapopotoka kwamba kwa vile mtu ni mlevi wa pombe (suala la morality) basi anaweza asiwe mtu mzuri kusimamia fedha za umma (ethics). Mtu ambaye ameoa mke mmoja, ameacha, ameeenda nje ya ndoa yake (morality) si lazima awe mtu ambaye ataachilia raslimali zetu ziuzwe kama njugu, kuruhusu wageni na wenyeji wale njama kuiba toka benki kuu (ethics).

Tukielewa tofauti ya haya, ushahidi unaosimama mbele yetu ni kuwa Dr. Slaa anaweza kuhojiwa kwenye suala la personal morality (maadili binafsi) na tukasema hatukurudhika na maamuzi au matendo fulani lakini haiwezi kutulazimisha tufikiria kuwa ameshindwa pia katika maadili ya umma (public ethics). Kati ya yeye na uongozi ulioko madarakani leo hii nitamchukua siku yeyote mtu ambaye anahangaika na maadili ya binafsi kwani ni sehemu ya maisha yetu ya kibinadamu (a human condition) kuliko kumkumbatia mtu aliyejionesha kushindwa katika maadili ya umma ya utumishi. Hicho cha mwisho kinaamua maisha ya mamilioni yanakuwaje.
 
Kaka nahofia kuchangia kwa upana zaidi suala hili hadi uchaguzi upite lakini ni kweli unaamini kuwa Personal Ethics/Maadili/Nidhamu binafsi hazina mahusiano na Public Ethics/Madili ya Umma/Madili ya Uongozi??
 
classic! kuna watu wanataka tuamini tu bila hata kuhoji kuwa endapo tungefanya kila kitu ambacho IMF imetushauri kufanya tusingekuwa hapa tulipo. Well.. miaka 25 iliyopita tumefanya kila kitu ambacho WB, IMF, UNDP, UNICEF, ADB na wenzake wanayotaka tufanye je tunaweza kusema kweli hali yetu ni bora zaidi? Kufanya yote ambayo Mtei alishauri isingekuwa a panacea ya matatizo yetu kama taifa. Ingekuwa just that - tumefanya tuliyoambiwa na wakubwa kufanya hata kama hayakubaliani na misingi yetu kama taifa. Pamoja na heshima yangu yote niliyonayo kwa Mzee Mtei leo hii mapendekezo yake yamefanyiwa kazi kuanzia Mwinyi hadi Kikwete, ameridhika?

Pamoja na kukubali....tunge-improve vipi......ilhali na Azimio la Arusha (maadili) tukalitia kapuni............na kuleta Azimio la Zanzibar.......watu walishaona prospects za ufisadi na kutafsiri vibaya.......sera za ubepari i.e UFISADI............
 
-
- Ninarudia hivi tukiendelea kuangalaiana usoni, basi tutaimba ufisadi mpaka mwisho wa dunia, DK. Salim angekwua na hela unzosema angeshinda urais 2005, moja ya sababu kubwa iliyomkosesha urais ni umasikini uliza wapambe wake Mzee Warioba, Butiku na Ndejembi watakuelimisha sana mkuu kuhusu hili.

William.

Dr Salim ...sio kwamba alishindwa urais kwa kukosa pesa binafsi.....ila kwanza hakutaka kuharibu deginity yake kwa kutoa rushwa....,infact ndie mgombea pekee ambaye mwaka 2005 ambaye alikuwa hagawi,...pesa...na hata kwa kura alizopata ukizingatia hakutoa rushwa ..ukijumlisha na hujuma za kikwete kwa kuwatumia wazee wa mapinduzi ni wazi kikwete alikuwa hamuwezi ...iwapo sio zile hujuma leo hii tungekuwa na rais msafi SALIM AHMED SALIM.....i always say that this guy will remain the president of our hearts,.......

Kuhusu uadilifu wa MZEE MTEI....Hilo halina mjadala ....hata mwalimu alikuwa akimuheshimu...nadhani kuna watu hawataki kukubali kuwa kuna wazee nchi hii ambao hawakuwa malaika lakini legacy zao hazipingiki....,aidha kwa uadilifu wao au msimamo wao binafsi.....hapo hutawakosa watu kama Salim,mtei,warioba.,kawawa.etc...pamoja na juhudi za wazi za kuchafua legacy za watu ili wote waonekane wabaya ,..ukweli unajulikana,,,...

Tusipende kujivunia umasikini...ni wazi uadilifu wa mtu unaanzia kwenye uwezo wa ku manage uchumi wake binafsi....ndio maana watu kama chediel mgonja na moses nauye pamoja na kuwa wamekufa maskini huwezi kuwaweka kwenye kundi la uadilifu kwa kuwa walishindwa hata kutumia kipato chao halali ...fikiria mshahara wa waziri ,na marupurupu....,lakini bado wakashindwa kujisitiri kwenye mahitaji muhimu....ambapo msiba wa mgonja ukafanyikia kwa shemeji yake IBRAHIM kaduma.....na wa NNAUYE kwa rafikiye MAKAMBA........Chediel kama kaduma alipata kuwa waziri kwa muda mrefu ikiwemo nafasi nyeti ya waziri wa nje..........lakini hadi anakufa alikuwa akifedheheka kwa kupanda daladala..baada ya gari yake ya ubunge aliyokuwa akiitumia kusanyia kama daladala akiendesha mwenyewe kuharibika..mzee Ibrahim Kaduma sio fisadi na ni kundi la viongozi wa mfano nchi hii ..si tajiri..kwa viwango vya leo lakini kwa mshahara wake aliokuwa akipata wa uwaziri anaishi maisha mazuri..aliyojiandalia............uadilifu lazima uanzie kwenye kuweza kujimiliki mwenyewe....
 
Mwanakijiji said:
classic! kuna watu wanataka tuamini tu bila hata kuhoji kuwa endapo tungefanya kila kitu ambacho IMF imetushauri kufanya tusingekuwa hapa tulipo. Well.. miaka 25 iliyopita tumefanya kila kitu ambacho WB, IMF, UNDP, UNICEF, ADB na wenzake wanayotaka tufanye je tunaweza kusema kweli hali yetu ni bora zaidi? Kufanya yote ambayo Mtei alishauri isingekuwa a panacea ya matatizo yetu kama taifa. Ingekuwa just that - tumefanya tuliyoambiwa na wakubwa kufanya hata kama hayakubaliani na misingi yetu kama taifa. Pamoja na heshima yangu yote niliyonayo kwa Mzee Mtei leo hii mapendekezo yake yamefanyiwa kazi kuanzia Mwinyi hadi Kikwete, ameridhika?

Mwanakijiji,

..mkuu nchi ilikuwa na hali mbaya sana ya uchumi na tusingeweza kuendelea na sera zilizotufikisha pale.

..naamini mapendekezo ya Mzee Mtei yalikuwa na lengo ya kuokoa uchumi usiharibike zaidi.

..naamini hatua zilizochukuliwa kutokana na mapendekezo ya Mtei zilipaswa kuwa "a tactical-retreat" ili baadaye tuweze kujenga uwezo wa kufanya maamuzi yetu wenyewe.

..sasa hivi serikali inaweza kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo[maji mkoani musoma,udom..] kwa kutegemea mapato ya ndani, kitu ambacho kilikuwa ni cha kufikirika tu miaka ile ya uhaba wa kila kitu--sukari,chumvi,na mafuta ya kupikia.

..mmomonyoko wa maadili ya viongozi ni suala ambalo halivumiliki ktk mfumo wowote ule wa utawala, iwe ni ujamaa, au hata ubepari.
 
Philemon Mikael,

..watu wengine hawana kipawa cha ku-manage hela.

..Thomas Jefferson, raisi wa pili wa marekani, alikufa akiwa amefilisika, na ilifika mahali hata watumwa wake wakapigwa mnada.

..masuala ya uongozi na utunzaji pesa ni vitu viwili tofauti kabisa.

..huwezi kuanza kuonyesha dharau kwa watu kama Nnauye, Mgonja, etc etc kwasababu tu walipofariki walikuwa na hali mbaya kiuchumi.

..Chediel Mgonja ninavyoelewa mimi ana nyumba yake amejenga maeneo ya Same. mauti yangemkuta nyumbani kwao Same, basi lazima msiba ungefanyika nyumbani kwake.

..kuna viongozi sasa hivi watafariki na shughuli za mazishi yao zitafanyika kwenye majumba ya kifahari hapa mjini lakini kila mtu anajua majumba hayo ni ya wizi. chukulia mfano hizi nyumba za serikali walizojiuzia. sasa si ni bora mara mia hao wakina Nnauye,Mgonja,etc etc.
 
classic! kuna watu wanataka tuamini tu bila hata kuhoji kuwa endapo tungefanya kila kitu ambacho IMF imetushauri kufanya tusingekuwa hapa tulipo. Well.. miaka 25 iliyopita tumefanya kila kitu ambacho WB, IMF, UNDP, UNICEF, ADB na wenzake wanayotaka tufanye je tunaweza kusema kweli hali yetu ni bora zaidi? Kufanya yote ambayo Mtei alishauri isingekuwa a panacea ya matatizo yetu kama taifa. Ingekuwa just that - tumefanya tuliyoambiwa na wakubwa kufanya hata kama hayakubaliani na misingi yetu kama taifa. Pamoja na heshima yangu yote niliyonayo kwa Mzee Mtei leo hii mapendekezo yake yamefanyiwa kazi kuanzia Mwinyi hadi Kikwete, ameridhika?

Mwanakijiji ukumbuke kuwa SAPs zilisaidia sana kufufua uchumi wa taifa. Ukumbuke Mwinyi alichukua nchi katika hali gani. tulikuwa hoi kwelikweli. Sasa hivi watu wengi wanasahau kuwa reforms and adjustments zilisaidia sana kutuodnia kufani. Tulikuwa na matatizo makubwa sana, sukari, sabuni, nguo, viatu, na mahitaji yote ya msingi yalikuwa adimu sana, kuna wakati mtu unakuwa na hela lakini duka la kaya lilikuwa halina kitu, ukinunua toka nje ya nchi kilitwa cha magendo na uliweza kupelekwa ndani, TV, radio gari ilikuwa ni kama kosa la jinai. Cellphone ilikuwa ndoto kabisa. RTC, NMC yalikuwa kama makaburi ya uchumi wetu.

Tulikuwa na serikali kubwa kupita kiasi, na kama utakumbuka hata akiba yetu ya fedha ilikuwa mbaya sana. Hali ilianza kubadilika baada ya kutekeleza SAPs. Ukiangalia kwa undani package ya SAP ilikuwa na lengo la kufufua uchumi ili upate nguvu ya kuweza kujiendeleza wenyewe, although in a process wengine tuliumia, na wengine kama kina JK na Kinana wakaamua kuacha jeshi na kuingia CCM. Sipigii debe IMF, WB na OECD kwa kuwa ushenzi wao unafahamika sana, lakini kwa kiasi fulani naweza kusema walitusaidia. Weakness bado iko kwetu, viongozi wetu hawaijali Tanzania hawana uzalendo, wanajali mifuko yao na akaunti zao, hata elimu waliyopata wanaitumia kujineemesha wao, sio kuiendeleza Tanzania. Kama kweli kungekuwa na lengo la kuiendeleza Tanzania, na elimu iliypo sasa miongoni mwa watanzania tungekuwa tumepiga hatua sana.

Ni vizuri sana tukiacha kulalamikia wengine wakati uozo mwingi uko ndani, Mwanakijiji sijui lini last time ulikuja Tanzania, unatakiwa uone uozo wa idara zetu za utendaji, uozo wa siasa zetu, na matatizo kwenye sturctures zetu. Ajabu ukiwaliza watu wanasema oh Tanzania today is not like that of 10 years ago, just a pack of crap, wanadanganyika kwa kuweza kuwa na simu za mkononi na laptop, lakini kila kitu kinaenda hovyo. Kitulacho ki nguoni mwetu, hakiko Washington wala London.

IMF, Donors na WB walituacha tujumanage baada ya kuona awamu ya tatu was doing "well" at least in term of implementing SAPs, waliona kama Tanzania ina mwelekeo mzuri and there was even a talk that TZ itakuwa bora zaidi, wakiamini kuwa tumeanza kutumia watanzania waliosoma kumanage uchumi wetu. Lakini awamu ya nne imevurunda kila kitu, tofauti sana na awamu ya tatu. Sasa hivi kuna sera nyingi sana za porojo, kama vile kilimo kwanza, maisha bora kwa kila mtanzania, lakini ukiangalia structures zote zilizopo ambazo zilitakiwa kufanikisha sera hizi ni kama zimekufa. Hakuna kitu kinachoitwa social welfare Tanzania at least in practical terms, angalia structures za wizara nyingi uone kama kweli zimetengenezwa ku deliver the goods. Nyingi unaona ni madawati tu ya kuchumia pesa ya maofisa wa wizara.

Hakuna political leadership inaweza ku-direct, kusupervise na kumanage mwelekeo wa nchi, hii sio siri. They talk about maisha bora lakini hakuna definition of it na targets za maisha bora, they talk about kilimo kwanza as new policy, wanasahau kuwa sera hiyo ni ya zamani sana. JKNyerere alituwekea mabwana shamba kutoka national level hadi village level, aliweza hata kuanzisha UFI (KIZAKU), TRAMA, TFA, kiwanda cha mbolea, tulikuwa na kitu kinaitwa Tanganyika packers, chakula barafu and things like that, serikali yake kweli ilikuwa inatekeleza sera hiyo...today they are fooling us na Kilimo kwanza as if tumesahau real kilimo kwanza. Tunafanywa watoto halafu na sisi tunapiga makofi.

Kwa hiyo Mwanakijiji, pamoja na ukweli kuwa IMF, WB can be questioned, bado Tanzania haijafikia hatua hiyo. We have to put our house in order first before we turn our guns to IMF and WB. Kuna mambo mengi sana tunayoweza kufanya as a country hatujafanya, hata kodi tu tunazotakiwa kukusanya hatukusanyi, hata wezi tunaowajua EPA, Kagoda, Radar tunawachekea, how can we be so brave to pint fingers at bretton wood institutions???

Kama awamu ya nne ingeendelea kujenga ilipofikia awamu ya tatu, ingesahihisha makosa ya awamu ya tatu, kweli tungekuwa tumepiga hatua zaidi. Tatizo ni kuwa wameleta matatizo zaidi na kutufanya tuone kuwa awamu ya tatu was better by far than ya nne. Lakini usishangae kusikia kuwa wameingia ena madarakani.
 
..sasa hivi serikali inaweza kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo[maji mkoani musoma,udom..] kwa kutegemea mapato ya ndani, kitu ambacho kilikuwa ni cha kufikirika tu miaka ile ya uhaba wa kila kitu--sukari,chumvi,na mafuta ya kupikia.

Hivi UDOM inajengwa kwa mapato ya ndani? Nilifikiri ni mkopo wa ndani kwa kupitia NSSF, PPF etc...But also haya mashirika si mashirika ya umma ambayo ni mabaki ya sera za ujamaa?

Suala la kukosekana sukari, chumvi etc naamini lilitokana na sababu mbili kuu. Moja ni hujuma ya walanguzi kuficha bidhaa ili wauze kwa bei za jjuu na pili ni kukosekana na fedha za nje (foreign currency). Katika hili la kukosekana kwa foreign currency naamini kuwa hata hivi sasa endapo hao IMF na Wb watatunyima mikopo holela na pia hayo mataifa yaliyotulazimisha kufakamia ubepari yakakata misaada ni wazi tutarudi katika hali kama ile tena wakati huu tusiwe na hata mkono wa dola kusaidia masikini abao wameongezeka kuliko enzi zile...
 
Omarilyas,

..NSSF/PPF ya miaka hiyo isingeweza kutoa mkopo wa kiasi cha kujenga UDOM.

..pia ipo miradi mbalimbali ambayo serikali sasa hivi inachangia kwa kiwango kikubwa kuliko mwanzo.

..mapendekezo ya Mtei pamoja na mambo mengine, yalikuwa na nia ya kuyaokoa mashirika yaliyoanzishwa wakati wa Ujamaa.

..tungechukua hatua mapema tungeokoa mashirika mengi zaidi.

..kuhusu suala la walanguzi ni kwamba lazima kuwe na uhaba wa bidhaa kwanza ndipo walanguzi wanashamiri.

..again, mimi hoja yangu ni kwamba mapendekezo ya Mtei yalikuwa na nia ya kutuletea ahueni na kutuwezesha kujipanga upya ili tuweze kusonga mbele kiuchumi.

..sasa hivi hatuwezi kumlaumu Mtei tena, pia hatuwezi kumlaumu Mwalimu Nyerere. kinachotuangusha sasa hivi ni sera na uongozi mbaya wa CCM na Jakaya Kikwete.
 
- Wakuu samahani sana naomba kuuliza swali kidogo tu na linaweza kua nje ya mada, hivi kwa standard za ufisadi sasa hivi katika nchi yetu Tanzania, Mzee Mtei binafsi, hawi fisadi pia?

- I mean mali yote aliyonayo ambayo aliikusanya akiwa katika uongozi mbali mbali wa taifa letu, ni kweli haina ufisadi kabisaaa? Kama inayo anapata wapi moral authority ya kum-lecture rais wetu wa sasa kuhusu ufisadi wakati yeye ni mmoja wa waanzilishi wa ufisadi, kama sikosei katika taifa letu, au?

- Ninafahamu kwamba aliwahi kufanya kazi nje, lakini hivi mbona hata wakina Dk. Salim, waliwahi kufanya kazi nje lakini hawana mali za ajabu kama za huyu Mzee wetu muhasisi wa upinzani nchini?

- Ahsanteni Ndugu Zangu na Pasaka njema Sana.

William.

Nakushauri kaangalie uwekeji wa Mzee Mtei kwanza. Pia unaweza kutuambia tu iwapo alifanya ufisadi wapi wa kitu gani na kiasi gani na lini? Hao wanaohusishwa na Kikwete ushahidi ulitolewa hadharani wakashindwa kujitetea na hawakwenda mahakamani kama walivyotishia.
 
Back
Top Bottom