Mtei amwonya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtei amwonya Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Asha Abdala, Apr 12, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na Mussa Juma

  GAVANA wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania(BoT) na aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Edwin Mtei amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete atakabiliwa na matatizo makubwa kama hatakuwa mkali na kuwachukulia hatua watendaji wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake eneo la Tengeru, mkoani Arusha mwanzoni mwa wiki hii, Mtei alisema baadhi ya wasaidizi wa Kikwete watasababisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kianguke katika uchaguzi mkuu mwakani kutokana na kuchafuliwa na tuhuma mbalimbali.

  Mtei alisema wasaidizi wengi wa Kikwete hawaaminiki tena katika jamii, hivyo wananchi watapiga kura za hasira ili kuing'oa CCM madarakani.

  “Ni vyema Rais Kikwete akawatazama upya wasaidizi wake, kwani wengi hawamsaidii na kama ataendelea kucheka nao nchi hii inaelekea pabaya, hivyo lazima akubali kuchukua maamuzi magumu kama anataka mambo yawe mazuri,” alisema Mtei.

  Alisema hali inakoelekea nchi yetu imewahi kutokea katika nchi nyingi ambako viongozi wake wameondolewa madarakani kwa kushindwa katika uchaguzi kutokana na kucheka na wasaidizi wao wazembe na wabadhilifu, badala ya kuwachukuliwa hatua kali.

  Mtei ambaye pia ni muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alitoa mfano wa serikali ya chama tawala cha KANU, nchini Kenya kuwa kilikosa mwelekeo kutokana na viongozi wake kujaa tuhuma mbalimbali chafu.

  Kuhusu watalaam kukimbia nchi, alisema inachangiwa na mfumo mbaya wa malipo ya kustaafu ambao hauwiani na mishahara yao.

  “Tanzania kuna wasomi wazuri, lakini wanaikimbia nchi kwa sababu mishahara yao ni midogo sana na wakistaafu hawana uhakika wa maisha mazuri, tofauti na wanasiasa,” alisema Mtei.

  Alisema kuna mambo mengi ya msingi ambayo yanapaswa kufanywa na Rais Kikwete, ikiwemo kuwa na mijadala ya kitaifa itakayosaidia kutoa suluhisho kwa matatizo yanayoikumba nchi, ili kuondoa tabaka kwa Watanzania wachache wanaoneemeka na rasilimali za nchi, huku kundi kubwa likibaki katika hali ya umasikini.

  Mtei alisema Mwalimu Nyerere, aliweza kuongoza vema kutokana na kuwa mkali na hakusita kuchukua hatua dhidi ya kiongozi yoyote alipopata tetesi kwamba, anahusika na ubadhilifu.

  “Mwalimu alikuwa anatuita na kutueleza kwamba,Tanzania kuna watu zaidi ya milioni 20 (wakati huo) wenye uwezo wa kushika nafasi za uongozi, hivyo yoyote kati yetu kama sio msafi atatoka na aliwaondoa wengi,” alisema Mtei.

  Mwanasiasa huyu mkongwe, alisema si vizuri Rais Kikwete kuwa na msaidizi ndani ya serikali au chama ambaye anatiliwa shaka na wananchi.

  “Ndio maana wakati wa Nyerere, viongozi wengi walikuwa wanakimbia nchi, kwani ikibainika tu kuna dosari ni lazima mhusika atachukuliwa hatua haraka,” alisema Mtei.

  Alisema ni aibu, hivi sasa unasikia kuna kiongozi ana fedha nje ya nchi zenye utata,lakini hakuna hatua zinachukuliwa; jambo ambalo halikuwahi kutokea wakati wa Nyerere.

  “Wakati ule Benki Kuu ndiyo ilikuwa inahusika na uchunguzi wa fedha nje ya nchi na tulipobaini kuwa mtu fulani ana fedha nje, tulikuwa tunampa taarifa mwalimu na yeye alikuwa mkali sana na kuchukuwa hatua haraka,” alisema Mtei.

  Alisema baaada ya kupitishwa Azimio la Zanzibar lililoua Azimio la Arusha, hakuna tena miiko ya uongozi na viongozi hawana woga wa kufanya biashara jambo ambalo pia ni hatari kwa taifa.

  “Nampongeza Rais Kikwete kwa kubaini hili na kutoa utaratibu wa mtu kuchagua moja kati ya siasa na biashara, hili ni jambo zuri na katika nchi hizi masikini ni lazima kuwepo miiko ya aina hii,” alisema Mtei.

  Akizungumzia kashfa ya ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Dowans, Mtei alisema wakati wa Nyerere jambo hili lisingewezekana hata kujadili.

  “Wakati ule kama kampuni yako au shirika likibainika tu linajihusisha na rushwa katika masuala haya ya manunuzi kulikuwa na faili jeusi la makampuni na ikiingizwa humo huwezi kupewa kazi yoyote ya serikali bila kibali maalumu cha waziri wa fedha,” alisema Mtei.

  Alisema kwa suala la Dowans ni wazi, kampuni hiyo ina uhusiano na Kampuni ya Richmond hivyo kuingilia katika mjadala wa kununua mitambo ambayo tayari iliwahi kutiwa doa ni jambo lisilopaswa kupewa nafasi hata ya kujadiliwa.

  Akizungumza mfumo wa maslahi ya watumishi wa umma; alipendekeza kuwa Rais Kikwete aunde tume maalum ya kupitia mishahara na marupurupu yote ya watumishi wa umma.

  “Hivi sasa hakuna uwiano katika malipo, kuna watu wanalipwa fedha kwa siku moja ambayo ni malipo ya mshahara wa mwezi wa mtumishi mwingine jambo ambalo lazima litazamwe,” alisema Mtei.

  Alifafanua kwamba, hata mfumo wa malipo ya wastaafu unapaswa kurekebishwa ili ulingane na malipo ya wastaafu wa ngazi za juu serikalini.

  “Tunapaswa kuwa na mfumo ambao utamwezesha mstaafu kuishi maisha mazuri na sio kufa baada ya kustaafu,” alisema Mtei.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa hawa ndio wazee, wasomi wenye busara na lugha ya kuweza kuongoza..kwani wapo wengi tu wanaoweza kuyaona makosa wakashindwa kujenga hoja ya tiba sawa na waganga wa Kienyeji!..
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hapa angalia tofauti ya hekima na busara anayoitoa Mzee Mtei, isiyokuwa na ushawishi wa kisiasa bali mapenzi ya nchi na utaifa. Je unaweza kufananisha busara zake na zile pumba zilizotolewa na wale wazee waganga njaa wakina Ndejembi?
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ushauri kama huu wa Mtei ni rahisi kweli mtu kuupokea na kuufanyia kazi maana haujaongozana na vijembe vya kisiasa na unaangalia facts zilizopo.

  Rais alitakiwa kuwa karibu na wazee kama hawa ili apate upande mwingine wa shilingi. Ushauri mzuri ni ule unaotoka kwa watu ambao hawategemei mlo toka kwako. Mwenye njaa hawezi kuwa na mawazo huru hata siku moja.

  Mzee Mtei kaongea mambo yote ambayo ni ukweli mtupu.
   
 5. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,399
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Charismatic/innocent, hagangi njaa! Angalia tuna wasomi wazuri kabisa; nice words; siyo kama yule mzee wetu wa Glasgow ambayo maisha yake yote ni kuganga njaa yake "by sleeping with a devil!"
   
 6. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145

  au unakuta mzee anajenga haraka haraka wakati akiwa anataka kustaafu unashindwa kuwelewa kwa nini hakufanya hivyo siku zote

  wazee wengi wamekufa sana baada ya kustaafu
  jamani hii inasababishwa na kipato au watu kuwa boored na kutokujuwa wafanye nini ili mda uwende
  au ni shock to the system ndio inawauwa
  embu nisaidieni kimawazo kwa hili...
   
 7. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pension anayopata mfanyakazi wa kawaida tofauti na mwanasiasa inatofauti kubwa sana kiasi cha kutomtosha mtumishi huyu akiwa mstaafu. Kwa jinsi hii hujikuta akishindwa kumudu mahitaji aliyokuwa akiyamudu wakati akifanya kazi. Hii ndio husababisha mawazo mengi na kukata tamaa ya maisha na ndio husababisha vifo.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni ushauri unaoonyesha mapenzi kwa nchi yake. Hakuwa na tamaa ya kutumia udhaifu aliouona katika chama tawala na serikalini kwa ajili ya kuimarisha chama alichokiasisi. kama akina Ndejembi wangekuwa na na moyo kama huu, nchi hii ingeweza kusomga mbele kwa kasi kuliko inavyokwenda hivi sasa
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Nampongea sana mzee wetu ametoa ushauri mzuri sana...kazi kwake mkwere kuamua kuufanyia kazi au kama kawa anauchuna maana ndio style yake uongozi....
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Akina Ndejembi waliojipachika heshima ya 'Wazee wa CCM' na kutumia vitisho na ubabe kutaka kuwanyima haki wanaCCM wanaotaka kugombea nafasi ya Urais 2010 eti kwa kuwa wana utamaduni wao wa kuachiana Rais wa kutoka chama chao akae madarakani kwa vipindi viwili kwa sababu 'kafanya mazuri' ukiwauliza ni mazuri yapi aliyoyafanya wayaorodhoshe, wanang'aa macho!!!!! Kuwa na makundi ndani ya CCM na kuyumba kwa chama hicho ni dalili nyingine ya uongozi duni wa Kikwete.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Hahusiki na lolote huyu Kikwete, hakuhusika katika mjadala wa vitambulisho, Dowans ingawaje alitaka ufungwe, hata huu wa kuruhusu ama kutoruhusu wanaCCM wanaotaka kumpinga 2010 nao hahusiki!!!!
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyu hana haja ya kubwabwaja yeye ndio alikuwa gavana taratibu alizoziacha ndizo zilizofuatwa hawa na akina jamal pamoja na Nyerere ambae alikufa baada ya kukosa fedha yake aliyoiweka kwa Jamal,Maana jamal alipofariki , Nyerere akamfuata mke wa Jamali na kumwambia kuwa kuna feza alimpa jamali amuekee ,Mama akang'aka na kusema hakuniambia kama kuna feza yako ,hivyo sijui zilipo wala sina habari nazo niondokee sitaki maneno mume nafariki wewe nadai feza baada ya hapo Mwalimu alipandwa na pressure na kuugua maradhi na hakuweza tena kuhimili maisha.

  Sasa Mtei anamshauri Kikwete hivi kwanini asiseme kuwa serikali ya Kikwete haifai na ajiuzulu mara moja ,kuliko kuzunguka huku na huko ,Mtei ni mwoga nae anaganga kula yake ,hivi ni kweli yeye halipwi mafao ? Ni miaka mingapi toka aachane na Ugavana ,Je leo ndio anawakumbuka wengine au nae njaa imeanza kumpata ?

  Kulipata katika Serikali hii hakupo ila kama wewe ni fisadi basi hata ukistaafu kibunda chako utatengewa lakini ,kwa wale wengine wafagia ofisi na wasafisha mji hao wakistaafu ,watadai mpaka wanaingia kaburini hakuna wanacholipwa ,huo ndio ukweli ,sasa Mtei kuzuka na kumlaumu Kikwete kuwa awe Mkali ,kwani hakumsikia alipotoa vitisho kule Zenji kuyalinda Mapinduzi ? Sasa ikiwa anaweza kuyalinda Mapinduzi anashindwaje kuilinda serikali yake iliyojaa viongozi walafi ? Bila ya shaka yeyote Kikwete nae atakuwemo kundini hivyo kusema Kikwete awachukulie hatua wenzake hilo haliwezekani , kama ni hatua basi Kikwete abwage manyanga na kuitisha Uchaguzi mpya ,zaidi kuendelea kwake hakuna sababu ya WaTanzania kuendelea kuichagua CCM ni kuikataa kwa kila kura ni lazima itumike hapana na ndio kwa upinzani ibaki CCM kutumia vyombo vya dola katika kujisimika maana hakuna njia nyingine.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..Hivi Mzee Mtei bado anaamini kwamba Raisi wetu uwezo anao, wanaomponza na kuharibu ni wasaidizi na washauri??
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Wakuu samahani sana naomba kuuliza swali kidogo tu na linaweza kua nje ya mada, hivi kwa standard za ufisadi sasa hivi katika nchi yetu Tanzania, Mzee Mtei binafsi, hawi fisadi pia?

  - I mean mali yote aliyonayo ambayo aliikusanya akiwa katika uongozi mbali mbali wa taifa letu, ni kweli haina ufisadi kabisaaa? Kama inayo anapata wapi moral authority ya kum-lecture rais wetu wa sasa kuhusu ufisadi wakati yeye ni mmoja wa waanzilishi wa ufisadi, kama sikosei katika taifa letu, au?

  - Ninafahamu kwamba aliwahi kufanya kazi nje, lakini hivi mbona hata wakina Dk. Salim, waliwahi kufanya kazi nje lakini hawana mali za ajabu kama za huyu Mzee wetu muhasisi wa upinzani nchini?

  - Ahsanteni Ndugu Zangu na Pasaka njema Sana.

  William.
   
 15. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Nnamwona mzee Mtei kuwa ni mtu mwenye "great vision" tangu akiwa na nyadhifa serikalini enzi hizo.

  Hii ni "key element" katika kutoa maamuzi ya hekima na busara.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio hapo ninapowashangaa watu humu ,wakiunga mkono kila kitu ,bila ya kuhoji ,yaani lazima watakuwa wamepata wasiwasi wakisoma hii iko na kuandika wewe,hawafahamu kuwa wafuasi wa Sultani CCM takriban wote ni mafisadi ,ila kila mmoja ana maficho yake ,wengine walichukua chao mapema sasa huwa wanamegua megua ili kutaka kuonekana kuwa wao ni wasafi.
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  William Malecela,

  ..ungesaidia sana kama ungezitaja mali za Edwin Mtei zilizopatikana kifisadi.
   
 18. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Sasa hili ni tatizo ambalo wewe ndie inabidi ulitatue kwa kutueleza jinsi mzee huyu alivyokusanya hio mali unayosema na ufisadi wake.

  Kumbuka kuna tofauti kubwa kati ya "fallacy" na "logic" na tofauti hio ni vigezo tu au "facts".

  Kwa hio mkuu tumwagie vigezo vyote vinavyothibitisha madai yako.

  Pasaka njema.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Richard,

  ..jamaa anataka kututoa kwenye mada na hoja ya msingi hapa.

  ..kama ana nia ya dhati ya kuzungumzia ufisadi wa Edwin Mtei basi angeanzisha thread mahsusi kwa ajili hiyo.

  ..hoja ya msingi hapa ni kwamba Raisi aliyechaguliwa yupo-yupo tu, na ameshindwa kuongoza nchi.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Na kama ziko ndani au nje ya nchi.
   
Loading...