Mtazamo wangu kuhusu Kiba na Mond

Mtazamo wangu kuhusu Kiba na Mond

mtazamo wako si mbaya lkn bado inaonekana umeegemea upande mmoja, mi niseme tu watanzania ifike mahali tubadilike , tufumbue macho na fikra zetu , na tuamue sasa kuwa kitu kimoja kwa mambo ya msingi na yenye kuleta tija na faida kwa mziki wetu hasa huu wa bongo fleva.

Niseme tu Diamond ni mwanamziki mzuri na Ali kiba vivyo hvy, kila mmoja wenu ana radha na vionjo tofauti hvy kuleta maudhui tofauti kwa wasikilizaji, kwa hvy kila mtu kuwa na mapenzi ya vionjo anavyotaka,na ninyi ni kati ya watanzania million 40 na ushehe , lkn watanzania wenzangu sisi tunatia aibu tunashusha ari na vipaji vya wanamuziki wetu , na tunajenga hofu kwa wanamuziki wetu,nchi ya watu milion 40 tunashinda kuwagombanisha wanamuziki wawili tu , kwa kuandika matusi na chuki sizizo na mantiki , diamond ni mwanamziki wa kitanzania na kiba tukiwapa nguvu wote maana ni kwamba tunaipa nguvu tanzania na kuwapa morali wanamuziki wengine pia.

Hz timu sisizo na tija kwenu Mond na Kiba mzikatae . leo zitaonekana ni bora sana kwenu lkn siku hazigandi hz timu ndio zitakozokuwa pilipili kwenu,kwa sasa hamtaona hilo leo ila jiulizeni tu wenzenu bongo muvi wapo wapi baada ya Kanumba?,mafanikio yenu ni faida kwa Tanzania nzima .VIVA DIAMOND VIVA ALI KIBA DUMISHENI UPENDO NA AMANI TANZANIA NI MOJA SISI NI WAMOJA IDUMU BONGO FLEVA NA WAINUA VIPAJI BONGO FLEVA?
 
Haya sasa tueleze wakati ambao Kiba anatoka na cinderela alitegemea bifu na nani? Hadi isiwezekane yeye kurudi sasa kisa bifu na diamond.

Kwa mara ya kwanza kutoka moyoni nakubaliana na wewe. Ukweli uliowazi kuwa Kiba ametoka kabla hata Diamond kujulikana. Amefanya collabo na msanii mkubwa RK kwa msaada wa dada 7.

Baada ya mafanikio hayo watu walianza kumchukia Kiba na kumwandika vibaya hasa magazeti ya udaku hadi wakammaliza kiusanii.

Ujio wa Diamond umeleta changamoto mpya, maadui wale wale wa Kiba wakaanza kumtandika Chibu. Mwanzo walitafuta watu wa kupambana na Diamond kama kumkweza Ommy Dimpoz, Barnaba, Ben pol na Rich Mavoko. Hawa wote walishindwa kutoa upinzani wa maana.

Ukubwa dawa, Kiba akaibuka tena, kwa kuwa uwezo wake ni mkubwa unanifurahisha kuleta changamoto katika hii tasnia ya muziki.

Kuna haja ya kuangalia mbali zaidi kwa kuangalia upande wa pili wa mapato yao. Je wanalipwa kulingana na hadhi zao au tunawasifu ili wawanyonye na kuwapa fedha kidogo ili waendelee kuwa watumwa wa sifa?

Nashauri mashabiki wa timubzote, baada ya kuisha kwa tuzo hizi sasa tutumie majukwaa haya haya kuwakemea wanaowanyonya.

Naandika kwa uchungu, watu wanajituma sana, wakitaka kujikomboa kwa kuwa huru na kuweza kuandaa matamasha yao wenyewe wachawi hawataki, watahakikisha huyo mtu hafanikiwi.

Hiki ni kizazi gani kisichopenda chao. Hawa hawampendi Kiba na hawa hawamtaki Chibu. Tunatakiwa tuwe mashabiki tunao support maendeleo yao na siyo maadui wanaofurahia kuanguka kwao.

Ninawatakia kila la heri, Chibu, Kiba na wasanii wote na wanamichezo katika maendeleo yao binafsi.
 
Kimba bila bifu na domo asingekuwa pale. Kipindi kile mnachosema kimba alihit na cinderela, alipata tuzo gani. Alishawahi kuwa nominated category 7.. Never.
 
Back
Top Bottom