Mtazamo wangu binafsi baada ya fainali ya kwanza ya shirikisho

Librarian 105

JF-Expert Member
May 6, 2023
239
325
images(16).jpeg

USMA walijiandaa zaidi ndani na nje ya uwanja kuikabili YANGA SC, ila YANGA SC wao mbali na kujiandaa kumkabili mwarabu, pia waliweka jitihada zao za ziada kumkomoa SIMBA SC.
Kwa mantiki hii, utani wa jadi wa timu zetu hizi mbili nchini, mara nyingi ni wenye kuumiza upande mmoja au mwingine katika ngazi ya michuano ya kimataifa kutokana na kutambiana na kupigana vijembe zaidi badala ya kuangalia maslahi mapana ya kushinda michuano hii.
Uyanga na usimba, ni vyema ukaishia ndani ya mipaka ya nchi yetu. Huko kwingine bora ukimya ukatawala kuliko kupigana vijembe na nyodo zisizo na manufaa.
Mwisho, kuteleza sio kuanguka, dakika zingine tisini zinafuata ugenini.
Yanga sc wajitathmini kisha kwenda na game plan yenye mikakati bora kuliko mpinzani wake.
Nawasilisha jukwaani.
 
Yanga wafungwe tu. Jana tulikua pamoja kuwashangilia Toka walivopigwa Moja bila. Walipokuja kuchomoa Kuna shabiki wa yanga akasema Hilo goli mayele ni sawa kawafunga Simba😡
Na mungu sio mrisho wakagongwa mbili moja mji ukawa kimya
 
waseme tu kimoyoni moyoni, mdomo uliponza kichwa.
 
Back
Top Bottom