Mtazamo unaopendekezwa na China kwa Pembe ya Afrika unachochea matumaini ya utulivu, maendeleo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
fdsafsaf.jpg


Wakati kukiwa na msururu wa hatari za zamani na zinazoibuka za kiusalama, nchi katika eneo la Pembe ya Afrika kama vile Kenya, Ethiopia, Eritrea na Djibouti zinahitaji haraka kutafuta mbinu mpya za utatuzi wa migogoro ili kuhakikisha utulivu na maendeleo ya amani ya kijamii na kiuchumi. Mgogoro unaoendelea nchini Ethiopia katika eneo la Tigray unahitaji suluhu ya pamoja na juhudi za kikanda na kimataifa ili kukomesha mapigano na mauaji.

Utulivu ni kiungo muhimu cha maendeleo

Kuna mambo mawili ya kuzingatia katika pendekezo la China, anasema Wu Peng, mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

La kwanza ni kuheshimu na kuunga mkono nchi katika kwenye kanda hiyo kutekeleza kikamilifu mipango yao wenyewe, kuondoa kuingiliwa na mamlaka nje ya kanda, na kuruhusu nchi za pembe ya Afrika kutatua masuala ya sasa ya amani na usalama wao wenyewe.

La pili ni kwamba China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na nchi katika pembe wa Afrika ili kukuza maendeleo ya uchumi wa kikanda na kuweka msingi imara wa amani na utulivu.

Je mchango wa kimataifa ni upi?

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alipozuru Kenya mapema Januari 2022 alisema China iko tayari kupendekeza "Mtazamo wa Amani na Maendeleo katika Pembe ya Afrika" ili kuzisaidia nchi za kikanda kushughulikia changamoto za usalama, maendeleo na utawala. Pendekezo hilo lilitolewa baada ya Bw. Wang kuzuru Ethiopia mapema Desemba mwaka jana na Eritrea mapema Januari, kabla ya safari yake nchini Kenya. Nchi zote tatu ziko kwenye pembe ya Afrika.

Mtazamo unaopendekezwa China

China imekuwa sehemu ya juhudi za kusaidia nchi za pembe ya Afrika kushughulikia changamoto za usalama, maendeleo na utawala bora.

Waziri Wang Yi anasema China inapendekeza mtazamo wa kusaidia kanda hiyo kufikia utulivu wa muda mrefu, amani na ustawi, na kuziunga mkono nchi za eneo hilo kujiepusha na ushindani wowote wa kijiografia kati yao na nchi kubwa.

Afisa huyo mkuu wa China alitaja vipaumbele vitatu vikuu, akibainisha kuwa Pembe ya Afrika inapaswa kuimarisha mazungumzo ya kikanda ili kuondokana na changamoto za usalama; inapaswa kuongeza kasi ya ufufuaji wa kikanda ili kuondokana na changamoto za maendeleo; na inapaswa kutafuta njia bora za kushinda changamoto za utawala.

Mchambuzi wa uhusiano wa kimataifa na kisiasa Eyob Belachew, anasema mpango wa China unaweza kuwa na nafasi kubwa kwenye mchakato wa ujenzi wa amani na maendeleo eneo la Pembe ya Afrika kwa kutoa jukwaa na pia uzoefu kwani China yenyewe ilitumia mpango kama huo kuinuka kiuchumi.

Tayari China imemteua afisa kutoka wizara ya mambo ya kigeni kuwa mjumbe wake maalum kwenye pembe ya Afrika, hatua inayoonekana na wataalam wa Afrika kama hatua muhimu ya kusaidia kufikia maendeleo ya amani katika eneo hilo.

"Sera ya nje ya China isiyohusisha mapigano inapaswa kutumika kama sauti ya kusaka amani na usalama endelevu katika kanda hiyo," anasema Cavince Adhere, msomi wa maswala ya kimataifa kutoka Kenya.

Wajibu wa China kwenye uendelezaji wa miradi ya maendeleo

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Taasisi ya Sera ya Afrika, tangu Mpango wa Ukanda mmoja na Njia moja (BRI) ulipopendekezwa mwaka 2013, China imesaidia miradi ya kisasa ya miundombinu kama vile reli, barabara, bandari, mabwawa, viwanda na uunganishaji wa kidijitali, vinavyochangia ukuaji barani Afrika.

Ripoti moja ya mwaka 2021 kwa jina Shared Prosperity: Tracking the Belt and Road Initiative Katika kipindi cha chini ya muongo mmoja, inaonyesha kuwa Kenya ina reli ya kisasa ya kilomita 670 (SGR) inayounganisha bandari ya Mombasa na bandari kavu ya Naivasha.

Na Reli ya kisasa ya Ethiopia-Djibouti iliyojengwa na China yenye urefu wa kilomita 752.7, inayounganisha Ethiopia isiyo na bandari na bandari ya Djibouti, ilirekodi mapato ya dola za kimarekani milioni 86.13 mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 37.5 ikilinganishwa na 2020.

Miradi kama hiyo na mingine mingi inaleta ukuaji wa kiuchumi, nafasi za ajira na hatimaye kupata utulivu wa kijamii kwa njia endelevu.
 
Back
Top Bottom