SoC01 Mtazamo hasi juu ya kukidhi kwa Walimu wa Sanaa(arts) na ongezeko la Wanafunzi

Stories of Change - 2021 Competition

Mirr

Member
Jul 14, 2021
16
30
Nawasalimu wana jukwaa,amani iwe nanyi!

Kwanza kabisa naomba nimshukuru Mungu kwa kunijaalia uzima hadi ninapoandika andiko hili sina budi kusema Alhamndulilah!

Bado kuna upungufu wa walimu wa masomo ya sanaa kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi hasa shule za mijini japo mahitaji ya serikali ni walimu wa sayansi.

Naomba niwe muwazi kabisa kuhusiana na tatizo la ongezeko la wanafunzi kwenye shule za mijini za kata kutokana na elimu bure.

Shule za sekondari hasa za mijini bado zinahitaji walimu wa masomo yote yani sanaa na sayansi. Kwa utafiti wangu wa moja kwa moja mfano shule za sekondari Ngarenaro, na Sombetini mkoani Arusha na zingine nyingi siwezi kuzitaja zote, zipo kwenye changamoto ya upungufu wa walimu masomo yote japo wa sayansi wanahitajika zaidi. Hii nikutokana na ongezeko la wanafunzi wengi ambapo inasababisha kuwa na mikondo mingi yenye wanafunzi wengi wakati huo mwalimu mmoja au wawili wa masomo husika. Hii ina mulazimu mwalimu aingie mikondo yote kwa siku moja kama ni mikondo 10 ni lazima aaingie sasa hii inapelekea mwalimu kuchoka kwasababu ni binadamu pia kuna wakati hatafundisha kwa mood hiyohiyo kuna haja serikali kutazama suala hili kwamba sio tu kuna upungufu wa walimu vijijini lakini pia hata mijini kuna upungufu kwasababu wanafunzi wameongezeka kwa mwamvuli wa elimu bure.

Ufaulu wa masomo ya sanaa unaendelea kushuka kutokana na dhana potofu kwamba walimu ni wengi hivyo hakuna haja ya kuajiri walimu wa sanaa. Kuna shule mwanafunzi akifika kidato cha tatu au cha nne anatakiwa achague masomo yake kama ni arts au science. Tatizo linakuja kwenye ufaulu kwamba wanafunzi wengi wanaosoma masomo ya arts au waliotengwa kwa masomo ya arta bado ufaulu wao ni hafifu sababu kubwa hapa ni idadi yao kubwa na mwalimu kuchelewa kumaliza mada kwa wakati ili kuwapa muda wa kutosha wanafunzi kufanya marudio na maswali mengi zaidi. Hivyo rai yangu nikwamba walimu wa arts pia waongezwe kuongeza au kuweza kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wenye uwezo wa masomo ya sanaa kama vile GEOGRAPHY, KISWAHILI, ENGLISH, CIVICS, na HISTORY.

Kutokana na mtazamo hasi juu ya walimu wa sanaa, wanafunzi wengi wanakata tamaa kwenye masomo yao baada ya kuona hawana uwezo kwenye masomo ya sayansi hivyo ukataji wa tamaa pia unaenda sambamba na kuona kaka, Dada ama ndugu zao waliosoma arts bado hawana ajira hivyo wanaona shule haina faida. Ombi langu nikwamba serikali isichoke kuajiri walimu wa sanaa ili wasaidie kuwa andaa na kuwapa moyo wanafunzi kulingana na uwezo wao ili baadaye wakawe viongozi wenye wasio kata tamaa na wenye mategemeo makubwa ya baadaye.

Mwisho kabisa, ningeomba wakaguzi na wanaosimamia ubora wa elimu katika idara zote wasichoke kutembelea mashuleni hasa shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi ili wawatie moyo walimu pamoja na wanafunzi na ikiwezekana wachukue maoni yao wayafanyie kazi. Kwenye hili suala kuna walimu wenye wito ambao wameamua kujitolea kuwasaidia wanafunzi bila kuangalia malipo hivyo itakuwa njema zaidi wawe wanatiwa moyo waendelee kuwasaidia wanafunzi na kuwapa mbinu mbali mbali za kufaulu mitihani yao, watakuwa wamesaidia sana kwenye kuinua ufaulu kulingana na ukata wa ajira.

Asanteni sana na kila atakayesoma andiko hili akabarikiwe kwa kukosoa, kupongeza ama kuongezea ushauri chanya ili tuweze kujenga jamii iliyostaarabika.
 
Back
Top Bottom