Mtawa Mkatoliki apigwa Zanzibar

Mtawa Mkatoliki apigwa Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Upendo ndio huo wa kuuza koti na kununua upanga?Na ndio huo upendo wanaomalizana kwa kuchinjana wa protestant na wakatoliki,Ireland ya kaskazini? Au kina Askof Joseph Kibwetere,kuwachoma maelfu ya watu kanisani,au upendo wa Kina John Garang,wakuuwa watu na kuwaacha maelfu vilema.Kweloi mna upendo.


Mkristo anatakiwa kuwa na upendo,lakini kwakuwa dhambi iliingia duniani,sio kila anayejiita mkristu ana UPENDO.
 
AUG202013


[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]
zenji.jpg


Kanisa la Minara Miwili, Unguja ambako Sista huyo na wenzake wanafanyia kazi.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Watawa wa kike wa Shirika la Moyo Safi wa Maria, Mgolole, Morogoro, wanaofanya kazi katika Parokia ya Minara Miwili, Unguja, wameiomba Serikali kuongeza ulinzi kwenye maeneo ya kiimani.



Wametoa mwito huo, baada ya jana kuvamiwa na kundi la watu kwenye makazi yao na kumpiga mmoja, Irene Mwenda na kumvua shela kichwani.



Tukio hilo japo lilihusisha majirani; nyumba ya watawa ya Bububu na majirani wa karibu na nyumba hiyo, waliodai kuku wao aling'atwa na mbwa wa watawa hao, watu wengine waliingilia ugomvi huo wakiwa na wenye kuku na kubishana na watawa hao, jambo lililosababisha ugomvi na hata baadhi yao kumpiga mtawa huyo na kumvua shela.


Mtawa Mkubwa wa Nyumba ya watawa hao visiwani, Sista Gaspara, alimwambia mwandishi jana kuwa tukio hilo halikuwa kubwa kiasi cha Polisi kuingilia kati.




Lakini, alisema ilibidi wapige simu Polisi baada ya kuona kundi la watu, wengi wakiwa vijana na silaha za jadi yakiwamo mawe, wakizungumza kwa jazba na matusi, wakidai kuku wao aling'atwa na mbwa wa watawa na bila kusubiri mazungumzo na namna ya kulipwa, walianza kumpiga mtawa mmoja.




"Ilikuwa saa 11 jioni jana (juzi), tulikuwa tumerudi kutoka shughuli za ibada nje ya hapa nyumbani, tulipofika likaja kundi la vijana na watoto wakidai mbwa wetu amemng'ata kuku wao, wakati Sista Mwenda akiuliza imekuwaje mbwa ang'ate kuku kwa kuwa huwa tunawafungia ndani, mmoja alimpiga sista ngumi chini ya jicho na sehemu zingine za mwili," alidai Sista Gaspara.




Alidai Sista Mwenda alitaka vijana wale wasiohusika na kuku waondoke, ili wasijae sana pale na abaki mmiliki wa kuku ili wazungumzie tukio hilo na namna ya kumfidia, maana nyumba ya watawa ina uzio na kuku huyo alirukia ndani kwa kuwa milango ilikuwa imefungwa.


Sista Gaspara alidai kuwa kinachosikitisha si kipigo dhidi ya mtawa, kwa kuwa hakuna damu iliyomwagika ila maumivu ya kawaida aliyopata na kutibiwa katika hospitali ya Jeshi ya Kibweni, lakini kibaya ni namna walivyopandisha jazba kuhusu tukio hilo na kitendo cha kumvua mtawa shela na kuitupa.


Katika utaratibu wa Kanisa Katoliki, shela anayovaa mtawa inabeba maana halisi ya kiimani ya utawa wake, hivyo kitendo cha kuvuliwa kitambaa ni sawa na kuvuliwa utawa. Hata hivyo, waliiomba Serikali kuongeza elimu ya maadili shuleni, wazazi kufunza nidhamu watoto wao na jamii nzima kuheshimu maadili na kuishi kwa amani na utulivu.


Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Zanzibar, Yusuf Ilembo, alithibitisha kutokea tukio hilo lakini akasema ulikuwa ni ugomvi wa kawaida wa majirani kwa majirani, hivyo pamoja na kwamba Polisi ilishirikishwa, lakini uliisha kiujirani.


"Ni kweli suala limetokea, lakini ni ugomvi mdogo wa jirani na jirani, kuku aliingia nyumbani kwa watawa, pale wanafuga mbwa, akang'atwa, wenye kuku walikwenda kudai, ndipo ugomvi ukatokea mmoja akampiga mtawa ila hakuna damu iliyomwagika," alisema Ilembo.



 
Siyo jambo kubwa kuvuliwa UTAWA!!! "ugomvi wa majirani kwa majirani". Hawa ndio walinzi wa amani. Upande ulioumizwa hauna jazba kama ule upande wa HIJAB ya muislam Feki Igunga ulioamsha hasira za jamii yote ya kiislamu. Tuendelee tu kuendekeza huu upuzi ambao unaleteleza kunguru mkubwa anayeitwa CCM kufaidi mizoga na ushindi poleni sana!!!
 

Yeah, Zanzibar inatka UHURU wake kamimi lakini sio kuchoma moto Madaraja yote yatakayoiwezesha ielee DUNIANI kimaendeleo.

Sasa kama Mataifa ya nje yatagoma kuipa MSAADA Zanzibar huru nchi si itakuwa kama Afghanistan ilipoachwa na Warusi?

Na nina Imani kuwa hilo kanisa lilikuwepo ENZI za UKOLONI halikuwa tatizo kwanini Sasa?

Mategemeo ya kupata Misaada nchi za KIISLAMU na KIARABU ili Zanzibar iendelee pia inatokana na AMANI; Sidhani kuwa OMAN itaweza kutoa Misaada kwa Zanzibar ya namna hii; Sababu OMAN ni rafiki Mkubwa sana wa Marekani
 
Ugomvi wa kiujirani tu maana yeke nini? Ukipigwa huumii? Ukikatwa na kitu cha nja kali hufi??
Waongeze elimu tu
 
Ni watu wapuuzi na wakupuuzwa... Mungu amewajalia roho ya upendo na uvumilivu wakristo.. Hata hawana haja na mambo ya kipuuzi... Adui wa mwislam ni mkristo Aduni wa mkristo ni shetani...mpende adui yako kama unavyojipenda mwenyewe.. Hayo ni maagizo kwa wakristo wote.. Msilipize kisasi maana kisasi ni kazi ya shetani..
 
Kama ni kweli hilo ni suala la aibu sana kwetu Watanzania na imani husika. Hili halina tofauti na lile tukio la Mbagala ambapo Makanisa yalivamiwa ati kwa kuwa mtoto alikojolea Quran.

Yaani imefikia wakati watu wanakutegea ufanye kosa dogo ili wapate uhalali wa kutekeleza mafundisho potofu ya kidini.

Serikali imelea sana upuuzi wa aina hii kwa muda mrefu sasa inakuwa vigumu kuung'oa.

hvi hyo tuiwekeje? hvi ni kuku wa kawaida au ni kuku wa aina gani hyo? au ndo tuseme ndugu wamegeuka watetezi wa haki za wanyama? hvi angejiruhiwa kuku wa mkristu hapo mtaani hao jamaa wangepatwa jazba namna hyo?....anyway msinielewe vbaya cjaimanisha kuwa kuku hyo alikuwa "WA KIISLAM" hapana ckuimanisha hvyo.
 
Udhalimu una mwisho wake. hawa watu wana choko choko sana. ngoja muungano ufikie mwisho tuone hawa wapemba waliojazana dsm na kote nchini wataenda wapi. wazanzibar ni wabaguzi sana mi hata huwa siwaelewi hata kidogo
 
Ingawa kamanda wa Polisi anataka tuamini kuwa ni ugonvi wa majirani lakini sijui analinda sheria ipi. Kupigana peke yaka ni kosa la jina, hata kama wamepigana ndugu, majirani n.k. Kama hao ni majirani walitakiwa kuheshimiana sana. Kitendo cha mmoja wao kuamua kumpiga mtawa aliyevaa kilemba sio kitendeo kidogo. Lazima kuwe na sababu zaidi ya kuku kuumwa na mbwa. Na kumbe kuku ndie aliyerukia uani kwa watawa. Kuna sababi kama ya kisasi hivi iliyofanya mtawa huyo akapigwa. kamanda wa polisi anatakiwa alichunguze na ajiridhishe kama hakukuwa na sababu zaidi ya hizo. kitu kingine kwa nini jirani huyo asanye wenzake nio waende kuwafanyia fujo watawa. Kamanda asichukulie vitu juu tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom