Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

Mtatiro, una moyo mzuri sana usio na hiyana. Mwenyezi Mungu akufanikishe kivingine.
 
Chadema tumekua mafala wa mwisho jimmbo la segerea mamate sana yaani kata zote ukawa afu ubunge kwa hawa wasengerema mamaye dah chadema mmeniudhi yaani kutompeleka mtatiro mjengon
 
Hongera sana kaka Julius Mtatiro, umeongea pointi za maana sana! Kikubwa kama ulivyosema ni USHIRIKIANO, yaani Umoja ni Nguvu!
 
Pole sana jembe julius wewe ni mwanafilosofia wa ajabu, umeongea maneno ya kimapinduzi ambayo uwa yanaongelewa na wanamapinduzi waliobobea, pia hilo la kushughulikia changamoto zilizotokea wakati wa kupitisha wagombea kupitia ukawa ili uko mbele kusitokee mikanganyiko.
Mie naamini tumepoteza mchezo, hatujapoteza mashindano wewe ni jembe ningependa nikuone huku wewe kule lissu pale kubenea hapa mdee wangetukoma mafisiemu, baki front line kamanda bado tunakuhitaji sana mjengoni.
Salute.
 
Big up, kwa tunakujua toka ukiwa UD! tunajua weledi wako na tunasikitika taifa kukukosa bungeni! Kwa wanaukawa tuchukulie hili kama fundisho kwetu, na mapambano yakweli kung'oa mizizi iliyobakia ya CCM ianze sasa!

Big up kwa demekrasia chanya kama za mtatiro
 
Huyu Dada wa CDM aliyemnyima Mtatiro nafasi ya kuingia bungeni hana akili kabisa
 
Siku zote nitakuheshimu Mtatiro. You are truly leader. Uchaguzi si kipimo halisi cha uongozi...kiongozi si lazima awe na wadhifa...Mungu akubariki
 
mbona umeruka 2010?
Hata hiyo 2005 aliyosema ni sawa tu inaonyesha hasivyotaka kuuona ukweli. Maandiko ya Mtatiro yalisema kuwa baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi hakujatokea CUF wakapata wabunge zaidi ya wawili huku bara na pia hawajawahi kuongoza halmashauri!
"Tokea chama chetu kilianzishwa hakikuwahi kupata zaidi ya wabunge wawili Tanzani Bara na hakikuwahi kuwa na halmashauri hata moja."
 
Well stated kamanda Mtatiro; hukwenda bungeni lakini baadhi yetu tunatambua na kuyaheshimu maono yako kuhusu mustakabali wa nchi hii; Do not give up the fight Julius; keep the fire within you burning for the good of this country; may God bless you.
 
I salute Mtatiro, usijali bado ni kijana mwaka 2020 jimbo utalipata kirahisi sana, ni matumaini Chadema itakuomba radhi na kumchukulia hatua yule dada aliyekuhujumu na kusababisha UKAWA tupoteze jimbo na mbunge makini.
 
UKAWA ni lulu na itaendelea kua lulu kwa wale wote wanaotaka mabadiliko hapa Tanzania mpaka pale CCM itakapong'olewa rasmi madarakani.

UKAWA imewezesha kufuta doa la udini na ukabila lililopandikizwa na CCM dhidi ya wapinzani ili kuwagawa na kuwadhoofisha katika juhudi zao za kuleta demokrasia ya kweli hapa Tanzania.

UKAWA imewezesha ufanisi katika zoezi zima la kuzisimamia kura na kuzilinda wakati wa uchaguzi huu kwani kila chama kilichounda UKAWA kilikuwa na Wakala wake ndani ya chumba cha kupigia kura na hivyo kufanya zoezi la kupenyeza kura feki au kuhonga mawakala wa upinzani kuwa gumu.

UKAWA imewapa matumaini Wazanzibari ya kupata uhuru kamili wa taifa lao na hivyo kuwaunganisha bila kujali vyama vyao ndani ya nchi yao na kukipigia kura CUF kwa wingi na kuzilinda kura zao kiasi cha CCM kushindwa kabisa kuchakachua kura za Wazanzibari.

Ushindi wa CUF Zanzibar ambao unasubiriwa kutangazwa tu kwa sasa utaongeza nguvu sana UKAWA kwenye mapambano dhidi ya kudai katiba mpya kwani CUF watakuwa wakifanya hivyo wakiwa wameshika hatamu Zanzibar na hivyo kuongeza nguvu ya wapinzani Tanganyika kwa ujumla wao katika mapambano ya kudai katiba mpya na demokrasia ya kweli ndani ya Tanzania.

UKAWA imewawezesha viongozi mahiri wanaotengwa na CCM kupata platform ya kuendeleza harakati zao za kisiasa nje ya CCM na hivyo kuongeza demokrasia na ushindani ndani ya Tanzania.

Ni kwa sababu ya UKAWA tunashuhudia mwaka huu wabunge wengi wa upinzania kutoka pembe zote za Tanzania wakiingia bungeni na hivyo kuwawezesha wapinzani kuwa na nguvu kubwa bungeni katika bunge lijalo.

UKAWA imeiwezesha CHADEMA kwenda Ikulu mwaka huu kama zoezi la CCM la kuchakachua kura likidhibitiwa na kuiwezesha CHADEMA kupata wabunge sehemu ambazo ingekuwa shida kwa wao kuzipata bila support ya muungano wa UKAWA. Nakumbuka kabla ya UKAWA Watanzania waligawanyika mno kwenye mtazamo wa kidini na kikabila uliorutubishwa na mikakati ya CCM ambao ulikuwa wazi ukiangalia uchangiaji wa hoja za kisiasa kwenye mitandao ya kijamii kama hapa JF, Facebook, n.k. Lakini UKAWA iliposimamisha wagombea wa coalition hali hii ilipotea kabisa kwenye mitandao ya kijamii na Watanzania wakaungana katika harakati ya kudai mabadiliko chini ya mwamvuli wa UKAWA.



Sababu za umuhimu wa UKAWA kwa mustakabali wa nchi yetu ni nyingi. Hizi ni chache tu.

Hivyo ni maadui wa demokraia ya kweli na maendeleo ya Tanzania tu ndio ambao watajenga mtazamo hasi kuhusu UKAWA kwa kutumia matokeo yanayojiri kwa sasa kwa kudai UKAWA imekibeba chama fulani badala ya kuona umuhimu wa UKAWA kwa ujumla wake katika uchaguzi huu.
 
Pamoja mkuu cha msingi baada ya uchaguzi huu mkae chini mfanye analysis ya changamoto za umoja wenu ili kuufanya uwe imara zaidi kwa manufaa mapana ya Tanzania na vyama vyenu pia.
 
Mtatiro kwa kweli wewe una Busara sana. Uwe chachu ya kudumisha umoja wa ukweli kwa UKAWA.
Tukianza kujipanga kuanzia sasa uchaguzi mwingine tutafanikiwa zaidi.

Hongera CUF Hongera UKAWA
 
Back
Top Bottom