Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

Mpaka muda huu CUF wamelamba viti 20 hapa bado vile pending vya Temeke na Kinondoni...masikini Lipumba sijui anajisikiaje sasa hivi huko alipo...ila inaniuma Mtatiro kufanyiwa fitna na yule dada wa CHADEMA...
Mkuu hivi mpaka mda huu Ukawa jumla wana viti vingapi?
 
Hili jamaa kwa kulialia na kujipendekeza halijambo aisee!
 
Huwa namfurahia sana Mtatiro, ni mwana-Siasa wa ukweli sana.

Hongera sana Mtatiro. Na hii ndiyo faida ya kukaa karibu na PROFESA. ume-grab fikra za Kizalendo. I can see another professor-not yet verified through CUF. Also be close to Hon. ZZK for betterment of your future as a visionary leader!
 
kuna watu bila aibu walikua wanasema ACT Wazalendo watafanya vizuri zaidi ya CUF....narudia tena CUF inazaliwa upya mpaka sasa wabunge 20 hapa bado pale Temeke na kinondoni...madiwani kwa DAR chama cha CUF kimefanua vizuri sana...heshima kwa Maalim Seif Sheriff Hamada, Mama Sakaya na Mtatiro...
pia mkoa wa Lindi CUF wanapata majimbo 4 katika majimbo 8 katika mkoa huo
 
kuna watu bila aibu walikua wanasema ACT Wazalendo watafanya vizuri zaidi ya CUF....narudia tena CUF inazaliwa upya mpaka sasa wabunge 20 hapa bado pale Temeke na kinondoni...madiwani kwa DAR chama cha CUF kimefanua vizuri sana...heshima kwa Maalim Seif Sheriff Hamada, Mama Sakaya na Mtatiro...

Kwa kweli cuf wamejitaidi sana wameirudisha Cuf huku bara imepata uhai nadhani waanze kujipanga vizuri watafika mbali. Le profeseri hakua na nia ya dhati zaidi ya kuchaganya wananchi
 
Huyu dada anatropia katusaliti sana wana Segerea...Ngoja uchaguzi upite
 
Last edited by a moderator:
Huyu dada anatropia katusaliti sana wana Segerea...Ngoja uchaguzi upite
Ahame tu Segerea ndio ataishi kwa amani, wananchi wana hasira naye kuliko maelezo, nipo Kinyerezi muda huu vijana ukiwasikiliza maongezi naogopa hata kusema. kama kuna jimbo ccm haitakiwi basi ni jimbo la Segerea maana washkaji zetu wengi wamegombea udiwani kupitia ccm lakini tuliwaeleza waziwazi hatunachuki na nao wao ila sisi hatuitaki ccm baasi, kama mnagombea kupitia chama hicho mnapoteza pesa zenu bure hatutowapigia kura licha kwamba tunakunywa bia wote kwenye bar moja kila siku, na ndicho tulichokifanya. Tumeipiga ccm 13 kwa 0.
 
looh kweli comrade mtatiro uko vizuri dogo! tangu mchakato wa kukupata kama mgombea, huyu dada kuvuruga bado upo imara? Mungu atakulipa tu
 
Tuko pamoja kaka Mtatiro usiwaze kuishia kutoa tuu ushauri mi naamini ukawa itashinda urais na Mtatiro utapewa ukuu wa mkoa.
 
CCM itatia fitina mpaka Chadema na CUF wafarakane....nyie subirini tu
 
looh kweli comrade mtatiro uko vizuri dogo! tangu mchakato wa kukupata kama mgombea, huyu dada kuvuruga bado upo imara? Mungu atakulipa tu
 

  1. Arumeru Mashariki – Joshua Nassari CHADEMA
  2. Babati Mjini – Pauline Gekul CHADEMA
  3. Bukoba Mjini – Lwakatare Wilfred Mugyanyizi CHADEMA
  4. Bunda Mjini- Esther Bulaya – CHADEMA
  5. Buyungu – Bilago Samson CHADEMA
  6. Hai -Freeman Mbowe CHADEMA
  7. Iringa Mjini – Peter Msigwa CHADEMA
  8. Kaliua – Magdalena Sakaya CUF
  9. Kibamba – John Mnyika CHADEMA
  10. Kigoma Mjini – Zitto Kabwe ACT
  11. Mbeya Mjini- Joseph Mbilinyi CHADEMA
  12. Mchinga- Hashim Hassan Bobali CUF
  13. Momba – David Ernest Silinde CHADEMA
  14. Monduli – Julius Kalanga CHADEMA
  15. Moshi Vijijini – Anthony Calist Komu CHADEMA
  16. Moshi Mjini- Jaffary Michael –CHADEMA
  17. Mtwara Mjini - Maftah Abdallah Nachuma CUF
  18. Ndanda- Cecil Mwambe CHADEMA
  19. Rombo- Joseph Selasini CHADEMA
  20. Same Magharibi- Livinston N Kaboyoka CHADEMA
  21. Serengeti - Chacha Marwa Ryoba – CHADEMA
  22. Siha - Dr. Godwin Mollel CHADEMA
  23. Singida Mashariki – Tundu Lissu CHADEMA
  24. Tandahimba- Ahmed Katani CUF
  25. Tanga Mjini – Musa Bakari Mbarouk CUF
  26. Tarime Mjini - Esther Matiko CHADEMA
  27. Tarime Vijijini – Heche john CHADEMA
  28. Temeke - Abdallah Ally Mtolea CUF
  29. Tunduma – Mwakajoka Frank CHADEMA
  30. Ubungo- Said Kubenea CHADEMA
  31. Vunjo – James Mbatia NCCR-MAGEUZI
 
MTATIRO u aa my modal.same ukawa imeondoa dhana ys udini kwenye vyama.nafas kubwa zinakusubiri CUF.labda wasijua value yako.
 
UKAWA IMELETA MAPINDUZI MAKUBWA SANA YA SIASA HAPA TANZANIA.

Hongereni sana Ubungo. Mimi sitakwenda Bungeni lakini mtu kama Kubenea anakwenda. Ni jambo kuu sana kwangu.

Kule Kinondoni CUF tuna kijana wetu mzuri anaitwa Mtulia Maulid, nikitoka ngome nakwenda kumuunga mkono kwenye majumuisho. CUF inaleta kijana machachari sana kutoka hapa Kinondoni.

Pale Temeke yupo Mtolea wa CUF huyu naye hadi sasa anaongoza. Kule Mbagala yupo Kondo Bungo wa CUF naye anaongoza. Ni faraja kubwa sana kwangu, vijana hawa wote wakawashe moto bungeni. Sisi tutawasaidia sana tukiwa nje ya bunge na huwenda ufanisi wao bungeni ukatokana na ushauri wetu huku nje.

CUF pia imetuletea SAKAYA, huyu ni samaki na huwezi kumfundisha kuogelea, kule kusini tayari tuna Kuchauka wa Newala, tuna Katani wa Tandahimba, tuna Bobali wa Mchinga, tuna ----- Bungala wa Kilwa kusini, tuna Musa wa Tanga Mjini n.k.

Bado vijana kadhaa wa CUF pia wanaelekea kushinda kwenye majimbo mengine.

Siyo hivyo tu, CUF pia imepata na itaongoza halmashauri kadhaa ikiwemo Tanga Mjini, Newala, Tandahimba, Kilwa n.k. Haya ni maeneo ambayo tumepata madiwani wengi.

HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA SANA KWA CUF..

Tokea chama chetu kilianzishwa hakikuwahi kupata zaidi ya wabunge wawili Tanzani Bara na hakikuwahi kuwa na halmashauri hata moja.

Ndiyo maana mimi ni mtu nayeamini sana katika ushirikiano. Leo CUF inapata wabunge wengi bara, inaelekea kuongoza halmashauri kadhaa...Hii ndiyo faida ya kujitosa kwenye ushirikiano.

Tulipokuwa tunaanzisha UKAWA kuna watu walisema CUF itamezwa. Mimi nimeendelea kushikilia msimamo kuwa CUF haiwezi kumezwa kwani hivi sasa ina wabunge wengi zaidi kuliko ilivyowahi kutokea. Chama chochote kinakuwa VIBRANT na kukua kinapopata wawakilishi wengi zaidi. Huu ni mwanzo mzuri sana kwa CUF na UKAWA yenyewe.

UKAWA inapaswa kushughulikia changamoto zake zilizosababisha kukosa baadhi ya majimbo muhimu na kujiwekea utaratibu bora kwa uchaguzi ujao.

Mtatiro J,
Segerea.

Umoja Ni Nguvu Kaka
 
mambo yangekuwa vizuri zaidi kama kusingekuwa na mkanganyiko kwa jimbo la Mtama na Segerea.
 
Habari hii imfikie yule Prof. Lipumba..vu aliyetoroka nchi ili kuisaliti na kuua UKAWA.
 
Back
Top Bottom