Tunahitaji bunge lenye mawazo kinzani kwa ajili ya maendeleo ya nchi

Twayemba

Member
Jan 29, 2024
12
14
Nikikumbuka bunge la Spika Sitta, hoja nzito za akina Lissu, Mbowe, Lema, Kabwe na wengine wengi waliokuwepo bungeni kipindi kile, unaona tofauti kubwa iliyopo kati ya bunge la wakati ule na hili la sasa.

Wabunge wa upinzani walikuwa wanajenga hoja mbadala nzuri na za kusisimua sana. Ni lazima tukubali huo ukweli kwamba bunge la chama kimoja kwa miaka hii ya leo, limepitwa na wakati na kimsingi halitakiwi.

Mheshimiwa Mbowe,aliongea pale Monduli msibani kwa Lowassa,kuwa tunapompata kiongozi mwenye vipaji bora vya uongozi,tumtumie "to the maximum" kwa ajili ya nchi, na kwamba Lowassa pamoja na kujaliwa vipaji hivyo, hakutumiwa Ipasavyo.

Nikifikiria hoja hiyo,nawakumbuka wabunge kadhaa ambao kama leo wangekuwepo bungeni, bunge hakika lingekuwa bora zaidi kuliko ilivyo leo.

Watu kama Mbowe, Lissu, Mdee, Kabwe, Mnyika, Lema, Msigwa, Heche, Matiko na wenzao wengine, walipaswa kuwepo bungeni ili bunge letu liwe bora zaidi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Wakulaumiswa ni dikiteeta mwendazake tulikuwa relini ghafla akaingiza treni korongoni
 
Back
Top Bottom