Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

UKAWA IMELETA MAPINDUZI MAKUBWA SANA YA SIASA HAPA TANZANIA.

Hongereni sana Ubungo. Mimi sitakwenda Bungeni lakini mtu kama Kubenea anakwenda. Ni jambo kuu sana kwangu.

Kule Kinondoni CUF tuna kijana wetu mzuri anaitwa Mtulia Maulid, nikitoka ngome nakwenda kumuunga mkono kwenye majumuisho. CUF inaleta kijana machachari sana kutoka hapa Kinondoni.

Pale Temeke yupo Mtolea wa CUF huyu naye hadi sasa anaongoza. Kule Mbagala yupo Kondo Bungo wa CUF naye anaongoza. Ni faraja kubwa sana kwangu, vijana hawa wote wakawashe moto bungeni. Sisi tutawasaidia sana tukiwa nje ya bunge na huwenda ufanisi wao bungeni ukatokana na ushauri wetu huku nje.

CUF pia imetuletea SAKAYA, huyu ni samaki na huwezi kumfundisha kuogelea, kule kusini tayari tuna Kuchauka wa Newala, tuna Katani wa Tandahimba, tuna Bobali wa Mchinga, tuna ----- Bungala wa Kilwa kusini, tuna Musa wa Tanga Mjini n.k.

Bado vijana kadhaa wa CUF pia wanaelekea kushinda kwenye majimbo mengine.

Siyo hivyo tu, CUF pia imepata na itaongoza halmashauri kadhaa ikiwemo Tanga Mjini, Newala, Tandahimba, Kilwa n.k. Haya ni maeneo ambayo tumepata madiwani wengi.

HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA SANA KWA CUF..

Tokea chama chetu kilianzishwa hakikuwahi kupata zaidi ya wabunge wawili Tanzani Bara na hakikuwahi kuwa na halmashauri hata moja.

Ndiyo maana mimi ni mtu nayeamini sana katika ushirikiano. Leo CUF inapata wabunge wengi bara, inaelekea kuongoza halmashauri kadhaa...Hii ndiyo faida ya kujitosa kwenye ushirikiano.

Tulipokuwa tunaanzisha UKAWA kuna watu walisema CUF itamezwa. Mimi nimeendelea kushikilia msimamo kuwa CUF haiwezi kumezwa kwani hivi sasa ina wabunge wengi zaidi kuliko ilivyowahi kutokea. Chama chochote kinakuwa VIBRANT na kukua kinapopata wawakilishi wengi zaidi. Huu ni mwanzo mzuri sana kwa CUF na UKAWA yenyewe.

UKAWA inapaswa kushughulikia changamoto zake zilizosababisha kukosa baadhi ya majimbo muhimu na kujiwekea utaratibu bora kwa uchaguzi ujao.

Mtatiro J,
Segerea.

Mkuu Mtatiro! Usijali sana. Mungu ana mipango yake tulia tu. Anapanga atakavyo! Kikubwa kumuabudu tu.
 
Ahame tu Segerea ndio ataishi kwa amani, wananchi wana hasira naye kuliko maelezo, nipo Kinyerezi muda huu vijana ukiwasikiliza maongezi naogopa hata kusema. kama kuna jimbo ccm haitakiwi basi ni jimbo la Segerea maana washkaji zetu wengi wamegombea udiwani kupitia ccm lakini tuliwaeleza waziwazi hatunachuki na nao wao ila sisi hatuitaki ccm baasi, kama mnagombea kupitia chama hicho mnapoteza pesa zenu bure hatutowapigia kura licha kwamba tunakunywa bia wote kwenye bar moja kila siku, na ndicho tulichokifanya. Tumeipiga ccm 13 kwa 0.

Mkuu Matola nakumbuka ulitoa tahadhari mapema sana,na ukamtaja jamaa Mkurya anayemuhamasisha huyu dada asiachie Jimbo...kweli dada katuangusha sana,siku ya ufunguzi wa kampeni za UKAWA wanasema yeye alijitenga na kufungua kampeni za Madiwani wa Chadema the same day..halafu hakuonekana Jimboni kufanya kazi na mtatiro..akaenda mikoani mpaka mwisho
 
Last edited by a moderator:
katika wagombea wote wa nafasi ya ubunge, kwa hekima, ustahimilivu wa kisiasa ujengaji na uwasilishaji wa hoja Julias Mtatiro ameonyesha kiwango cha juu sana. Ningekuwa na mamlaka ningmpatia ubunge ili ajenge hoja na atetee maslah ya wananch.
 
Hongera sana Mtatiro. Na hii ndiyo faida ya kukaa karibu na PROFESA. ume-grab fikra za Kizalendo. I can see another professor-not yet verified through CUF. Also be close to Hon. ZZK for betterment of your future as a visionary leader!
well-said!
 
bila Chadema kumhujumu Mtatiro jimbo la Sengerea leo hii na yeye(mtatiro) angekuwa anaenda bungeni kiurahisi sana
 
Ulichoandika kinaendana na cv yako niliyosoma ktk gazeti la mwananchi...kweli wewe ni Msomi. Big up.
 
Back
Top Bottom