Mtanzania Bingwa wa Dunia

Mtanzania Bingwa wa Dunia

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,776

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre

[video=youtube_share;FdifkhentBw]http://youtu.be/FdifkhentBw[/video]
 
Hongera Bingwa Khamis. Ungezaa bidii na utafika mbali.
 
Hiyo sio hoja kwani amelelewa na Sister Jean Pruitt, na anafadhiliwa na Amy Canady mbona siwaoni akina .........kama kweli mnapenda maendeleo ya dogo

Mpe hongera basi.
 
Kwa hiyo nawe umeleta post kwa sababu ni anitwa Hamis? Mwezi wa toba

Of course siyo sababu hiyo lakini nilipoona watu wanaipita nyuzi na wanaona kama hastahiki inabidi niulize sababu.
 
Au kwa kuwa anaitwa Hamisi?
Hivi ndugu, unafahamu madhara ya hicho unachokifanya humu?

Yani unaanzisha timbwili la udini from nowhere yani?

Unaelewa kweli madhara ya migawanyiko ya kidini kwenye jamii?
 
Of course siyo sababu hiyo lakini nilipoona watu wanaipita nyuzi na wanaona kama hastahiki inabidi niulize sababu.

Hukuuliza sababu , umetoa umefikiria kwa niaba ya wachangiaji. Kijana huyu yupo zaidi ya wiki tangu amekuja na mambo yake yalionekana wazi kwenye Tv na bado hujasoma mitandao mingine kama fb kuona kama hawajamkubali. Binafsi nahisi labda watu hawapendi uzi zako hapa Jf wameona zina mapungufu
 
Hahahahah.......eti kisa ni Hamis. Anyway, hongera Sister kwa malezi bora kwa Hamis hadi ameleta medali. Hapo je?
 
Hukuuliza sababu , umetoa umefikiria kwa niaba ya wachangiaji. Kijana huyu yupo zaidi ya wiki tangu amekuja na mambo yake yalionekana wazi kwenye Tv na bado hujasoma mitandao mingine kama fb kuona kama hawajamkubali. Binafsi nahisi labda watu hawapendi uzi zako hapa Jf wameona zina mapungufu

Hapa ni fb? hivi unafikiri kila mtu anakwenda huko fb? umechelewa.

Hivi wewe kwa akili yako uko hapa ili upendwe? unanchekesha.
 
Back
Top Bottom