Mtanzania Anarudishwa Bongo Kutoka Marekani. Ana USD 10,000 (23M Tshs) Tu. Mnampa Ushauri Aitumieje?

Inategemea. Mimi binafsi USA ndio imenitoa. Ila mimi niko tofauti na waTz wengi. Nilikuja kutafta maisha. Naishi kwa kujinyima nk. Wabongo wengi wakija huku ni starehe tu na wanasahau nyumbani. Mwisho wa siku ndio inakuwa hivi. Ni kuwa na malengo. Kazi USA zipo nyingi. Ila Tz kazi za mshahara mzuri ni changamoto kwa wengi. Inategemea tu.
Na ndugu wengi huko State ila hAli Yao ngumu no investment at all, wanazidiwa na Hadi ma mangi wenye duka la kawaida
 
Ni kweli maisha ya diaspora hayana formula ila majority waishi Kwa shida heri tu kurudi nyumbani na huyu mleta mada alienda kwa shule lakini kufika kule akashindwa shule Sasa anaona arudi home wakati angekuwa bongoland angekuwa mbali sana, home is home tu mzee
IMG-20180302-WA0010.jpg

Hata kusafiri nasafiri vizuri tu. Jamaa yeye hajarudi tz tokea aondoke. Ukiwa hauna makaratasi hata kusafiri hauwezi.
 
Na ndugu wengi huko State ila hAli Yao ngumu no investment at all, wanazidiwa na Hadi ma mangi wenye duka la kawaida
USA hela ipo.. ila maisha waTz wanaishi kwa kushindana kwa hio wananunua mavitu ya gharama kwa kuonesheana. Mimi wala sina muda na wabongo wa huku. Nilishaona tunaleta ujinga wa tanzania tunakuja nao huku USA.
 
USA hela ipo.. ila maisha waTz wanaishi kwa kushindana kwa hio wananunua mavitu ya gharama kwa kuonesheana. Mimi wala sina muda na wabongo wa huku. Nilishaona tunaleta ujinga wa tanzania tunaluja nao huku USA.
Hatushindani na mtu watu huwekeza for future use
 
Sasa hapo atafanyaje ana majanga huyu
At least anajirudisha mwenyewe. Ukirudishwa kwa mamlaka hauondoki hata na wallet yako. Kwa hio kuna uzuri flani.. ila kweli atapata shida. Alikuwa mtu wa bata ila kabadilika sana. Naamini ataweza tu. Asanteni wote kwa ushauri mzuri 🙏🙏
 
Ww itakuwe umeishi nje ya Tz. Well said brother. Umechanganua vizuri sana. Need say no more.

Kweli brother.

Kuna watu wanaishi mbele,wanasema sina mpango na bongo ila ukiwaona unaona kabisa akili zao ziko bongo.

Kuna wale wamejiwekea akilini mwao kwamba udayasporani ni pakupita njia, naishi ila ipo siku nitajikuta nipo bongo.

Kuna wale wanaoishi kwa malengo sana baada ya muda fulani nitakuwa bongo, hawa wanasahau hata kuishi maisha ya kule ni wachumi sana.

Sasa hawa wakirudi nyumbani kwa namna yoyote hawewezi kuwa sawa hata saikolojia ya kiakili.
 
dah comment za watu zinafurahisha sana...

mkali asiogope mwambie adondoke tu bongoland ila aache unyamwezi huku kuna wenyewe wenye anga zao kama wako Denver au Miami vile.....

24mil asiingie kichwachwa kwenye risk business aanzie kwenye non risk anapiga mdogomdogo anakula anavaa na kusave kidogo huku akiisoma game....24mil kibongo bongo kama mpambanaji ndani mwaka inabadili ubao...

Mkuu naomba idea ya non risk business
 
Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.

Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.

Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.
Atataka kuishi sehem gani hapa Tanzania?

namshauri kwanza achukue milioni 5 tu aangalie upepo wa biashara.

asizamishe mtaji wote.

Akitaka employee wa kwanza kama operations manager, nipo hapa.

Itapendeza sana kama tutaanzisha biashara ya importation kama mifuko hii ya magufuli kutoka Kenya. Sisi tutauza kwa JUMLA.

milioni 5 ni nyingi sana.
 
ww mpenzi ulinisikitisha sana siku moja. Ila mie bado nakupenda. Nikupe info tu za ile biashara yangu ya tours kwa sasa nimepaki tu magari na lodges hazifanyi kazi sana. Nimerudi ughaibuni huku kuna fursa nzuri za pe$$a. Bongo bado assets zangu zipo, na nitazifanyia kazi ila biashara huko covid nk zilivuruga. Ila nilihuzunika ile post fulani ukasema maneno badala ya kuniuliza.
Haaaaa Haaaaa 😂 nisamehe mpenzi tafadhali, nikeikumbuka sana hiyo post.
Tuachane na ya nyuma tafadhali tugange yajayo
 
Msela mmoja alikutwa na picha za child porn, alifungwa jela miaka kadhaa. Alipotoka DBS imeoza na bila DBS hupati kazi zinazolipa vizuri.

Bahati nzuri alikua na Pagala Dar, alilijenga enzi Mkapa ndiye Rais. Amerudi bongo na milioni 25. Amemaliza vyumba viwili kwenye Pagala lake anapika biriani jioni.

Hahahahahahaaa!!! Namjua
 
Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.

Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.

Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.
Mrejesho???
 
Back
Top Bottom