Mtanzania Anarudishwa Bongo Kutoka Marekani. Ana USD 10,000 (23M Tshs) Tu. Mnampa Ushauri Aitumieje?

Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.

Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.

Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.
usd 10,000 nyingi sana Le mutuz alirudi na usd 1000.
 
Kutokujua cha kufanya anaporudi nyumbani ndio changamoto kubwa ya wanadiaspora wote wanaoamua kurudi Tz. Wapo ambao hurudi na elimu na utaalam ambao huwasaidia vyema kuanzisha biashara ama kuekeza fedha zao kwa utaratibu mzuri.

Kwake ndugu yetu inakuwa ngumu kumshauri anze vipi kwasababu hatumjui utaalam na uzoefu alionao. Sio vyema kumshauri cha kufanya kwa kuwa wengi wanaofanikiwa huwa wanafanya wanachokijua katika kujikwamua na changamoto zinazosababishwa na uchumi wa Tz.

Biashara, kuwekeza ama kufanya ujasiriamali ni baadhi tuu ya maeneo ambayo mtu mwenye mtaji ama asiyekuwa nao huwa anawaza kujiingiza. Ila kitu kibaya zaidi katika maisha ni kukosa wazo sahihi la kujiendeleza na ndio maana nyenzo kubwa katika kufanikiwa ni maarifa na uthubutu kuhusu mtaji ni kitu cha pili na cha maana sana katika kutafuta mafanikio.

Ningeshauri bwana mdogo aende benki yoyote inayotoa ushauri wa kibiashara akapata kushauriwa namna ya kuwekeza au kifungua biashara kitaalam na wajuzi wa mambo katika sekta ya fedha.
 
24m ni mtaji mkubwa kama ana akili ya kijasiriamali. Kuhusu atafanya nini inategemea na yeye mwenyewe. Aje atulie asome mchezo atajua aanzie wapi.
Kitendo cha kusoma mchezo 10m inakuwa imeshakatika. 24m ni mtaji mdogo sana wamachinga wengi wanao huo mtaji kwa sasa. Mambo yamebadilika sana Tanzania, watu wana pesa sana. Ukitoka nje na 24m ni kuja kuteseka tu ni ngumu kutoboa maana watu siku hizi wanajua kuchungulia fursa siyo kama zamani.
 
Ha ha ha.
 
Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.

Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.

Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.
Hiyo mbona ni hela ya mboga mkuu, milioni 23 hajui azitimiaje? Ndo maana imeonekana hastahili kuendelea kuishi huko
 
Asije na cash huko huko states atafute used iphone au computer ashuke nazo bongo za kutosha

Ajichanganye k/ko makumbusho lazima zitoke
 
Ningekua mimi ndiye yeye. Kwanza ningejifunza vitu hivi..(na assume kama mtu katoka nje basi ana exposure na ni mtu asiye na ugomvi wa vitabu)

1. Ngetumia mwaka mzima kujifunza forex

2. Ningejifunza jinsi ya kuwekeza kwenye crypto currencies..

3. Ndani ya mwaka huo mmoja ningejifunza digital marketing na SEO!

4. Ningejiuliza nini napenda then ningefungua youtube channel ili nitengeneze videos za nnacho penda.. Na kwa sababu nimesha jifunza SEO hapo kwenye namba 3 basi hapa nisinge teseka! Maana knowledge ya SEO ndio ningeitumia ku rank video zangu youtube!!

hii ni nzuri maana in the long run ina faida!

Baada ya hapo ningefanya hivi...

1. Ningetoa 1000usd ni nunue laptop mpya (kama hana kabisa ila kama anayo anaweza acha).. hii ni muhimu maana hii ndio kama jembe shambani, lazima uwe nalo ili ulime!

2. Ningetenga 3000usd na kufund account ya forex (ningefanya hivi baada ya kuhakikisha nime practise vya kutosha na nna strategy inayo eleweka otherwise ningeacha kwanza).

3. Ningetumia 2000usd na kuwekeza kwenye coin kama ENJIN, eCASH, ZIL etc pia ningeangalia hizi meme coins hasa hizi mpya mpya na kuziwekea walau dola 500...

Hapo ningekua nimebakiwa na 4000usd.. then hii 4000 usd ningefanya hivi..

A. Ningetoa 1000usd nifungue kampuni ya digital marketing.. na hapa ningekomaa sana na kazi za freelancing za nje!

B. Kwa sababu nna laptop (rejea namba 1 hapo juu) basi ningefungua youtube channel na ninge hakikisha natenga 500usd kwa ajili ya kununua mic nzuri!

Mpaka hapo nimebakiwa na kama 2500usd hivi! Hii ningeiweka reserve incase of anything pamoja na matumizi ya hapa na pale!
Ushauri wako ni WA kimotiveshno speaker zaidi aisee una mpoteza huyu
 
Yaani ulichobaki nacho ni laptop + usd2500 nyingine sahau kabisaa mkuu
 
Back
Top Bottom