Mtanzania adakwa na mihadarati China

Mtanzania adakwa na mihadarati China

Jamani, hata matamko ya kuzugia hakuna! naona kama watawala wameridhika nayo vile......
 
kama rais kikwete ni mzalendo wa kweli na anaipenda nchi yake ni bora hiyo rist aliyonayo aitaje hadharani ili tuwajue watu wasioitakia mema nchi yetu. Na ili tusiendelee kuwachagua. Badala yake rais amekaa kimya na kuendelea kuikumbtia hiyo orodha maana yake kaendelea kuwakumbatia waovu. Je rais wetu anaipenda nchi yake?au ni mzalendo wa juu juu tu?
 
anabahati hajakamatiwa mainland china huko Guanzhou maana kifo kilikuwa kina muhusu sana
 
sawa, ndio serikali yetu... tutafanyeje?

Yaani hapa ndio pana utata, looks like so far hakuna cha kufanya (sisemi kwa kufurahia). Manake nani mwenye dhamana na nguvu ya kuwachukulia hatua hao wahusika? Ni nani anaweza kuanzisha operesheni kabambe ya kuwatimua timua huko waliko na kuwaleta mbele ya vyombo vya sheria? Kimsingi, ni watawala na watendaji. Ambao kwa sasa wako wapi? Na wao, kama sisi, wako nyuma ya mapazia wanachungulia kama raia mwingine yeyote....Sasa sijui tuandamane? Wa kuandamana naye unamuona ndugu yangu? Labda akina Nkya wenye sauti watuanzishie....

Kwani mheshimiwa si alipewa mahali pa kuanzia? Umemsikia tena? Sasa, kuna mtu atatoka tena kupeleka hint nyingine?
 
Watanzania kwa kulalamika tu hamjambo,mulitangaziwa ajira million,vijana wenu wamepewa ajira ya kubeba mzigo kutokana na elimu yao ndogo,bado tena mnalalamika nini?
 
ukweli ni kwamba kuna wageni wanauziwa pass zetu. kwa nini mtaani unakuta wanaigeria kumi wanakaa chumba kimoja na wanajifunza kiswahili cha kuondokea bongo pale uwanja wa ndege, na kuna ma agent ambao wanawatunza muda huo wote baada ya kukatiwa kitu kidogo. kazi ipo na wakuu wanaelewa mpango mzima ndiyo hivyo tena.

Wa-nigeria wameanza kuja bongo juzi tu. Passport za tanzania zimeanza kuuzwa zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Nilishuhudia enzi hizo nimeenda uhamiaji kutafuta passport. Waliniagiza documents ambazo ilibidi nisafiri kuzitafuta na nyingine nilitakiwa niende hadi mahakamani zikapigwe muhuri, halafu nilivyoenda uhamiaji nilisimama kwenye foleni ambayo haisogei, nilikua naona wahindi tu wanaingia na kutoka na passport na hawapangi foleni. Siku ya kwanza iliisha sikupata kitu ofisi zikafungwa. Ikabidi kesho yake niende tena niandae na rushwa kwa sababu kiburi changu cha kutaka haki hakikufua dafu mbele ya wale maofisa wa passport.

Kuna kipindi passport zilibadilishwa, sasa huko kwenye kubadilisha passport walikuja wahindi mpaka wenyewe wanaona aibu, hata kiswahili hawajui.

Wa nigeria wakinunua passport ya TZ mara nyingi hawasafirishii madawa ya kulevya, huwa wanazitumia kupata viza especially kuja U.S etc kwa sababu ukiwa mnigeria viza ni ngumu kutoka. Hivyo hawazitumii hovyohovyo hizo passport, wanaweza kuzitumia kwenye ma fraud ambayo haukamatwi hapohapo na kuswekwa ndani.
Wapo wengi wana passport za south afrika, nilishakutana na mmoja anaitwa Khumalo nikadhani msouth, kumuuliza ananiambia "my broda dhis is nigerian name" nikaona haina haja ya kubishana nae.
Kuna mmoja alikuwa na jina la kike kabisaa halafu ni mwanaume, hapo nilichoka nao, amefoji passport ya mwanamke.

Halafu m-nigeria hata awe na passport ya TZ kama hana mtu wakumvusha JNIA atakamatwa na hakuna MTZ atakayemwamini mnigeria amfanye punda kwa sababu atakimbia na mzigo na pesa hakuletei ng'o.
Hawa wanaopita JNIA na mzigo mkubwa ni watanzania ambao wanakuwa na watu wao wakuwavusha.
 
ajira za JK na vijana kuwawezesha wadada( AGNESS MASOGANGE) na wakaka wengi tu mizigo ya RITHIWANI
 
"apigwe tu"

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Bintiwangara

Macau siyo Thailand, Macau ni China Special Administrative Region kama ilivyo Hong Kong. Rekebisha heading.
 
Last edited by a moderator:
Ndio imefikia hapa sasa
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1375833164903.jpg
    uploadfromtaptalk1375833164903.jpg
    107.1 KB · Views: 301
Ndio hivyo tena jina la Tanzania linavyozidi kupakwa matope.

  • Kupakwa matope?!?!. Kiswahili kigumu. Usahihi ni kuwa jina la Tanzania linavyochafuka.
 
Eti Prisoner Exchange Makubwa! Kwani haya madudu yalianza mwaka gani? Sembe lilianza kuwa maarufu wakati wa awamu yangapi? Jamani hili janga jingine limetoka wapi? Nacho weza kuchangia nikwamba kama tutaweza kupambana na maadui watatu. Ujinga, Maradhi na Umaskini ndio tutaweza kutatua matatizo yote ya nchi hii! Lakini kama ni taifa la Wajinga na tumeshindwa kuu futa ujinga basi Maradhi, umaskini na matakataka mengine yataendelea kuwepo mpaka mtu wa mwisho kuishi katika nchi hii.
 
kama rais kikwete ni mzalendo wa kweli na anaipenda nchi yake ni bora hiyo rist aliyonayo aitaje hadharani ili tuwajue watu wasioitakia mema nchi yetu. Na ili tusiendelee kuwachagua. Badala yake rais amekaa kimya na kuendelea kuikumbtia hiyo orodha maana yake kaendelea kuwakumbatia waovu. Je rais wetu anaipenda nchi yake?au ni mzalendo wa juu juu tu?

hawezi kuwataja, hiyo alikuwa anawazuga tu kusema atawataja
 
Wapigwe risasi, halafu hivi wakuu kuna sheria ya madawa ya kulevya Tanzania? Kama ipo ninaomba ipitiwe upya ili adhabu ziongozwe ikiwepo ya kifo. Jamii yetu imeharibiwa na madawa na miaka inavyosonga sote tutakuwa tumeathiriwa in one way or the other.
 
Drug traffickin is the big biznes in da world,a lot of tycoons are doin dis ish.
 
Hivi inapita wiki mbili kweli mbongo hajakamatwa nchi za nje kwa ajili ya madawa?
Na swala la serikali ku-sign kubadilishana wafungwa mbona ni njia moja kwa moja kuprove kua serikali inahusika na jamaa wanaofanya hii kazi maana watu watafikiri jamaa wanataka wasafirishe wale waliokamatwa kule kuwaleta huku afu kuzima mambo kimya kimya, Duh! wabongo Bongo imewashinda wanataka maisha ya fastafasta, pamoja na kusikia kelele zooote kila sehemu bado tu mtu bila uoga unajaribu kusafirisha hii mishe, hahaha hata wakikufata kwa bunduki ukipanda ndege ingia chooni flash, fika safe potelea huko, its much better kuliko kudakwa na kutupwa miaka 20 au kuuliwa
 
Back
Top Bottom