Swala la pass za TZ kutoka kiholela lipo lakini usilitumie kama justification kuwaondoa waTZ kwenye uchafu huu, vijana wengi waliokamatwa hivi karibuni ni watanzania tunaowafahamu kwa majina na kucheza nao, wengine ni wasanii na hata waandishi wa habari nao wamejiunga kuna mmoja wa TV na redio maalufu ya Mwanza amedakwa India huko, kwa pamoja tuungane kupaza sauti ya kukemea hili tatizo tusianze kusingizia wageni. Rais wetu alidai anayo orodha mbona amekaa nayo kimya huku tatizo linaongezeka? mbaya zaidi miongoni mwa wanafamilia yake nao wanatajwatajwa kuusika kwa namna moja au nyingine kushiriki. Alipomuondoa kamanda Shekiondo na kumuweka Nzowa kwenye kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya alituahidi kuwa sasa hakuna atakayesalimika lakini matokeo yamekuwa mabaya zaidi, hivi ni kwa nini mpaka leo hii huyu Nzowa anaendelea na wadhifa wake pamoja na kuthibitika kuwa hizo kilo 150 zilizokamatwa Afrika Kusini zilipitia uwanja wetu wa Ndege tena chini ya usimamizi wa afisa wa kudhibiti biashara hiyo? Kukosekana kwa uwajibikaji na ukondoo wa watanzania ndio kiini cha tatizo, vijana wanazidi kudhoofika afya zao, vibaka wanaongezeka na sasa tunatengeneza wafungwa wa kimataifa kwa wingi maana hapa kwetu wanaachiwa tu kwa rushwa.ukweli ni kwamba kuna wageni wanauziwa pass zetu. kwa nini mtaani unakuta wanaigeria kumi wanakaa chumba kimoja na wanajifunza kiswahili cha kuondokea bongo pale uwanja wa ndege, na kuna ma agent ambao wanawatunza muda huo wote baada ya kukatiwa kitu kidogo. kazi ipo na wakuu wanaelewa mpango mzima ndiyo hivyo tena.