mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,502
- 257
Naomba Mungu wawe wanakamatiwa nchi nyingine maana wakikamatwa Thailand alafu tukabadilishana ndio itakuwa kwishney! hatutasikia tena habari zao.
Soma vizuri post uliyojibu mkuu! Unadhani akiuziwa passport ya kitanzania itawekwa jina la kinaijeria?!
Macau leo imekua thailand?mijitu haina akili kabisa asee.
Hii biashara isije ikawa ni kitega uchumi cha chama chetu. Make uchaguzi umekaribia.
Macau leo imekua thailand?mijitu haina akili kabisa asee.
SIKU chache baada ya serikali za Tanzania na Thailand kutiliana saini mkataba wa kubadilishana wafungwa na kutekeleza sheria ya vifungo, raia wa Tanzania amebambwa na dawa za kulevya nchini humo.
Mtanzania huyo aliyefahamika kwa jina moja la Kileo, alikamatwa Jumanne wiki iliyopita katika kisiwa cha Macau akiwa amemeza dawa hizo aina ya cocaine akielekea China.
Kwa mujibu wa maofisa wa polisi wa Thailand, dawa hizo zinakadiriwa kufikia kilogram 1.091, zikiwa na thamani ya dola za HongKong 900,000.
Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, akiwa ziarani nchini alitiliana saini na serikali kubadilishana wafungwa, jambo ambalo baadhi ya wadadisi wa mambo walidai ni hatua ya kuwanusuru vigogo waliofungwa huko kwa makosa ya kujihusisha na biashara hiyo.
Katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi wiki hii kwenye makao makuu ya polisi, msemaji wa polisi nchini Thailand alisema wanamshikilia Kileo (37) aliyekamatwa Jumanne 5:30 asubuhi kwenye eneo la kukagua mizigo katika uwanja wa ndege.
Polisi walimsimamisha baada ya kumtilia shaka na kumweka katika kamera za X-ray ndipo wakabaini kuna kitu tumboni.
Alisema kuwa baada ya kubaini kuwa ana kitu kisicho cha kawaida tumboni alichukuliwa na kupelekwa kwenye hospitali ya Conde de Sao Januario kwa uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa gazeti la The Macau Post Daily la nchini humo lililochapisha habari hiyo, polisi walisema kuwa mshukiwa huyo aliwaambia kuwa alichukuliwa ili kusafirisha dawa hizo kutoka mji mmojawapo ulioko Tanzania mapema mwezi huu.
Taarifa zaidi zilisema kuwa mtuhumiwa huyo awali alipanda ndege kwenda Ethiopia kisha akaenda Thailand mahali alipomeza dawa hizo na baadaye akapanda ndege hadi kisiwa cha Macau ili kuelekea Guangzhou mahali ambapo alitarajiwa kuonana na mchora mpango wa sakata hilo.
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.
Polisi walisema kuwa Kileo aliwaeleza kwamba alilipwa dola za Marekani 7,000 kukubali kumeza na kusafirisha dawa hizo.
Hii ni mara ya pili ndani ya wiki mbili kwa raia wa Tanzania kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumeza na kusafirisha dawa za kulevya.
Mtuhumiwa mwingine alitokea kusini mashariki mwa Afrika na kisha kukamatwa na polisi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Thailand Julai 10 mwaka huu.
Mtuhumiwa huyo pia aliwaeleza polisi hao kuwa alipita akiwa amemeza dawa za kulevya na kuzisafirisha kupitia njia ile ile.
Polisi bado wanachunguza kama watuhumiwa hao walichukuliwa na kundi lilelile linalosafirisha dawa ya kulevya.
Tanzania Daima - 06, July 2013
Ndo jibu, mengine ni blah blah blah ambazo hazina mshiko. Source ni ya mambo yote ni hapo. Ukiwaza sana, utajikuta unapata majibu hivi fedha za kuhonga miezi 3 mfululizo kwenye General Election zinatoka wapi? jibu ni hapo kwenye bold, nachoamini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.Kubadilishana wafungwa kwa manufaa ya nani,ya mfungwa au mwenye mzigo
Hii biashara ya unga ina mkono wa Mkuu wa kaya hata afanye nini na mwanae Ritz,umesaini mkataba wa kubadilishana wafungwa halafu Mtanzania anakamatwa na Mzigo huko huko Thailand Maigizo hayo au Ikulu ya Tanzania ndo masupplier wa hizo dawa make hawafanyi chochote kuhakikisha biashara hiyo inakoma Rais katulia kama hayupo
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi nae ni mdau wa biashara hiyo nini make hazionekani jitihada zinazofanywa na kiongozi huyo yumo ofisini anafanya nini
Au ndio biashara ya chama tawala na serikali yake make hamna jitihada zozote za kukomeshaji ugawaji wa dawa hizi
Tuendelee kuwauzia wanaigeria passport zetu... Hii ndio effect zake
Haka kanjama ka kubadilishana wafungwa ndio JK ana2ona sisi ni watoto kiasi hicho?
Inawezakana ndio huyo maana MACAO ni kisiwa cha CHINA na sio Thailand kama kichwa cha habari kinavyosemaMwingine kakamatwa CHINA jana, kwa kweli hii biashara ina mkono mrefu zaidi ya tujuavyo