Mtanzania adakwa na mihadarati China

Mtanzania adakwa na mihadarati China

Bintiwangara

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
551
Reaction score
287
SIKU chache baada ya serikali za Tanzania na Thailand kutiliana saini mkataba wa kubadilishana wafungwa na kutekeleza sheria ya vifungo, raia wa Tanzania amebambwa na dawa za kulevya nchini humo.

Mtanzania huyo aliyefahamika kwa jina moja la Kileo, alikamatwa Jumanne wiki iliyopita katika kisiwa cha Macau akiwa amemeza dawa hizo aina ya cocaine akielekea China.

Kwa mujibu wa maofisa wa polisi wa Thailand, dawa hizo zinakadiriwa kufikia kilogram 1.091, zikiwa na thamani ya dola za HongKong 900,000.

Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, akiwa ziarani nchini alitiliana saini na serikali kubadilishana wafungwa, jambo ambalo baadhi ya wadadisi wa mambo walidai ni hatua ya kuwanusuru vigogo waliofungwa huko kwa makosa ya kujihusisha na biashara hiyo.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi wiki hii kwenye makao makuu ya polisi, msemaji wa polisi nchini Thailand alisema wanamshikilia Kileo (37) aliyekamatwa Jumanne 5:30 asubuhi kwenye eneo la kukagua mizigo katika uwanja wa ndege.

"Polisi walimsimamisha baada ya kumtilia shaka na kumweka katika kamera za X-ray ndipo wakabaini kuna kitu tumboni.

Alisema kuwa baada ya kubaini kuwa ana kitu kisicho cha kawaida tumboni alichukuliwa na kupelekwa kwenye hospitali ya Conde de Sao Januario kwa uchunguzi zaidi.

Kwa mujibu wa gazeti la ‘The Macau Post Daily' la nchini humo lililochapisha habari hiyo, polisi walisema kuwa mshukiwa huyo aliwaambia kuwa alichukuliwa ili kusafirisha dawa hizo kutoka mji mmojawapo ulioko Tanzania mapema mwezi huu.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mtuhumiwa huyo awali alipanda ndege kwenda Ethiopia kisha akaenda Thailand mahali alipomeza dawa hizo na baadaye akapanda ndege hadi kisiwa cha Macau ili kuelekea Guangzhou mahali ambapo alitarajiwa kuonana na mchora mpango wa sakata hilo.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.

Polisi walisema kuwa Kileo aliwaeleza kwamba alilipwa dola za Marekani 7,000 kukubali kumeza na kusafirisha dawa hizo.

Hii ni mara ya pili ndani ya wiki mbili kwa raia wa Tanzania kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumeza na kusafirisha dawa za kulevya.

Mtuhumiwa mwingine alitokea kusini mashariki mwa Afrika na kisha kukamatwa na polisi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Thailand Julai 10 mwaka huu.

Mtuhumiwa huyo pia aliwaeleza polisi hao kuwa alipita akiwa amemeza dawa za kulevya na kuzisafirisha kupitia njia ile ile.

Polisi bado wanachunguza kama watuhumiwa hao walichukuliwa na kundi lilelile linalosafirisha dawa ya kulevya.

Tanzania Daima - 06, July 2013
 
Police bust another drug swallower from Tanzania


Judiciary Police (PJ) officers have caught another drug swallower from Tanzania on suspicion of trying to smuggle cocaine via Macau into the mainland, this time swallowing 1.091 kg of the drug with an estimated street price of roughly HK$900,000.

In a press conference held at the PJ headquarters on Saturday, a PJ spokesperson said that PJ officers found the 37-year-old suspect, surnamed Kileo, acting suspiciously on Tuesday at about 11:30 a.m. in the airport's luggage collection area.

They stopped the suspect and put him through an X-ray scanner where officers saw something suspicious in his stomach.

He was taken to the public Conde de Sao Januario Hospital Centre for medical examination where it was confirmed that the suspect had swallowed 83 pellets of cocaine, after taking three days to excrete all of the drugs.

According to the spokesperson cited by The Macau Post Daily, the suspect told police that he was recruited by an international criminal organisation in his hometown earlier this month.

He first boarded a flight to Ethiopia and from there to Thailand where he swallowed the drugs. He then flew on to Macau with Guangzhou as his final destination where it was planned he would meet up with members of the racket.

The spokesperson said the suspect would be sent to the Public Prosecution Office (MP) on possible arraignment on drug charges, adding the suspect told police that he was paid US$7,000 to smuggle the cocaine.

This is the second case in two weeks in which a drug swallower from Tanzania has been caught by local police. The other suspect from the southeast African country was also busted by police at the local airport after arriving from Thailand on July 10. That suspect also told authorities that he was recruited to smuggle cocaine using the same route with the same final destination.

The spokesperson said that officers were now investigating the two cases to see if the suspects were recruited by the same gang.(macaunews)

Source: http://www.macaunews.com.mo/content/view/2335/3/lang,english/
 
duuu ajali kazini,sasa imekuwa keroooo
 
sorry lakini naamini hii ya kubadilishana wafungwa yaweza kuwa pia dili la punda wa kubeba... hukawii kukutwa sasa wanakamatiwa Thailand, wanarudishwa in the exchange program na wanaendelea na maisha

I am deeply disturbed kwamba drug business in link katika nyumba kuu kabisa Tanzania... kwa namna moja au nyingine
 
Huyo punda na mapunda wengine wana kila sababu ya kujifunza kutoka kwa yanayowakumba wenzao.
 
CCM wanaangamiza Taifa... Ndugu zangu tuwang'oe wahalifu hawa
 
Mbona kichwa cha habari kinasema THAILAND halafu maelezo yanasema MACAU ambayo ni kisiwa cha China??

Duh! Sijui niifiche wapi sura yangu mbele ya marafiki zangu wa mataifa mengine??
 
Hii biashara isije ikawa ni kitega uchumi cha chama chetu. Make uchaguzi umekaribia.
 
Yaani watanzania tunatia aibu!! Yaani kumbe utajiri wa watu wengi mjini hapa ni sababu ya madawa ya kulevya? Ndio maana unaona magorofa yanaibuka tu utafikiri uyoga. Mwenzangu na mie anajenga nyumba miaka ishirini lakini gorofa linajengwa mwezi tu tena la nguvu! Kumbe.....!!!
 
Soma vizuri post uliyojibu mkuu! Unadhani akiuziwa passport ya kitanzania itawekwa jina la kinaijeria?!


Duh!Kumbe hadi jina wanaforge pia? Kwa nilivyosikia pande za huku nilipo huwa wanazitengeneza fake lakini majina yanakuwa ni yao halisi. Nilikuwa silijui hilo mkuu, basi kazi ipo.
 
Mwingine kakamatwa CHINA jana, kwa kweli hii biashara ina mkono mrefu zaidi ya tujuavyo
 
Kubadilishana wafungwa kwa manufaa ya nani,ya mfungwa au mwenye mzigo

Hii biashara ya unga ina mkono wa Mkuu wa kaya hata afanye nini na mwanae Ritz,umesaini mkataba wa kubadilishana wafungwa halafu Mtanzania anakamatwa na Mzigo huko huko Thailand Maigizo hayo au Ikulu ya Tanzania ndo masupplier wa hizo dawa make hawafanyi chochote kuhakikisha biashara hiyo inakoma Rais katulia kama hayupo

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi nae ni mdau wa biashara hiyo nini make hazionekani jitihada zinazofanywa na kiongozi huyo yumo ofisini anafanya nini

Au ndio biashara ya chama tawala na serikali yake make hamna jitihada zozote za kukomeshaji ugawaji wa dawa hizi
 
Tuendelee kuwauzia wanaigeria passport zetu... Hii ndio effect zake


Kuwa muwazi hao wanigeria unaowasema wanauziwa passpot na nani

Hamna cha mnigeria wote wanaokamatwa na dawa hizo ni watanzania wa hapahapa nchini unadanganya au you are among the supplier or you do not know what you are talking about, better shut your mouth idiot
 
Back
Top Bottom