Mtangazaji wa ITV Mabere Makubi usiangaike na ajira ITV, wiki ijayo utapata ajira nje nakamilisha mazungumzo

Okay..
Kwa hiyo mume mkristo kumiliki zaidi ya mke mmoja ni sahihi?
Ni sahihi, mke anaolewa kimila si lazima kwenda kanisani, kanisa linatambuwa ndoa ya mtu mmoja, lakini mtu mwenye akili timamu na anayezitumia vizuri hawezi kufungwa na kanisa.

Mfano mimi Putin simpendi kabisa kwa kusababisha dunia kuingia kwenye mfumuko wa bei, lakini ameombwa na Papa Fransic waonane Putin amempotezea mpaka leo, hivi ndivyo mwanaume unapaswa kuwa ingawa simuungi mkono kuivamia Ukraine.
 
It's very true, hiyo ndio kazi yetu na hayo ndio maisha yetu.
P
kuna haja ya maslahi ya wanahabari kuboreshwa na kupiganiwa kwa sharti la wao kutii na kufuata sheria na kanuni za taaluma hii.

Wana familia zinawategemea kwa mahitaji, wanauguza, wanasomesha n.k

Natamani wanahabari wetu wawe huru na wasihodhiwe. Wafanye kazi yao kwa uhuru.

Mayalla umewahi kufikiria kuanzisha movement yoyote kutetea maslahi za wenzio kwenye circumstances ngumu kama hizi?!
 
Nawashangaa sana waandishi wazoefu wanaotafuta kazi zama hizi, zama hizi ni za social media makampuni kibao yanahitaji wenye ujuzi wa uandishi wa habari. ni kuji tune tu kidogo na kujiongezea maarifa ya IT hususan kwenye graphics, kazi zimejaa tena wanatafutwa.

Ni vyepesi sana mmwandishi wa habari kujiajiri mwenyewe kwa dunia ya leo kuliko fani yoyote ile. Mwandishi anaweza kuwa freelancer au correspondent wa media kibao zilizojazana.

Tuna tatizo kubwa sana la uelewa Tanzania hii. Tuko finyu sana.

Tanzania bado waandishi wanakimbizana na vibahasha tu. Ni ujinga wa hali ya juu.
 
Nasikitika na nashangaa kuwa muda Wote hukujua kuwa hakuna Watu Hypocrites na Hopeless duniani kote kama Waandishi wa Habari wa Tanzania.
Duh...!
Wewe umeibuka leo Kuwasema kwakuwa tu kuna Tukio limemtokea huyu Makubi ila ulijiiuliza ni kwanini kwa lile Tukio la Mwenzao wa MWANANCHI aliyepotelea mazima Kibiti walinyamaza na kuwaachia tu Waajiri wake MCL ndiyo wampiganie katika Kumtafuta?.
Media, hatukunyamaza, media zote tuliandika, uwezo wetu ni kuandika tuu. hatuna kitu kingine chochote cha kufanya zaidi ya kuandika, au ulitaka tufanye nini?. Baada kifo cha Daudi Mwangosi, media tukataka kususia habari za polisi lakini tulishindwa, na RC wa DSM, Paul Makonda alipovamia Clouds, TEF ikatuhamssishe tususie habari za Makonda, tulishindwa!. Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.
ulitaka tufanyeje,?
Ukitaka tu kujuua Kiini cha tatizo la Waandishi wa Habari wa Tanzania anza Kuliangalia Jukwaa lao la Wahariri ( TEF ) kisha waangalie Kiumakini Watendaji wake Wakuu akina Balile na Wenzake utanielewa nikisemacho hapa.
Hapa labda utueleweshe.
Kitendo tu cha Misingi ya Uandishi wa Habari kuanza Kuharibiwa na Kuingiliwa na Watawala ( hasa Wanasiasa ) na Watu wa Mfumo ( System ) ndiyo Safari yao ya Kifo Kitakatifu cha Kitaaluma ilianzia hapo.
Naomba tufafanulie
Leo hii Vyombo vyote vya Habari pamoja na Waandishi wa Habari nchini Tanzania wamekuwa ni Government Mouth Piece and PR Machine yao badala ya kuwa The Voice of the Voiceless na kusimama katika Kuibua Masuala, Kukosoa na kuonyesha the way forward ya Matatizo Mtambuka ya nchi yetu hii ya Tanzania.
Hii ni tuhuma nzito!. Thibitisha!.
Nina mengi ya Kukuambia kuhusiana na hili na hii Taaluma nzima ya Habari na Mawasiliano ila nikuambie tu usichokijua ni kwamba baada ya Serikali kuonyesha kuwa inawateua Waandishi wa Habari katika Nafasi za Kisiasa na Kiutendaji hivi sasa ukiwa huko News Room katika 99% ya Media Outlets kinachofanyika ni Kusifu na Kunipotezea kwa Watawala ili Wasikike na Wateuliwe
Hii ni tuhuma nzito, Thibitisha!
na wapo ambao mpaka Wanaroga na Kulalwa hovyo ili Wateulowe au wapigiwe Pande wapate Uteuzi badala yake Uteuzi hawaupati ila wanachokipata ni Kuambukizwa HIV na Wao Kuwaambukiza Wenzao mbalimbali katika Vyombo vya Habari tofauti tofauti.
Duh...!, hii ni tuhuma nzito sana!, Thibitisha kwa wale uliowasindikiza kwa waganga, wale uliowashikia miguu wakati wanalalwa, na kuambukizwa HIV na hao waliowalala na kisha ukawashikia tena miguu wakati wakiwabukiza HIV wenzao mbalimbali katika vyombo vya habari tofauti tofauti!.
Tumechelewa na hakuna Media nchini.
Duh...!, kama hakuna media nchini, jee hii media iliyopo na tunayoita ni media ya Tanzania ni nini?!.
P
 
Nawashangaa sana waandishi wazoefu wanaotafuta kazi zama hizi, zama hizi ni za social media makampuni kibao yanahitaji wenye ujuzi wa uandishi wa habari. ni kuji tune tu kidogo na kujiongezea maarifa ya IT hususan kwenye graphics, kazi zimejaa tena wanatafutwa.

Ni vyepesi sana mmwandishi wa habari kujiajiri mwenyewe kwa dunia ya leo kuliko fani yoyote ile. Mwanidishi anaweza kuwa freelancer au correspondent wa media kibao zilizojazana.

Tuna tatizo kubwa sana la uelewa Tanzania hii. Tuko finyu sana.

Tanzania bado waandishi wanakimbizana na vibahasha tu. Ni ujinga wa hali ya juu.
Naunga mkono hoja!.
P
 
Njia nzuri ya kumaliza matatizo ni kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi na siyo kupika habari za uongo za kuonyesha watu hawana kero na wanaishi kwa furaha wakati si kweli.
Rais kwakua ni binadam inatakiwa awe makini sana na watu wanaomsifia kiasi cha kumuaminisha hakosei chochote kwanza anatakiwa ajue watu hao ni wanafiki na wanafiki siku zote wanasura mbili.

Wa Tanzania wana shida sana kumfanyia mtu fitina kiasi Cha kusababisha asimamishwe kazi kisa tu kuusema ukweli ambao haukufurahishi na kusababisha familia za watu ziishi kwenye dhiki na umasikini huko ni kufanya dhulma kubwa sana na siku zote dua ya anae dhulumiwa inapokelewa haraka sana na Mungu haijalishi una madaraka kiasi gani maana hata kina firaun walikua na madaraka makubwa lakin leo hii hawapo tena.
 
kuna haja ya maslahi ya wanahabari kuboreshwa na kupiganiwa kwa sharti la wao kutii na kufuata sheria na kanuni za taaluma hii.
Naunga mkono hoja
Wana familia zinawategemea kwa mahitaji, wanauguza, wanasomesha n.k
Naunga mkono hoja
Natamani wanahabari wetu wawe huru na wasihodhiwe. Wafanye kazi yao kwa uhuru.
This is true, and this is how it should be
Mayalla umewahi kufikiria kuanzisha movement yoyote kutetea maslahi za wenzio kwenye circumstances ngumu kama hizi?!
Kiukweli sijawahi kufikiria kuanzisha movement yoyote, ila kama baada tuu ya kuuliza lile swali Ikulu siku ile, kilichofuatia ni siri yangu!. Jana nimemsikia Mama kasema Rais Samia: Ukinikuna Vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa na kukupuliza. Lakini "Ukinipara...Nakuparura!, kuna kuanzisha movement yoyote kweli?.
P
 
Naunga mkono hoja

Naunga mkono hoja

This is true, and this is how it should be

Kiukweli sijawahi kufikiria kuanzisha movement yoyote, ila kama baada tuu ya kuuliza lile swali Ikulu siku ile, kilichofuatia ni siri yangu!. Jana nimemsikia Mama kasema Rais Samia: Ukinikuna Vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa na kukupuliza. Lakini "Ukinipara...Nakuparura!, kuna kuanzisha movement yoyote kweli?.
P
Kuanzia ulipotangaza kuwa Kada wa CCM huna haja ya kutuambia kuwa hujafikiria kuanzisha movement yoyote, tuambie tu kwamba huwezi kabisa kuthubutu kufanya jambo kama hilo!
 
Back
Top Bottom