Mtangazaji wa ITV Hemed Kivuyo, atosha

Mtangazaji wa ITV Hemed Kivuyo, atosha

Ukewenza ni mgumu...majuto ni mjukuu..hayo ni mane no ya siti binti saad..taifa stars...ilishakunywa sumu...ilichokuwa ilifanya ni kurusharusha miguu tayari kwa kufa......neno moya tuu ni Kuwa...
 
Ukewenza ni mgumu...majuto ni mjukuu..hayo ni mane no ya siti binti saad..taifa stars...ilishakunywa sumu...ilichokuwa ilifanya ni kurusharusha miguu tayari kwa kufa......neno moya tuu ni Kuwa...
Neno moja tu ni kuwa taifa starz ilitaka kuuma chuma kwa meno,ikasahau Nazi haivunji jiwe

Ingawa anatoa maziwa ,lakini ng'ombe akinywa sumu anakufa,ndivyo ilivyokufa Leo
Ana kweli kamba hukatika pabovu,alisema shabaan bin Robert, wakijinasibu kwa madaha!! Huku wakipiga Paso mujaraabu,staz waliambulia dhahama bin dhoruba kutoka kwa naijeria
 
kenda haipo mbali na kumi!!

timu hiyo kutoka mitaa yenye pilikapilika nyingi mtaani kariakoo!!

hamkani hali si shwari kwenye timu hiyo baada ya serikali kutaka kupora eneo la wanajangwani na kujenga bwawa la samaki.

maneno yakasemwa,,masikio yakasikia ,kwani hata ujitahidi vipi,tone la mwisho la mkojo ni la chupi!!
Jamanii wewe jamaa ni noma hadi maneno yote umeyakariri?
 
Hawa ndo watangazaji, siyo kama wale wanaoigana kila kitu. Kwa mfano kuna karedio station kamoja nilishawahi kukasikiliza kapo Arusha wanakaita triple A, yaani watangazaji wake hawana tofauti kabisa na Clouds FM ya Dar es salaam. Kila kitu wanawaiga jamaa. Kuna vimisemo sijui alianzisha nani mfano ni SHIDAA au BONGE MOJA WIMBO n.k sasa hauoni kabisa ubunifu wa hawa watangazaji wanafanana hadi sauti.

Kweli isee kwa kuiga hawajambo utasikia kipindi hichi cha michezo kinaletwa kwenu nimimi jezi namba 5 nisiekuwa na mpinzani hamza kalemara wamemuiga kitenge akiwa radio one.
 
Neno moja tu ni kuwa taifa starz ilitaka kuuma chuma kwa meno,ikasahau Nazi haivunji jiwe

Ingawa anatoa maziwa ,lakini ng'ombe akinywa sumu anakufa,ndivyo ilivyokufa Leo
Ana kweli kamba hukatika pabovu,alisema shabaan bin Robert, wakijinasibu kwa madaha!! Huku wakipiga Paso mujaraabu,staz waliambulia dhahama bin dhoruba kutoka kwa naijeria

we utakua kivuyo.. maana unachokiandika ndo kilekile anachoongea
 
Daaaaah! Alaf tangazo hilo liwe la tajiri aliekufa alafu ndugu wanagombea mali.

Aisee hao ndugu wa marehemu si wataandamana hadi radio one.. by the way nimewaza afu nikacheka
 
Huyu jamaa ni noma, kuna ndugu yangu mmoja shabiki wa simba hataki kabisa kuangalia kipindi cha michezo ITV hivi sasa kwa kuogopa maneno ya Kivuyo.....
 
mi huwa nacheka moyoni ya tbc 1. yuko hassan marini na mtangazaji mwingine sijui nani. wanaigana sauti hadi kichefuchefu.sijui nani anamwiga mwenzie
 
Huyu jamaa ni noma, kuna ndugu yangu mmoja shabiki wa simba hataki kabisa kuangalia kipindi cha michezo ITV hivi sasa kwa kuogopa maneno ya Kivuyo.....

E bwana weee kama timu yako imefungwa usithubutu asilani kumsikiliza Kivuyo.. Atakupa majonzi mengine kwa nahau zake za kuiponda lol..

Maulidi wa Kitenge nae alikuwa ananikosha sana lakini toka ahame Radio 1 sijapata kumsikia tena..
 
Back
Top Bottom