Mtangazaji Maarufu wa RTD Amefariki Dunia Asubuhi Hii!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,475
2,000
Wanabodi,

Nimepokea taarifa kuwa Mtangazaji Maarufu wa RTD, (sasa TBC), ABISAY STEVEN, amefariki dunia asubuhi hii.

Mpashaji habari wangu, amesema, msiba huo umetokea katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa kufuatia kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa zaidi zitafuatia.

Kwa wale wa zamani huyu mtangazaji alikuwa maarufu sana enzi zike za kina David Wakati, Tido Mhando, Seif Salim Mkamba, Edda Sanga, Debora Mwenda etc. Aliwahi kuwa Mkuu wa Idhaa ya Biashara chini yake wakiweno Charles Hilary na Julius Nyaisanga.

Mpaka Mauti yalipomkuta alikuwa bado ni muajiriwa wa TBC.

Poleni wafiwa.

Mungu aiweke Roho ya Abysai Steven Uronu, Mahala Pema Peponi, Apumzike kwa Amani....
Amen!.

UPDATE: 1.
TBC wametoa update kwenye taarifa yao ya habari ya saa 2 usiku.

Marehemu atazikwa kijijini kwao Hai mkoani Kilimanjaro siku ya Jumanne.

Heshima za Mwisho ni Jumatatu saa 4 asubuhi nyumbani kwake Temeke Mikoroshoni na baadae kusaliwa Kanisa la KKKT Temeke Vetenari.

Abysai Steven alizaliwa mwaka 1951 huko Moshi. Aliajiriwa na RTD mwaka 1970 kama Mtangazaji Msaidizi Daraja la III. Alipanda ngazi mpaka mauti yalipomkuta akiwa ni Mtangazaji Mwandamizi Mkuu Daraja la I.

Marehemu ameacha mjane, watoto 3 na mjukuu 1.

Rip Abysai Stephen.

UPDATE: 2.
Msiba umehamishiwa kwenye nyumba yake nyingine iliyoko Banana Kitunda.

Ili kupunguza mahangaiko, mwili wa marehemu utatoka hospitali ya Muhimbili saa 5 asubuhi moja kwa moja kanisa la KKKT Vetenari kwa misa na heshima za mwisho.

Baada ya hapo, safari ya kuelekea Hai, Moshi Kilimanjaro kwa mazishi, itaanza.

Rip Abysai Stephen.

UPDATE:3.
Heshima za mwisho kwa Abysai Stephen zimemalizika hapa kanisa la KKKT Vetenary Temeke ambazo zimehudhuriwa na record ya umati wa watu kwa mtangazaji wa RTD.

Umati huo umejumuisha viongozi wa vyama na serikali, wafanyakazi wa TBC, waandishi na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari na kukolezwa na idadi kubwa ya watangazaji wakongwe wa iliyokuwa RTD.
Msafara kuelekea Hai Kilimanjaro umeanza.

RIP A.S
 

Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,623
2,000
Thanx kwa taarifa..namkumbuka sana huyu bwana!! Umelitumikia taifa vyema katika nyanja ya habari. R.I.P
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,419
2,000
Duh! Namkumbuka sana huyu moja ya watangazaji wenye unique identity kilafudhi na sauti,Makamanda wanakwisha! R.I.P
 

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,414
1,195
Duh! Poleni sana familia ya Abisaay, poleni TBC. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Kuna wakati nilisafiri kikazi Songea, huyu bwana alinisaidia sana wakati huo akiwa mwakilishi wa RTD Kanda ya Kusini. Alikuwa na mwenzake fundi mitambo akiitwa Silvanus Haule.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom