Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,552
- 19,420
Mkuu kwani hujui kwamba hata uhuru alipigania peke yake
il hali watu chungu mzima waliacha kazi ku sabatage wakoloni
Haya ndiyo matokeo ya propaganda za Mohamed Said.
Historia haisemi kuwa Nyerere alipigania uhuru peke yake bali inasema aliongoza mapambano ya kudai Uhuru. Ukiongoza unakuwa na wafuasi wengi wanaosadia kufikia lengo hilo. Mandela wa SA alifungwa miaka 26 jela lakini mapambano ya uhuru yaliendelezwa kwa inspiration alioanza na mpaka leo anapewa credit ya kuongoza mapambano hayo. Hata ukimchukia Nyerere ni vizuri pia uwe mwungwana na kutoa credit panapohusika. Hata jeshi letu lina askari wengi sana lakini lilipoenda kutuliza maasi huko Komoro, credit zilikuja kwa Kikwete kwa vile ndiye aliyekuwa Amiri jeshi mkuu. Jeshi la Marekani lilipomuua Osama, credit zilikwenda kwa Obama kwa vile ndiye aliyekuwa Amiri jeshi na mpaka leo hujui ni askari yupi aliyempiga risasi na kumwua Osama