Mtanganyika wa kwanza kuhutubia UN

Nov 13, 2010
91
7
Inasemekana Nyerere si mtanganyika wa kwanza kuhutubia UN, na kwamba wapo waliomtangulia lakini wazee wakajikomba kwa babu wakapindisha historia......kuna mwenye data!

Kitambo nlipata kujuzwa kuwa kuna mtanzania mmoja kutoka jamii moja iliyoko Kaskazini mwa Tanzania alienda mpaka Umoja wa mataifa(UN) kudai uhuru wa Eneo lake alilotoka na sio Uhuru wa Tanzania Nzima.
Ni ya kweli hayo? mwenye historia juu ya jambo hili Atujuze basi.
 
Mkuu kwani hujui kwamba hata uhuru alipigania peke yake
il hali watu chungu mzima waliacha kazi ku sabatage wakoloni
 
Inasemekana Nyerere si mtanganyika wa kwanza kuhutubia UN, na kwamba wapo waliomtangulia lakini wazee wakajikomba kwa babu wakapindisha historia......kuna mwenye data!
siasa za CUF hizo (itikadi ya CUF ni kuleta majungu kwa kuendesha siasahistoria, mara dhuluma ya Nyerere dhidi ya wazanziba,mambo ya HANGA na ushiriki wa SEIF MAALIM kumdhalilisha Rais JUMBE)
vijana tunataka siasaleo hoja bin hoja kwa issues zenye maslahi kwa taifa na sio tantarira za kihistoria.
 
Marytina tuheshimiane, mimi sifanyi siasa bali nafanya utafiti. Na huwezi kupingana na historia. Utapata wapi siasa leo usipoanzia jana. Ignorance of history made man to repeat same mistakes.
 
Mkuu kwani hujui kwamba hata uhuru alipigania peke yake
il hali watu chungu mzima waliacha kazi ku sabatage wakoloni

Wewe sasa naona unachuki binafsi na nyerere!hakuna sehemu yoyote katika historia ya Tanganyika inayosema nyerere alipigania uhuru peke yake!tuache chuki binafsi!!
 
Marytina tuheshimiane, mimi sifanyi siasa bali nafanya utafiti. Na huwezi kupingana na historia. Utapata wapi siasa leo usipoanzia jana. Ignorance of history made man to repeat same mistakes.
Tanzania bila Zanzibar haiwezekani kwani Tanzania ni zao la nchi 2 ZANNIBAR +TANGANYIKA,Labda umaanishe Tanganyika bila Zanzibar inawezekana.
 
siasa za CUF hizo (itikadi ya CUF ni kuleta majungu kwa kuendesha siasahistoria, mara dhuluma ya Nyerere dhidi ya wazanziba,mambo ya HANGA na ushiriki wa SEIF MAALIM kumdhalilisha Rais JUMBE)
vijana tunataka siasaleo hoja bin hoja kwa issues zenye maslahi kwa taifa na sio tantarira za kihistoria.

Ulisema ni kweli lakini taifa ambalo halina historia ni taifa gani? angalia wenzetu wana sheherekea uhuru walioupata miaka mia mbili iliyopita lakini wanaheshimu historia yao. Kuna upotoshwaji mkubwa wa historia yetu kuna watu kama kina tedy kasela bantu hawajatendewa haki na historia ya nchi hii. Ikiwa historia haina mpango basi suala la Richmond limebaki historia hali kadhalika hukumu kwakuwa imepita tuiche ibaki historia tulipe tunyamaze? Muwe mnafikiria impact ya ujumbe unaotoa. Miaka mia ijayo mtu kama Rostam atakuja kuandikwa kwenye historia pengine tofauti na mnavyomjadili humu JF atakuja andikwa alikuwa mpambanaji mwenye uchungu na mengi mengineyo itabidi tukubali historia!

Au ulike wakati historia ya CUF isimtaje James Mapalala eti kwa kuwa ni Mkristo na wao wanasemwa ni chama cha kiislamu! huu utakuwa ni uwendawazimu. Au ifike wakati watu wasiseme kuwa mzee Mtei ni mwanzilishi wa CDM ilikuficha wasiojua historia kukihusisha chama na uchagga lazima historia iwe intact si ya nchi si mtu mmoja mmoja, si ya chama na wala si ya nchi.
 
Marytina tuheshimiane, mimi sifanyi siasa bali nafanya utafiti. Na huwezi kupingana na historia. Utapata wapi siasa leo usipoanzia jana. Ignorance of history made man to repeat same mistakes.

Utafiti wako utakuwa mgumu sana mkuu kwasababu ya "Tanzania bila Zanzibar inawezekana :israel:" itakuchukua miaka hamsini kujua kuwa neno Tanzania linajumuisha neno Zanzibar ambayo ni nchi na kabla ya hapo yaani before 1964 hakukuwa na kitu kinaitwa Tanzania. NA ulivyo mbishi hadi ukijakukubali utafiti wako utakuwa umepoteza maana.

Tanzania bila Zanzibar inawezekana :israel: inanitia shaka na wigo wa uelewa wako na kuwa hukusoma somo la historia shuleni.
 
Back
Top Bottom