Mtandao wa Zitto Kabwe ni mkubwa

Mtandao wa Zitto Kabwe ni mkubwa

Status
Not open for further replies.
Hiki chama hakiwahusu kabisaa! Jengeni cha kwenu!
CDM ina misingi yake ya uongozi na ukiruhusu misingi hiyo kudondoka chama kitakufa, maana ndicho wanachotamani magamba! Wao badala ya kufanya kazi wanaangaika na vyama vya upinzani kana kwamba ndivyo vinavyotawala nchi!
Hao mnaowashabikia hakuna anayewajua isipo kupitia CDM. Watamwagwa kama hayo masalia mliochukua.
Ushauri wangu kwa magamba acheni kutumia nguvu kubwa kuomba CDM ife badala yake tumieni nguvu hizo hizo kuondoa ufisadi,rushwa, elimu duni, magonjwa, wizi wa maliasili zetu na mambo mengine yanayozolotesha maendeleo ya nchi.
Vyama vya upinzani havitakufa mlifahamu hilo!
Mkiambiwa ukweli inawauma sana, tupeni chama sisi magamba tukiendeshe halafu mtuhoji juu ya mapato na matumizi,
Ikiwa tunaongoza ukaguzi wa fedha kitaifa tushindwe za chama.
 
Ha ha kwa hiyo Zitto ndio mwenyekiti kwa kupitia nje ya vikao kwa maoni yako Zitto tunamgoja awe mwenyekiti wa chadema 2050 atakapo kuwa ameenda jando mnafiki na mzandiki atasikia historia ya kuwa mwenyekiti alidekezwa dekezwa sana wananchama tutahakikisha uchaguzi ujao tunachagua mwenyekiti stahili yeye atabaki mwanacham kama anavyotaka kwa sababu kama mbowe hafai au Dr Slaa hafai na yeye hafai kwa sababu ni sehemu yao
 
Mkiambiwa ukweli inawauma sana, tupeni chama sisi magamba tukiendeshe halafu mtuhoji juu ya mapato na matumizi,
Ikiwa tunaongoza ukaguzi wa fedha kitaifa tushindwe za chama.

Jjaribu kuwa na soni wewe ni nani kwenye CCM , mwenye ushawishi na uwezo wa kuvuta hisia kama Jakala lakini leo mwenyekiti wako wa CCM aliyekulia humo maisha yake yote anawaandaa kisaikolojia maana anajua 2014 munapigwa asubuhi na mapepa na 2015 munazikwa rasmi wewe wakataa utaendesha chama gani wakati chama chako cha wala rushwa JK 2013 October 22
 
Kama kuna viongozi wanaojipanga katika harakati za kutawala nchi miaka ijayo basi mbunge wa kigoma kaskazini mh Zitto Zuberi Kabwe ni namba moja.

Kwanza alianza kwa kuweka mikakati ya kuwa mwenyekiti wa chama kwa kuandaa kambi kabambe ya akina Mtela, Shonza, Msafiri Mtemelo na wengineo wengi.

Sasa nimeshikwa na butwaa kuona amethubutu hadi kumshika mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Mwigamba yaan mahali ambapo chadema wanajivunia zitto amepachika mtawala, sikwambii mikoa iliyopo ukanda wake kama tabora, shinyanga. Na kama amefaulu kuweka kiongozi arusha, inawezekana vipi kwa Mbowe kuwa na viongozi katika mikoa mingine?

Minadhani umefika wakati wana chadema kuachana na kupambana na zitto na badala yake kuweka nguvu kubwa katika kukijenga na kukiimarisha chama kwa kuruhusu demokrasia kutawala ktk uendeshaji wa chama ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea.

Hivyo hakuna haja ya kufukuza kila mtu anayejaribu kukikosoa uendeshaji wa chama. Jk kama angewatimua akina Sitta,januari,mwakyembe ccm ingekufa mapema lakini alitumia busara za kuwapa nafasi za kiutendaji ili waweze kufanya marekebisho mahali ambapo wengine walijikwaa.

Wito wangu kwa Mbowe na Dr Slaa, mmefanya kazi kubwa ya kukijenga na kukiimarisha chama sasa tunawaomba umefika mda kwa wengine kushika madaraka na kukiongoza chama, mbona Mzee Mtei na Bob Makani walishika uongozi kwa vipindi vya miaka mitano tu vipi wewe?

Nashukuru sana!
PUmba tupu. Na wewe upo kwenye mtandao wa ZZK. Nataka niwaambie kuwa kwa kuwa mnataka kuupata uongozi kwa hila kamwe hamfiki kokote. Mtapukutika wote
​
 
Hivi CCM mnatoa wapi mapenzi ya dhati na Zitto angali si mwanachama wenu? Why??? ...mnapata wapi kuona ya Zitto kuliko ya wengine wote walioko CDM? Nimeamini jamaa mnamlipa pesa nyingi sana ila kamwe hatokuja kuweza chini ya mapenzi yake Mungu wanaowauza wenzao kama kule Misri utumwani ipo siku watashindwa tu.. CDM for life&for victory.
 
Hata mimi huwa najiuliza......yaani kwa tathmini ya haraka haraka huyu dogo anaungwa mkono na robo tatu ya watanzania wa itikadi zote za kichama, dini bila kusahau makabila.

Jamaa akiamua kuazisha chama chake na kugombea uraisi, atakayekuwa mpinzani/wapinzani wake atalazimika kujiondoa kabla ya siku ya uchaguzi.

...Zitto ni turufu ya Chadema kwenda kwenye level ya kuweza kutawala,ni mwanasiasa anayeweza kuyavuta makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwepo ata ndani ya CCM kuelekea kwenye common goal,aina ya siasa za Mbowe na Dr Slaa zitaishia tu kuwafanya wawe chama kikuu cha upinzani lakini sio kutawala...

...Kama Chadema wanahitaji kuingia ikulu basi hawana budi kuitumia aina ya siasa za Zitto...
 
Kama kuna viongozi wanaojipanga katika harakati za kutawala nchi miaka ijayo basi mbunge wa kigoma kaskazini mh Zitto Zuberi Kabwe ni namba moja.

Kwanza alianza kwa kuweka mikakati ya kuwa mwenyekiti wa chama kwa kuandaa kambi kabambe ya akina Mtela, Shonza, Msafiri Mtemelo na wengineo wengi.

Sasa nimeshikwa na butwaa kuona amethubutu hadi kumshika mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Mwigamba yaan mahali ambapo chadema wanajivunia zitto amepachika mtawala, sikwambii mikoa iliyopo ukanda wake kama tabora, shinyanga. Na kama amefaulu kuweka kiongozi arusha, inawezekana vipi kwa Mbowe kuwa na viongozi katika mikoa mingine?

Minadhani umefika wakati wana chadema kuachana na kupambana na zitto na badala yake kuweka nguvu kubwa katika kukijenga na kukiimarisha chama kwa kuruhusu demokrasia kutawala ktk uendeshaji wa chama ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea.

Hivyo hakuna haja ya kufukuza kila mtu anayejaribu kukikosoa uendeshaji wa chama. Jk kama angewatimua akina Sitta,januari,mwakyembe ccm ingekufa mapema lakini alitumia busara za kuwapa nafasi za kiutendaji ili waweze kufanya marekebisho mahali ambapo wengine walijikwaa.

Wito wangu kwa Mbowe na Dr Slaa, mmefanya kazi kubwa ya kukijenga na kukiimarisha chama sasa tunawaomba umefika mda kwa wengine kushika madaraka na kukiongoza chama, mbona Mzee Mtei na Bob Makani walishika uongozi kwa vipindi vya miaka mitano tu vipi wewe?

Nashukuru sana!

duplicate
 
PUmba tupu. Na wewe upo kwenye mtandao wa ZZK. Nataka niwaambie kuwa kwa kuwa mnataka kuupata uongozi kwa hila kamwe hamfiki kokote. Mtapukutika wote
​

Msije kupukutika nyinyi kwani tayari tumejipanga, we ujiulizi ikiwa tuna mwenyekiti wa arusha vp kuhusu anaokula nao Mbowe meza moja ni wangapi wapo upande wetu?
 
Zamani nilikuwa namfagilia sana Zitto kutokana na misimamo dhidi yake ya Ufisadi lakini tangu atekwe na mafisadi nimepoteza imani naye kabisa.

Nina jamaa zangu watu wa CCM walio karibu kabisa na vigogo wa CCM huwa wananipa data za ndani kabisa kuhusu Wanasiasa mbalimbali wanasema wanamhofia Dr Slaa tu peke yake .

Unajidanganya. Slaa ni choka mbaya sana kwa sasa.
 
Zitto ndio habari ya mjini,yaani nipo hapa moro kila kijiwe watu wanamjadili zitto na namna anavyoweza kuwa kete pekee ya kuipeleka chadema mbele.

CHADEMA ni taasisi hakuna kete pekee labda chama cha kufikirika.Acha uongo
 
...Zitto ni turufu ya Chadema kwenda kwenye level ya kuweza kutawala,ni mwanasiasa anayeweza kuyavuta makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwepo ata ndani ya CCM kuelekea kwenye common goal,aina ya siasa za Mbowe na Dr Slaa zitaishia tu kuwafanya wawe chama kikuu cha upinzani lakini sio kutawala...

...Kama Chadema wanahitaji kuingia ikulu basi hawana budi kuitumia aina ya siasa za Zitto...

Zitto turufu yake na familia yake CCM anawavuta kwa sababu kashibishwa mshiko, na wanamtumia lakini mission zake zote zinabuma yuko under 24 surveillance ha ha angojee mwenyekiti wa ccm ampishe uenyekiti 2015 atakapokuwa Raisi kwa ticket ya CCM
 
Mbona hili suala la uchaguzi inaonekana kama linapigiwa upata sana na watu wa upande uleee, nini kimejificha katika uchaguzi wa CHADEMA!? Isije kuwa ndo yale maneno ya waheshimiwa flani " CHADEMA itakufa mwaka huu". Tafakarini wanachadema, kabla ya kucheza kila mdundo unasikiwa, Kwa jicho la mbaaali, naona kama kuna mkono wa adui.
 
Zitto sasa yupo Ufaransa ,wakati mbowe yupo dar,wakati mbowe anarusha ngumi kumpiga Mwigamba, Zitto anashughulika na mambo ya kimataifa. Zitto ni msomi anaejua thamani ya elimu yake. Na pamoja na majukumu yote hayo utaambiwa Zitto kasoma vitabu kadhaa ili kujiongezea maarifa, wakati mbowe kaishia kusoma gazeti la Tanzania daima na mawio. Huwezi linganisha akili ndogo iliyoambulia zero na akili kubwa ilipata div one kwa ngazi zote.

Hatuhitaji kupamba vyeti vya div 1 ofisini bali tunahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kututoa katika mikono ya wanyang'anyi ccm.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mbona hili suala la uchaguzi inaonekana kama linapigiwa upata sana na watu wa upande uleee, nini kimejificha katika uchaguzi wa CHADEMA!? Isije kuwa ndo yale maneno ya waheshimiwa flani " CHADEMA itakufa mwaka huu". Tafakarini wanachadema, kabla ya kucheza kila mdundo unasikiwa, Kwa jicho la mbaaali, naona kama kuna mkono wa adui.

Adui ataaibika vibaya sana.
 
point muhimu,kocha ukiwa na wachezaji wengi wazuri,ndio ushindi unakuwa mkubwa,angalia buyern munich kila mtu anafunga,so CHADEMA chukueni ushauri watu wote muwakeke katika timu yenu ili ushi uwe mkubwa
 
Mwenyekiti wa CHADEMA hatokani na matamanio na mipango ya Lumumba

CHADEMA kinachagua viongozi kwa mujibu wa katiba.

Katiba gani inayoongozwa na misingi ya kidemokrasia inampa Mbowe nguvu na mamlaka ya kuwa mwenyekiti mwaka wa 12 huu?
Je katiba ya namna hii inafaa katika nchi ya kidemokrasia?
Ni chama gani cha siasa duniani kinachofuata misingi ya demokrasia hakina ukomo wa madaraka?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom