Hiki chama hakiwahusu kabisaa! Jengeni cha kwenu!Tatizo la viongozi wengi wa Africa wamejaa unafiki na uzandiki.chama cha demokrasia leo kinaiona demokrasia kama msumari wa moto.mtu anapobanwa na kukosa fursa ya kutoa maoni yake siku zote hutafuta mbinu mbadala,hiki ndicho alichofanya Mwigamba na naamini wapo viongizi wengi chadema wenye manung`uniko zaidi hata ya mwigamba.
Mabadiliko ni lazima,kama mbowe na slaa ni wahafidhina basi mwisho wa hila zao umefika."KIVULI KINAISHI" tutashuhudi viungo vya bi kilembwe vikiukana mwili wake na hapo ndio utakuwa mwisho wa viongozi madhalimu wanaotuhadaa kwa msamiati wa ukombozi ,huku wanajinufaisha wao na familia zao.
Chadema ukitaka kosana nao wambie watubu dhambi na wakili ukweli hapo ugomvi wake ni balaa.
Kama kuna viongozi wanaojipanga katika harakati za kutawala nchi miaka ijayo basi mbunge wa kigoma kaskazini mh Zitto Zuberi Kabwe ni namba moja.
Kwanza alianza kwa kuweka mikakati ya kuwa mwenyekiti wa chama kwa kuandaa kambi kabambe ya akina Mtela, Shonza, Msafiri Mtemelo na wengineo wengi.
Sasa nimeshikwa na butwaa kuona amethubutu hadi kumshika mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Mwigamba yaan mahali ambapo chadema wanajivunia zitto amepachika mtawala, sikwambii mikoa iliyopo ukanda wake kama tabora, shinyanga. Na kama amefaulu kuweka kiongozi arusha, inawezekana vipi kwa Mbowe kuwa na viongozi katika mikoa mingine?
Minadhani umefika wakati wana chadema kuachana na kupambana na zitto na badala yake kuweka nguvu kubwa katika kukijenga na kukiimarisha chama kwa kuruhusu demokrasia kutawala ktk uendeshaji wa chama ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea.
Hivyo hakuna haja ya kufukuza kila mtu anayejaribu kukikosoa uendeshaji wa chama. Jk kama angewatimua akina Sitta,januari,mwakyembe ccm ingekufa mapema lakini alitumia busara za kuwapa nafasi za kiutendaji ili waweze kufanya marekebisho mahali ambapo wengine walijikwaa.
Wito wangu kwa Mbowe na Dr Slaa, mmefanya kazi kubwa ya kukijenga na kukiimarisha chama sasa tunawaomba umefika mda kwa wengine kushika madaraka na kukiongoza chama, mbona Mzee Mtei na Bob Makani walishika uongozi kwa vipindi vya miaka mitano tu vipi wewe?
Nashukuru sana!
Matamanio mengine humu yanachekesha sana
Zamani nilikuwa namfagilia sana Zitto kutokana na misimamo dhidi yake ya Ufisadi lakini tangu atekwe na mafisadi nimepoteza imani naye kabisa.Nina jamaa zangu watu wa CCM walio karibu kabisa na vigogo wa CCM huwa wananipa data za ndani kabisa kuhusu Wanasiasa mbalimbali wanasema wanamhofia Dr Slaa tu peke yake .
Hiv kwa nini watu wa ccm wa buku 7,cc na nec wanampenda sana zitto?
Mbowe anajua fika hawezi shinda nafasi ya uenyekiti tena kama uchaguzi utafanyika siku za karibuni
Makada wa CCM wameungana kumpigania Zitto awe mwenyekiti cdm.
Naukitaka CCM wakutoe macho na kukung'oa kucha kwa koleo bila ganzi basi washauri waachane na rushwa na ufisadi!Chadema ukitaka kosana nao wambie watubu dhambi na wakili ukweli hapo ugomvi wake ni balaa.
CHADEMA kimeanzishwa kwa misingi ya kilaghai hata vijana wake kupitia BAVICHA wanaendeleza huo ulaghai.Kupambana na zitto kabwe ni sawa na kupambana na nguvu ya Mungu iliyoweza kuumba mbingu na dunia. Kina Yericko Nyerere wamejaribu mpaka kutengeneza id fake jason bourne na kumchafua zitto kwa kutengeneza propaganda ath katika wale mafisadi walioficha pesa uswisi nae yumo lakini holla! Wengine kina Ben Saanane wametumia mpaka sumu holla! Dah zito ni mpango wa Mungu jamani.
mbowe na slaa ni wapambanaji wazuri hamna sababu ya kuwawekea miaka 10 ya kuongoza chama,waongezewe hata ifike miaka 30.