Roger Sterling
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 13,010
- 23,656
Kinachosumbua watanzania ni kuanza kusema maovu ya mtu pale anapoingilia anga zao. Mimi ni kati ya watu ambao wanadhani Makonda ni mwepesi sana kwenye kazi ya mkuu wa mkoa, anapaswa kuwa kwenye uenyekiti wa mtaa au vijiji. Ila kuanza kusema maovu yake baada ya aka ka-operesheni kake ka madala ya kulevya itaonekana kama ni kutaka kumpunguza nguvu, mimi nadhani kuna haja ya kuwa-expose watu waovu mapema kabla ya kusubiri hatua kama hii ya Makonda.
Kinachowasumbua watanzania wengi ni kuongozwa na hisia na mihemuko, na sio vichwa vyao. Tatizo sio timing, sababu, wala aliye nyuma ya tuhuma, bali tuhuma zenyewe. Tuhuma zinazotolewa ni za msingi, na zinatakiwa kutolewa ufafanuzi na uchunguzi kwa sababu zinamhusu kiongozi wa uma, na zinahusika na 'vita' inayoendelea.