Habari za wakati huu ndugu msomaji wa blog hii
www.jamii.app/JFUserGuide? Ni siku nyingine nzuri tuliyo barikiwa kuiona na kuiishi. Hakika ni jambo la kushukuru sana kuiona siku nyingine.
Leo kwenye chapisho langu naenda kujibu swali ambalo watu wengi huuliza au kuomba ushauri sana kwa watu. Swali hilo ni hili βNina mtaji kiasiβ¦. Kwa mtaji huo biashara gani inayolipa nifanyeβ?. Ungana nami mpaka mwisho kwenye chapisho hili nitakalo jibu swali hilo kulingana na uzoefu wangu na uelewa wangu.
Kwanza kabisa ukiona mtu anasema βnina mtaji kiasiβ¦. biashara gani inayolipa naweza kufanya kwa mtaji huoβ? Ukiona unaulizwa swali hilo tambua kuwa unachoombwa hapo ni wazo la biashara. Muulizaji anakuomba umpe wazo la biashara anayo weza kufanya na itakayomlipa kulingana na kiwango cha mtaji alionao. Hii ndiyo maana yake.
Biashara gani ya kufanya..?
Mara nyingi wengi ya wanao uliza swali hili ni watu ambao aidha wamepata hela ya ghafla na inawezekana wanakuwa wamepata hela ambayo hawakutarajia kupata hivyo hela imekuja tu. Pili ni watu ambao walitarajia kupata hela hiyo ila wakati wanatarajia kupata hela hiyo walikuwa hawaiwekei malengo hela hiyo. Hivyo walitarajia kupata hela hiyo na wamepata ila hawajui wafanyie nini hela hiyo. Na tatu ni watu ambao tayari wana hela. Kuna watu ambao tayari wana hela. Kuna biashara au kazi wanazofanya ambazo zinawaingizia hela. Sasa anakuwa hana wazo la kufanya biashara au kazi nyingine. Kuna kipindi kinafika kwa binadamu ambapo anakuwa na pesa kiasi kwamba anakosa mawazo mapya ya kuendeleza biashara zake.
Kwenye makundi haya matatu, watu wote wana shida inayofanana ingawa wana tofautiana kwenye uzoefu. Kundi la tatu lenyewe lina uzoefu zaidi. Na sema shida yao ni moja kwa sababu wote hawa wanatafuta wazo jipya la biashara ya kufanya.
Siyo vibaya kuomba ushauri wa wazo gani la biashara unayoweza kufanya na ika kulipa. Lakini inategemea unapo amua kuomba ushauri wewe ulikuwa na wazo gani kabla la kufanya biashara. Kwanini nasema hivi?
Nasema hivi kwa sababu wazo la biashara utakayofanya na ikakulipa litazalishwa na kutoka kwenye akili yako mwenyewe. Wazo la biashara utalizalisha na utalitoa kwenye akili yako kwa aidha kwa kuona, kwa kusikia, kwa uzoefu wako na kwa akili yako kubuni wazo jipya la biashara ambayo haikuwahi kuwepo.
Kwa maneno mengine wazo zuri la biashara itakayo kulipa na utakayofanya kulingana na mtaji ulio nao litatoka ndani yako wewe mwenyewe. Hili ndiyo wazo bora la biashara utakayoweza kuifanya na ikakulipa vizuri. Kwa hiyo kama kesho una mtaji umepata ghafla ambao hukutegemea kupata, au ulitegemea kupata mtaji huo lakini hukuwekea lengo/wazo la biashara utakayofanya pindi hela hiyo ikitoka, au wewe tayari una uzoefu wa kufanya biashara/kazi fulani inayolipa na pesa kwako siyo shida ila shida ni akili yako haitoi mawazo mapya ya biashara, basi tambua kabla hujaomba ushauri kwa watu juu ya biashara gani ufanye kwa mtaji waβ¦. Tambua kuwa mtaji wa biashara ya ukweli na itakayo kulipa itazalishwa na kutokea kwenye akili yako mwenyewe. Jambi muhimu ni wewe kujua namna ya kuamsha akili yako iendelee kuja na mawazo mapya kila unapohitaji.
Kuwa na wazo la biashara ulilozalisha mwenyewe kwenye akili yako ni muhimu kwani utakuwa tayari kutafuta maarifa na kujifunza juu ya wazo hilo jipya la biashara.
Sijasema usiombe ushauri kwa watu. Omba ushauri kwa watu wa kueleze namna ya kutekeleza wazo la biashara yako ambalo akili yako tayari ishalizalisha. Hii itakuwa rahisi kwako kupambana na changamoto za biashara na pia itakuepusha na hali ya kukosa hamasa pindi mambo yakiwa hayaendi kama unavyo taka yaende kwenye biashara yako.
Kabla hujaomba wazo la biashara kwa watu wengine tambua kuwa una mgodi mkubwa kwenye kichwa chako ambao kama utautumia utakuletea wazo au mawazo bora ya biashara utakayoweza kufanya. Namna pekee ni wewe kujua namna ya kujua kutumia mgodi huo ili uwe utakuletea mawazo bora ya biashara.
Moja ya faida ya kuja na wazo la biashara wewe mwenyewe ni kukuepusha na majuto na lawama pindi ikitokea wazo la biashara yako haliendi kama ulivyo shauriwa na watu. Kwani siyo watu wote unao waomba ushauri wa juu ya wazo la biashara unayotaka kufanya watakupa ushauri sahihi. Wengine watakupa ushauri kwa lengo la kujinufaisha wao na wengine watakupa ushauri wa biashara ya kufanya hata kama hawana maarifa yoyote ya biashara na kuweza kutoa ushauri.
Ni hayo tu kwa leo ndugu msomaji wa blog hii ya . Endelea kutembelea blog hii kujifunza zaidi machapisho bora kila siku.
Unaweza kuwasiliana nami kwa kutuma ujumbe Whatsapp kwenye namba hii:
0769770288 au unaweza kutuma ujumbe kwenye email ambayo ni: