Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Nakusaidia kwa mawazo yangu kidogo yakikusaidia ninunulie kahawa na mandazi mbili......
shilingi milion moja utafanya hivi.
1.Kibanda cha CD(video library)
Meza ya computer: 40000/
Computer: 250,000/=
subwoofer ndogo: 60,000/=
Hard disk: 100,000/=
Shelf za CD: 50000
Plastic chair 3pcs: 15000x3=45000/=
Memory 1Gg original 5x5500= 16500/=
memory 2gb og 5= 30000/
4GB memory = 21000/=
CDBongo movie 1500X30= 45000/=
DVD collectin 1000x20= 20000
Season Movie 20x1000= 20000
Kodi 30000x3= 120,000
Kujaza harddisk: 30000
leseni 40000.
extension 2: og 30000
chaja za pin ndogo,smartphon na tecno angalau tatu tatu.
Total: 917,500
Epuka usharobaroo,
Epuka mademu wengi.
Epuka Disko
Epuka ushabiki wa mpira
Epuka Kupenda HipHop
Epuka Kupenda Singei Singeli
Epuka Unafiki
Epuka Bangi
Epuka Pombe
Epuka Mkopo.
Usiuze shamba.
Usiuze nyumba aliojenga baba au iliyokwenye kiwanja cha baba.
Epuka dharau
Uwe mwenye Tabia nzuri.
Fanya utafiti eneo ulilopo...
Uwe mbunifu kama sio wacha kabisa biashara haifanywi kwa mazoea.
Usitake uwe kama fulani
Kua wewe kama Wewe.


Ukiona Ushauri na mawazo haya yatakusaidia ninunulie mandazi mbili.

mimi nami ni msaka mtaji mawazo ninayo mengi pesa ndio tatizo
unaweza nigaia 500 tu itanisaidia pakubwa.
 
Mtafute mkulima alieko kijijini, jiridhishe awe muaminifu.

Fanya partnership na huyu mkulima. Andikishana nae mkataba. Mjengee mkulima huyu uwezo wa kufuga, mf Mbuzi.

Chukua Tshs 150,000 jenga banda la mbuzi lenye uwezo wa kubeba Mbuzi 60+ katika shamba la mkulima wako ili malisho iwe rahisi. Nimeassume wewe upo mjini, km upo shamba fanya mwenyewe kwa kununua hata eka 2!

Kama shamba ni lako mwenyewe, otesha mazao ambayo baada ya mavuno, mabaki ni chakula cha mbuzi. Kuna baadhi ya majani ni chakula cha mbuzi na pia ni dawa kwa maana ya kinga dhidi ya magonjwa. Sikumbuki jina.

Chukua Tshs 600,000 ingiza Mbuzi wa kuanzia. Usinunue mbuzi mnadani. Nunua Mbuzi kutoka kwa wafugaji, pita banda kwa banda kijijini kununua mbuzi hao.

Mbuzi hao wasiwe ndama, wasiwe wazee. Chukua Mbuzi rika la kati, ie 4 months old. Naskia kuna mbuzi wa kisasa wanatoa maziwa mengi, ukipata hao safi sana, lkn hata hawa wa asili wazuri.

Kwa bei za kijijini, utapata mbuzi 20 kwa bei ya Tshs 30,000 kwa mmoja na hao ni wale wakubwa wa kuliwa, ukitaka wale wadogo kiasi, unaweza pata chini ya hiyo Bei.

Chukua dume mmoja tu na majike 19. Weka standby fund kama Tshs 100, 000 kama emergency ikitokea dharura kama ugonjwa. Japo ni mara chache sana.

Baada ya Miezi 4-6 mbuzi wako si chini ya 10 watakuwa wamezaa. Tufanye mbuzi 10 wamezaa, na Hapa tunazungumzia mapacha kwa kila uzao. Hii inamaanisha utakuwa na mbuzi ndama 20. Weka malengo ya kuhakikisha ndama 15 watakuwa mpk kuzaa. Ni nadra sana mbuzi kushambuliwa na maradhi.

Chukua mbuzi 15 + Mbuzi 20 wa mtaji = Mbuzi 35 ndani ya miezi 6 ya kwanza.

Hesabu ikibaki hivo hivo, ndani ya mwaka hukosi mbuzi. 70+ kumbuka mbuzi anazaa mara2 kwa mwaka. Na pia mbuzi hukomaa miezi 6 tu, cha ajabu ni kuwa mbuzi anaweza kubeba mimba na akakua nayo.

Baada ya miaka mi3 weee tajiri wa Mbuzi. Kuhusu soko, usiwaze. Ukishindwa peleka Vingunguti ama CHAMAKWEZA.

NB:
Kumbuka kufanya ibada na kumtanguliza Mungu mbele.
Hiyo nzuri sana mi ndo naifanya ila eneo andaa walau la Hekari 5
 
Kwa hiyo hela unaweza fanya biashara hata zaidi ya moja!!!

Ngoja wataalamu waje
 
Natumai mu wazima wapendwa, lengo la Uzi huu ni kuomba ushauri wa nini cha kufanya na kikalipa vizuri kwa mtaji wa shilingi milioni mbili, naomba tushauriane vizuri na kwa faida ya wengi, pia naomba ushauri kati ya mambo haya:-
#Je, ni bora kununua kiwanja kabla ya kuwekeza kwenye vimiradi vidogovidogo,

NB: kiwango cha hela nilichoweka kinaweza kikawa zaidi au chini ya hapo, tushauriane wapendwa.
 
Umeanza vizur Ila unatupima mwshoni,,,Ila ntachangia baadae kdgo mada hii maana nimeshashauri wengi Ila kwa sasa ngoja nilewe kdgo kuondoa stress za majina ya leo
 
Milioni mbili unaweza kufungua duka, unaweza kufanya biashara ya samaki au dagaa kutoka wanapovuliwa na kuwaleta masokoni, kufunga kuku wa kisasa na wa kienyeji, kufungua grocery, m-pesa/tigopesa, kulima Nyanya /matikiti maji nk.

Kuhusu kiwanja kabla ya mradi jibu ni ndio, kiwanja kinalipa baada ya miaka kadhaa iwe kwa kuamua kuishi hapo au kuuza na usisahau biashara 6 kati ya kumi zinazoanzishwa hufa na mbili kati ya hizo nne zilizobaki hudumaa yaani unapata pango hela ya kula na mavazi tu biashara miaka kibao iko level hiyo hiyo
 
Natumai mu wazima wapendwa, lengo la Uzi huu ni kuomba ushauri wa nini cha kufanya na kikalipa vizuri kwa mtaji wa shilingi milioni mbili, naomba tushauriane vizuri na kwa faida ya wengi, pia naomba ushauri kati ya mambo haya:-
#Je, ni bora kununua kiwanja kabla ya kuwekeza kwenye vimiradi vidogovidogo,

NB: kiwango cha hela nilichoweka kinaweza kikawa zaidi au chini ya hapo, tushauriane wapendwa.
Mkuu inategemea kama kuna biashara ambayo ipo waziwazi kbs na umefanya tathmini kujua kuwa ukiifanya at least utapata faida ya laki 2 au zaidi kwa mwezi.

Kama tayari una banda hiyo hela inaweza kutosha kuweka kuku wa nuama na kukupa faida ya laki 2 mpaka 3

Ila kama huna idea ya biashara yoyote hivi sasa ni bora ununue kiwanja utajenga taratibu au utakuja kukiuza kwa faida kwasababu ukiacha hicho kiwanja mwakani utakikuta kinauzwa Mil 6.
 
Back
Top Bottom