Mtaani Serikali ya Rais Samia inapoteza uungwaji mkono kwa kasi ya kutisha

Tatizo wananchi wanataka Rais Samia aendeshe nchi kama Magufuli alivyokwa . Hapa tunasahau kuwa hawa ni binadamu wawili wenye uzoefu , utashi na maono tofauti. Ingawa wanaongozwa na ilani ya CCM. Vilevile serikali ya awamu ya sita imejaribu siasa za uwazi na ukweli. WaTz wengine hawapo tayari kwa siasa hizi- wanataka kusikia mambo mazuri tu masikioni mwao. Awamu ya sita imesema imesikia vilio vya wananchi na wanafanyia kazi malalamiko -tuvute subira. Kuongoza nchi ni kazi ngumu - tumpatie Rais Samia muda zaidi kama yeye mwenyewe alivyoomba ili aweke safu nzuri ya kuendeleza Tz. Mambo kama katiba yatafuata tu! Waswahili wanasema ahadi ni deni.
 
Watu wanamuona anavyovunja katiba na kuminya haki za kikatiba za makundi mengine ya kisiasa kama vile vyama vya siasa, wamemuondolea zile credits za kudhani ni muungwana
 
Pro-Chadema bana naona mnalia lia na kuwasemea watamzania, Rais asipoungwa mkono si ndiyo faida kwa Chadema au mnatakaje?
 
Ukiwa kiongozi Bora ufanye unachoamini inafaa kwa unaowaongoza bila kuvunja taratibu
 
Mkuu nina swali hapo
Kwa nini serikali ya mama iliweka hizi tozo? Ok tuseme hakujua Kama watu watalalamika, sasa inakuwaje wanasema hawawezi kuziondoa(rejea kauli ya Msigwa Jana)
Tukubali tu huyu mama uraisi hauwezi
 
Toka huyu Mama aingie Madarakani haijawahi kupita siku Umeme haujakatika.. Maji nayo yamekuwa ya shida shida tu.
 
Unakuaje rais na unashikiwa masikio? Ndio maana nikasema hakua tayari kuwa kwenye nafasi hiyo. Magufuli aliitumia ipasavyo hiyo nafasi japo hakua na maono. Laiti angekua na maono, angetufikisha mbali sana. Hakuyumbushwa kwa kile alichokiamini yeye

Mambo hua hayopa mepesi kihivo mkuu, Asilimia kubwa ya maraisi wa mpito huwa wanakosa nguvu ya kisiasa, si yeye hata sehemu nyingi Duniani. Ameingia kwenye system katikati bila ya kuwa na support ya kutosha kwenye system, so ni rahisi kupelekeshwa na watu ambao walikua na influence kwenye system kwa mda ule.
 
Mitaa ipi??Huku nnapokaa watu hawajadili siasa kabisa..hawana hata time na mijadala..

Ukiingia JF ndo unakuta malalamiko tele..

Huku mitaani no body cares that much
Wewe ni mpumbavu
Usilalamike na wala kuita mods waje kumpiga mtu pin haisaidii kwa sababu....

You deserve it,huwezi kusimama hapa kuwasemea watu huyu aloanzisha uzi hapa hakai mbinguni yupo mtaani wanao-comment JF wapo mtaani hawakai mbinguni wewe ulitaka wale wenye malalamiko waje kwako wakugongee mlango wakueleze ndo uamini?wewe ilibidi huu uzi uufungue hukuelewa kinachozungumzwa u-click home button urudi utafute kingine cha kusoma siyo kuandika vitu vya ajabu ajabu.
 
Mitaa ipi??Huku nnapokaa watu hawajadili siasa kabisa..hawana hata time na mijadala..

Ukiingia JF ndo unakuta malalamiko tele..

Huku mitaani no body cares that much
Mie huku Kilimanjaro hakuna mijadala inayozungumzwa humu. Wananchi wanajadili masuala ya maendeleo.
 
Mkuu siyo kwamba unademka tu au?
 
Naunga mkono hoja, kweli kabisa huku mtaani kadili siku zinavyozidi kusonga, Raisi samia huugwaji wake unapungua kwa kasi sana.

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Alianza vizuri mno nikasema km ni kiongozi tumepata. Ila sasa hivi kapotea yani sitaki hata kusikia jina lake.
1. Tozo ya miamala(big failure)
2. Mbowe stuff
3. Vaccine issue/contraversial
4. Bei ya mafuta kupaa
5. Kulipa kodi ya ardhi via LUKU
6. Kuacha mawaziri na watendaji wa juu kujibu watu ovyo. Ref Mwigulu anaambia waTZ wahamie Burundi.
7. Kuwaaacha kina Mdee na covid19 wenzie bungeni

Sitegemei maajabu yoyote amalize tu muda wake akapumzike kwao.
 
Katiba mpya hataki hata kusikia wakati alikua kiongozi wa kamati ya katiba mpya. Mchumia tumbo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…