Mtaandika vitabu na vitabu, ila hamtaweza kubadili chochote juu ya Hayati Magufuli

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Nimeamini! Mtandao wa mafisadi nchini, mwenye kuuvinja sio mfano wa Magufuli tena, anapaswa awe ni mtu katili kuliko Hitila, mwenye sura mbaya kuliko Idd amini dadaa

Kila Mtanzania kwa sasa, hahitaji kuuliza kwa mwenzake kuhusu ufisadi ulivyokithili sasa, watu wako bize kuiba kiasi hata Mh Rais akijisahau haya majizi yanaweza kuondoka na pochi yake

Ni Magufuli pekee aliyeipandisha hadhi nchi yetu, ni yeye pekee aliyeibua miradi kedekede na isiyohesabika, miradi ya kimkakati na kuileta nchi katika uchumi wa kati mdogo! Hivi utamdanganya nani?

Ni Magufuli pekee aliyekuwa na huruma ya dhati kwa wananchi wote hasa wa chini, aliwajali na kutatua kero zao bila kuogopa wenye ukali

Ni serikali yake tu, iliyotaka kuondoa tabaka la walionacho na wasiokuwa nacho, watu hawa wanatuona kana kwamba wote tulikuwa chekechea siyo?

Halafu wasomi uchwala hao waliondika daftari Lao hilo, wote wako nje ya nchi na hawataki kurudi,

Hata hivyo, kwa nini wanatumia nguvu nyingi kiasi hiko? Nini kipo nyuma yao? Na ukichunguza zaidi, unagundua tu kwamba, miongoni mwa walioshiriki ni pamoja na waliotemwa kwenye nafasi za uteuliwa utawala wa Magufuli na wanafahamika, watu hawa wanaroho mbaya kuliko hata shetani, wako tayari kutoa uhai wa mtu hasa anapogusa maslahi yao!

Ninauhakika, Waovu hawawezi kutawala Milele hata kama katikati yao kuna mmoja tu mtenda haki, Sharti mtenda haki huyo, kwa nguvu isiyoshindwa, atapenya katikati yao, Hilo ninahakika nalo! Mungu hawezi kuruhusu upuuzi huu ukatawala, kwamba keki ya Taifa iishie kwa wachache na wengine kuishia kuwa na maisha ombaomba na ya kutangatanga katika nchi yao njema yenye kila aina ya vinono?

Tunarudia tena, hayati Magufuli, ni mtu ambaye, mafisadi mtatumia nguvu na shekeli zenu nyingi mno, lakini nasikitika kusema kwamba, mnapata hasara bule, hamtamchafua kamwe, utawala wake uliwagusa watu ambao nyinyi ni mabwege kwenu, watu dhaifu na ambao kwenu nyinyi hamkuwahi kuwahesabu kama ni watanzania na wenye kuistahili heshima na haki kama raia wa nchi hii njema

Hata hivyo, mbona bado ni walewale vilaza na mafisadi?

Watu ambao wamejikusanya kuandika kitabu cha kumchafua Magufuli, ndio hao waliokuwa wakitafutwa wakihusishwa na wizi wa mali za watanzania wengi wao wakakimbilia nje ya nchi

Wasomi uchwala hao, wameandika kitabu kinachohusu serikali ya Magufuli ilivyowekeza katika mji wa Chato ambapo ni sehemu ya Tanzania.

Mantiki yao ni ipi haswa!

Hata iweje, waandike vitabu na vitabu, nyinyi wasomi uchewara, tunachukua nafasi hii kuwakumbusha sisi wamachinga, wafanya biashara, wamama ntilie, wananchi wa kawaida, tunawakumbusha tu kwamba, Magufuli hawezi kuchafuliwa na yeyote kwa njia yoyote ile! Na kujaribu kufanya hivyo, ni kuchochea ghadhabu yetu sisi,

Tutaendelea kuguswa na yale ametufanyia kama nchi na wananchi!

Magufuli! Lala salama!

Kuna wajinga wachache wanadhani eti ni rahisi tusahau mema uliyotuachia Magufuli!

Akili za fisadi siku zote huwaza apate wapi pesa hata kwa kutoa roho! MUNGU mwenyeenzi Ibariki Tanzania, wabariki viongozi wema! Amina
 
Kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya ni sababu haswa ya JPM.

Juzi nimepita pale Buzirayombo nikaona jinsi ule mnada wa Kimataifa ulivyobakia kuwa jumba la makazi ya popo.
Hahaa! Wewe na buzirayombo wapi na wapi!

Vipi biashara zako hapo Kariakoo mkuu
 
Ukiona wanatumia nguvu nyingi kuchafua ujue ilikuwa safi. Angekuwa mchafu wala haihitajiki nguvu kubwa kuonesha umma.
Watanzania sio wajinga. Hao wamenikumbusa korean movie-iljimae) mwizi anayeiba kusaidia maskini.

Mengine ni majizi makubwa yanaiba na kupelekea mabeberu! Wamuache apumzike kwa amani
 
Nimeamini! Mtandao wa mafisadi nchini, mwenye kuuvinja sio mfano wa Magufuli tena, anapaswa awe ni mtu katili kuliko Hitila, mwenye sura mbaya kuliko Idd amini dadaa

Kila Mtanzania kwa sasa, hahitaji kuuliza kwa mwenzake kuhusu ufisadi ulivyokithili sasa, watu wako bize kuiba kiasi hata Mh Rais akijisahau haya majizi yanaweza kuondoka na pochi yake

Watu ambao wamejikusanya kuandika kitabu cha kumchafua Magufuli, ndio hao waliokuwa wakitafutwa wakihusishwa na wizi wa mali za watanzania wengi wao wakakimbilia nje ya nchi

Wasomi uchwala hao, wameandika kitabu kinachohusu serikali ya Magufuli ilivyowekeza katika mji wa Chato ambapo ni sehemu ya Tanzania.

Mantiki yao ni ipi haswa!

Hata iweje, aandike vitabu na vitabu, bado Magufuli hawezi kuchafulika kijinga!

Zaidi, soma: From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)
Alikuwa janga la taifa.
 
JPM ata kama wange igiza move ya kumchafua awawezi.
Yule jamaa kuna namna alijua kucheza kwenye cheo chake.
Na ili nch ibadilike anahitajika kiongoz more than JPM kuna kikund cha watu flan iv wakikipiga pin bas nchi ime win haiwezekani
Mbuga,maziwa,mito,madini,viwanja vya ndege,gas n.k lakin bado at shule znakosa vit af znatolewa mil200 kununua gar ya sjui nan nani ambalo gar ilo ni kubeba wadada na wake zawatu kupeleka kwenye lodge non sens.
 
Magufuli atabaki kuwa rais aliyeigawa nchi yetu kwa misingi ya kikabila na mtu aliyevuruga mshikamano wetu. Atakumbukwa kwa visasi, kufanya maamuzi bila kushirikisha bunge, upendeleo wa kikabila na kindugu, uteswaji na hata kwa vifo vya wapinzani wake kisiasa. Alivuruga uhusiano wetu na nchi jirani na hata nchi za Ulaya. Ameacha doa kubwa katika historia ya Tanzania.
 
JPM ata kama wange igiza move ya kumchafua awawezi.
Yule jamaa kuna namna alijua kucheza kwenye cheo chake.
Na ili nch ibadilike anahitajika kiongoz more than JPM kuna kikund cha watu flan iv wakikipiga pin bas nchi ime win haiwezekani
Mbuga,maziwa,mito,madini,viwanja vya ndege,gas n.k lakin bado at shule znakosa vit af znatolewa mil200 kununua gar ya sjui nan nani ambalo gar ilo ni kubeba wadada na wake zawatu kupeleka kwenye lodge non sens.

Hivyo vyote unavyotaja sijui mito, maziwa nk viko hata enzi za Nyerere, na Nyerere hakuwa mwizi, mbona bado tulivaa hadi viraka?
 
Nimeamini! Mtandao wa mafisadi nchini, mwenye kuuvinja sio mfano wa Magufuli tena, anapaswa awe ni mtu katili kuliko Hitila, mwenye sura mbaya kuliko Idd amini dadaa

Kila Mtanzania kwa sasa, hahitaji kuuliza kwa mwenzake kuhusu ufisadi ulivyokithili sasa, watu wako bize kuiba kiasi hata Mh Rais akijisahau haya majizi yanaweza kuondoka na pochi yake

Watu ambao wamejikusanya kuandika kitabu cha kumchafua Magufuli, ndio hao waliokuwa wakitafutwa wakihusishwa na wizi wa mali za watanzania wengi wao wakakimbilia nje ya nchi

Wasomi uchwala hao, wameandika kitabu kinachohusu serikali ya Magufuli ilivyowekeza katika mji wa Chato ambapo ni sehemu ya Tanzania.

Mantiki yao ni ipi haswa!

Hata iweje, aandike vitabu na vitabu, bado Magufuli hawezi kuchafulika kijinga!

Zaidi, soma: From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)
Kwan kumetokea nn tena?
 
Mti wenye matunda hupondwa mawe.
 
Na mtampamba sana Magufuli wenu lkn kamwe hamtobadili kitu ktk uovu wake.
Atabakia kuwa mtu hatari sana aliyejaribu kuligawa taifa lkn Mungu mwema aliingilia kutunusuru waja wake
 
Back
Top Bottom