Mtaa wa kwa Kindande Temeke visa vyake

We mtoto wa Kota nyamaza!!

Unajiita Da Hustla halafu unaogopa watu wenye nyembe mfukoni!!! Watu hadi kesho wanatembea na full-loaded gun, na ukimzingua anaku-shoot, unakuja kuogopa kisu halafu bado unajiita Da Hustla!!!
We unafikiri kuwa Hustla ni kuwa msela mavi au ku-hustle ki old school hivo na mambo ya bisi bisi,wembe na mapanga...watu wana hustle kwa kutumia brains sio kwa kutumia hayo mataka taka,na ndo tofauti kati ya watoto wa mjini kinondoni(sio ile ya uswazi) na huko swekeni sijui tandika ,temeke,tandale ,mwananyamala etc
 
Umeelewa lakini context ya kutofautisha kati ya Dar es salaam na Mzizima katika kumjibu huyo aliyesema haipendi Dar ?

Sio unaleta story za mwananyamala sijui tandika...yes hizo ni story zinayovutia watu wake na kuna watu haziwavutii na hawana habari nazo hapa hapa Dsm

Off course,Temeke yenu ni yenu na we don't give a damn about it
Wa kuja wewe!!!
 
We unafikiri kuwa Hustla ni kuwa msela mavi au ku-hustle ki old school hivo na mambo ya bisi bisi,wembe na mapanga...watu wana hustle kwa kutumia brains sio kwa kutumia hayo mataka taka,na ndo tofauti kati ya watoto wa mjini kinondoni(sio ile ya uswazi) na huko swekeni sijui tandika ,temeke,tandale ,mwananyamala etc
Utakuwa wa kuja wewe, Dar ukafikia kota!!!

Huwezi kuwa husler halafu ukaogopa life la mtaa la kwa sababu hata ukitumia brain, kwenye hustling utazinguana tu na watu!!

Au mtoto wa kishua hujui nini maana ya hustle?!!
 
Wewe ndo wala huijui Dar es salaam!!! Kama unadhani Mikocheni, Masaki, Mbezi, Oysterbay and the like ndio Dar es salaama basi huijui Dar es salaam!!!

Huwezi kuitenganisha Dar es salaam na Uswahilini Max au Uswahilini Pro ambako nakuita Ushenzini!!!

Huko Ushenzini ndo unapata flavor halisi ya Dar, na sio kule ambako videmu na vivulana vinaongea Kiswahili kwa lafudhi ya kizungu wakati hata Nairobi hawajawahi kufika... fvck them all!!

Huwezi kusema upo Dar es salaam au umewahi kufika Dar es salaam wakati huijui Dar es salaam Asili!

Hujawahi kuuona wala kuusikia mdundiko, vigodoro unapata kuvisikia tu Instagram, hujawahi ona mwanamama mtu mzima anaendewa na vigoma kwake kusutwa mbele ya familia yake kwamba aache umbeya; halafu unasema unaijua Dar es salaam?!

Enzi hizo, mdunduko unaanzia Temeke Mikoroshini hadi Mwananyamala kwa Waswahili wenzetu and all the way to Mwananyamala watu wanaunga tela njiani...!!

Na kama kuna ndugu wengine say pande za Msasani huko (sio Msasani ya Kishua) basi mdundiko hautaishia Mwanyamala!!

Hiyo ndo Dar es salaam, na mambo mengine yoooote ni fake!! Huwezi kuitenganisha Dar es salaam na Uswahili au na uhuni wa Kiswazi!!

I miss Temeke, ndo vile tu ili kupambana na maisha wanaume tunatakiwa kuwa mbali na familia na ndugu!!!

Nimeona hapo juu Jason Statham2 akisema "hiyo ndo TMK yetu, mtuache", nami nakazia, tuachieni Temeke yetu!!
Kama ndo hivo mbona Dar kwa kipuuzi sasa kama izo fleva zenye?
 
Kama ndo hivo mbona Dar kwa kipuuzi sasa kama izo fleva zenye?
Sasa ukienda Arusha halafu ukakutana na Mdundiko huwezi kujiuliza mdundiko na Arusha wapi na wapi?!

Miaka kadhaa iliyopita nilitembelewa na mshikaji wangu mmoja... foreigner!

Nilivyokuwa boya wakati ule, eti siku ya kwanza kumtembeza nikampeleka city kumuonesha "tulivyo na bonge la jiji" wakati anakotoka, hizi flyovers zinazoshabikiwa leo Dar kule kwao zilijengwa hata kabla hajazaliwa!!!

Tena nakumbuka tumefika pande za Gymkhana jamaa akaonesha wazi kwamba ameboreka na ile tour, na akaja ku-enjoy siku ya pili yake tulivyoenda Mafia!!!

Nilijiona boya ile mbaya!!

So, YES, hizo ndo flavor za Dar labda siku nitembelewe na Msukuma ndipo nitampeleka akaangalie flavor za Kisukuma Sukuma kama vile Mabugando n.k :D🤣😅!!

Wasukuma msini-mind, nawatania tu!!
 
Mwaka 88 baada ya kupata kazi idara moja ya serikali nilipata chumba maeneo ya Manzese Midizini, wezi wote wa kwenye mitumba walikua wanakaa midizini. Nilikua nikirudi saa kumi sitoki ndani mpaka kesho yake kwa kuogopa vibaka. Siku moja kaja dogo mmoja kuniambia, shoferi usipende kukaa ndani kama dem. Njoo nikuyembeze. Basi nikatoka nae break ya kwanza kwenye banda la gongo. Enzi zile kituo cha polisi cha karibu ni urafiki. Basi nikaagiza kijeti kilipoisha nikaagiza cha pili. Wahuni walikunywa mpaka wakasema shoferi basi. Kuanzia hapo niliyembea Manzese yote mida yoyote bila kuulizwa na mtu. Ila wakikuomba kistaarabu kifanta au fegi wape tu. Nikaja kugundua kwamba kumbe hakuna mhuni ambae hana utu.
Mwanzoni miaka ya 2000 nliiingia dar kwa Mara ya kwanza, mzee aliniacha kijijini kuja kufight maisha jijini alipokaa sawa kidogo mwamba nikapata nafasi ya kuingia town!

Vingunguti kwa mnyamani ndio mzee alikaa miaka hiyo.

Ile napanda dala dala pale kiembe mbuzi niingie tuition chaaap wahuni wamepita na wallet nafika karume Sina hata mia na simu Sina. Taabu niliyopata siku hiyo acha na vile nilikua ndio nimeingia mjini ilikua balaaa.

Nilifanikiwa kurudi jioni Nikamwambia mzee, akaniambia changamka wewe mjini hapa, akanichukua tukaenda vichochoro kwa vichochoro aisee, yaani matusi matusi tu, uhuni uhuni, bangi bangi, gongo gongo, umalaya umalaya, mchanganyiko wa hatari, mzee ananiambia mwanaume lazima ujue kuishi mazingira yote,

Hatumaye tukafika kwa hao mateja, nashangaa wanamuamkia mzee kwa heshima kabisa Ila wamechoka kinyama. Baada ya salamu mzee akawaambia nimekuja kumtambulisha mdogo wenu, wahuni walifurahi kinyama, wananipa ushauri niwe makini kitaa nisije kuwa Kama wao na vitu vingine positive, nikaanza kubadili mtazamo wangu juu yao, nikaona kumbe wale ni wagonjwa Kama wagonjwa wengine, ni wahanga tu wa maswaibu ya dunia.

Akawaambia mmepiga asubuhi kawallet na kasimu kake wakaomba msamaha pale, Ila walishauza muda huo. Mzee akawapa buku tukasepa.

Leo ni mwaka wa kumi na nane Niko town sijawahi pata shida na vijana wenzangu nilijifunza jinsi ya kuishi nao.

MEISHO.
WAO NI WAHANGA WA MASWAIBU YA DUNIA TUJIFUNZE KUISHI NAO NA TUKIWEZA TUWASAIDIE.
 
Mwaka 88 baada ya kupata kazi idara moja ya serikali nilipata chumba maeneo ya Manzese Midizini, wezi wote wa kwenye mitumba walikua wanakaa midizini. Nilikua nikirudi saa kumi sitoki ndani mpaka kesho yake kwa kuogopa vibaka. Siku moja kaja dogo mmoja kuniambia, shoferi usipende kukaa ndani kama dem. Njoo nikuyembeze. Basi nikatoka nae break ya kwanza kwenye banda la gongo. Enzi zile kituo cha polisi cha karibu ni urafiki. Basi nikaagiza kijeti kilipoisha nikaagiza cha pili. Wahuni walikunywa mpaka wakasema shoferi basi. Kuanzia hapo niliyembea Manzese yote mida yoyote bila kuulizwa na mtu. Ila wakikuomba kistaarabu kifanta au fegi wape tu. Nikaja kugundua kwamba kumbe hakuna mhuni ambae hana utu.
Wahuni wana utu sana ukienda nao sawa, halafu huwa wanahitaji vitu vidogo vidogo sana, ukiwaelewa tu unaishi kibosi sana hata ulinzi wanakupatia. ukijifanya huwajui hiyo mitaa utapata taabu sana
 
Ukifika Temeke kuna mtaa unaitwa Mji mpya ndani yake kuna kamtaa korofi kanaitwa KINDANDE.

Kindande kuna maskani maarufu inaitwa Lebanon.

Huu mtaa kwa kindande ni mtaa ambao unaogopeka kupita bila taadhari kwa saa 24..Mambo yote maovu yapo hapo kuanzia wizi kukaba mchana umalaya uvutaji bangi ulio kubuhu.

Katika maisha yangu yote sijawai kuona wanawake wanavuta bangi kupita wanaume ni mewaona kwa Kindande.

Mabinti wa kwa Kindande wanatabia ya kukaa nje wakikuomba hela ukakataa kutoa hayo matusi yake ni balaaha.

Mabinti wa kwa Kindande wanaongoza kucheza vigodoro wakiwa uchi sometimes wanakodishwa kwenda kusasambua kwenye vigodoro vya majirani zao Mtongani,Tandika,Wailes, na Mbagala.

Hawa mabinti wana tabia ya kukodi boda boda usiku mishale ya saa 7 usiku na kuendelea wana tegesha sehemu za starehe ukijiroga ukampakia mkifika tu kwa Kindande kuna makaburi mitaa hiyo litakuja kundi litakupiga piki piki inaondoka.

Kwa Kindande ukimpenda demu ukichepuka kazi unayo utapigwa na kundi lake plus matusi juu hila yeye kuchepuka ruksa.

Wana maskani yao inaitwa Lebanon hiyo na polisi ni kufukuzana kila siku hapo unawapata madogo wa miaka 12 waliopinda wapiga bangi hatari.

Huku unakuta dogo naye ni baba vibinti vidogo navyo ni single mother.

Huu mtaa unaongoza kwa matusi kwa lika zote hakuna heshima kwa mkubwa wala mdogo.

Hiki kimtaa kimepakana na Tandika Kwa Aziz Ally Temeke mwisho na Mtoni mtongani.

Kama sio mtu wa vulugu usipange mtaa huu...
Duh
 
So wazawa wote wapo uswahilini?
Hakuna mzawa anayekaa ushuani anayeweza kushangaa au kuponda Uswahili wa Dar es salaam kwa sababu bado atakuwa na ndugu wa kutosha huku Uswahilini, na maisha ya Kiswahili yataendelea kuwa sehemu ya maisha yake!!!
 
Basi sawa
 
Ukifika Temeke kuna mtaa unaitwa Mji mpya ndani yake kuna kamtaa korofi kanaitwa KINDANDE.

Kindande kuna maskani maarufu inaitwa Lebanon.

Huu mtaa kwa kindande ni mtaa ambao unaogopeka kupita bila taadhari kwa saa 24..Mambo yote maovu yapo hapo kuanzia wizi kukaba mchana umalaya uvutaji bangi ulio kubuhu.

Katika maisha yangu yote sijawai kuona wanawake wanavuta bangi kupita wanaume ni mewaona kwa Kindande.

Mabinti wa kwa Kindande wanatabia ya kukaa nje wakikuomba hela ukakataa kutoa hayo matusi yake ni balaaha.

Mabinti wa kwa Kindande wanaongoza kucheza vigodoro wakiwa uchi sometimes wanakodishwa kwenda kusasambua kwenye vigodoro vya majirani zao Mtongani,Tandika,Wailes, na Mbagala.

Hawa mabinti wana tabia ya kukodi boda boda usiku mishale ya saa 7 usiku na kuendelea wana tegesha sehemu za starehe ukijiroga ukampakia mkifika tu kwa Kindande kuna makaburi mitaa hiyo litakuja kundi litakupiga piki piki inaondoka.

Kwa Kindande ukimpenda demu ukichepuka kazi unayo utapigwa na kundi lake plus matusi juu hila yeye kuchepuka ruksa.

Wana maskani yao inaitwa Lebanon hiyo na polisi ni kufukuzana kila siku hapo unawapata madogo wa miaka 12 waliopinda wapiga bangi hatari.

Huku unakuta dogo naye ni baba vibinti vidogo navyo ni single mother.

Huu mtaa unaongoza kwa matusi kwa lika zote hakuna heshima kwa mkubwa wala mdogo.

Hiki kimtaa kimepakana na Tandika Kwa Aziz Ally Temeke mwisho na Mtoni mtongani.

Kama sio mtu wa vulugu usipange mtaa huu...
mdogo wangu pole sana ila shukuru mungu tu sasa hivi huko ndio kumepoa sna, way back mitaa ya huko ulikuwa huoni hata kuku kufugwa, familis nyingi zilihalibika , watoto walikuwa wezi hatari danger zone za way back " stombagi" plus na talban camp hapo mbele ya makaburi kuelekea raha leo, " teqwin" " kwa mayawa a k.a santamigo" kwa keni" damu ya simba , from 2003 kurudi nyuma aisee ilikuwa mbaya kupitiliza coz sisi tumeishi hyo mitaa
 
Uswahilin kuna vituko sana picha linaanza tu kwanza demu anakuja kukutongoza mwenyewe alafu kibabe huku anakuchamba kinyama ukimkataa visa vyake utahama mtaa
 
Back
Top Bottom