Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,520
- 2,091
Jambo wana JF... baada ya kumaliza karibu majina yote ya watu mashuhuri kwa Mitaa na Barabara hapa BONGO nawaomba tufunguke kuhusu Mtaa/Barabara tumpatie ******? Ndg.B.Mkapa tume-reserve Morogoro road... Hivyo tusahau hiyo...
Mimi napendekeza Barabara ya ipitayo Tandale Uzuri...kutokea Sinza Kijiweni hadi Magomeni kanisani... sifa ya kwanza ni ndefu na ni pekee ambayo haina jina rasmi...toa maoni yako bila jazba...
Haya SHIME SHIME Mbunge wetu wa Ubungo twaomba utoe Pendekezo hilo kwa Baraza la Madiwani wa wilaya ya Kinondoni walipe kipaumbele jambo hilo Murua...
Moja ya vitega uchumi muhimu vilivyopo kwenye barabara hiyo ni Hotel ya Den France-Sinza,Mtanzania-Manzese Uzuri,Vatican City,Deluxe Hotel,Lion Hotel-Sinza na Hotel le Grande Migomigo...
Vingine ni WALE WAJASIRIAMALI WA Mtogole,Perfume safi ya mfereji wa Tandale kwa Tumbo...na kile kituo cha Magari yaendayo kasi pale barabara ile inapokutana na ile ya Kawawa
Sijakupata mkuu. Unasema "Ndg Ben Mkapa TUME-RESERVE Morogoro road" Ni wewe na nani mwingine mliokaa na KURESERVE Morogoro rd? Nielimishe juu ya hili kabla sijaendelea na kuchangia kuhusu hii mada.