Ukiambiwa uthibitishe kuwa mwili ulikuwa na matundu ya....utakubali!!? Au wewe ndiye ulihusika kwenye Postmortem. Halafu Je mlikuwa wapi kumuuliza Julius maana ndiye alikuwa Mkulu kabisa. Je ni nani alikuwa IGP, Intelligence chief , Home Affair minister nk.
Nasema mna imani za kichawi kwa kuwa kati ya hoja zenu eti kwavile alikuwa anapata mauzauza.!!! Sasa hii inahusika vip.!!!? NDIO MAANA NASEMA TOKENI HUKO kwenye fikra za ajabu ajabu.
Otherwise mpo hapa KISIASA ZAIDI. but be very careful unapoamua kumchafua mtu huwa inarudi na wewe ipo siku utahusishwa na kifo cha mtu hata kama hujahusika. ACHENI SIASA MAJI TAKA
Unataka kutuambia ni sahihi kwa Msuya kwa vile alivyoitwa "kidole cha damu"?
Kwanini sasa "nduguzetu" walimbeba Prof Shaba kutoka New Africa Hotel kumrudisha kwake chapchap baada ya kunywa whisky na kuanza kusema "Sokoine hakufa kifo...alikuwa na matundu ya..."
Searching....
hallucinations ni uchawi? Mambo mengine yanahitaji jitihada binafsi kuelewa siy lazima yawe kwenye syllabus ya shule bwana.
Naomba usiweweseke. Ukitulia inaleta sense kuliko unavyotaka ku punic. Kwani wewe unajihami nini? Vifo vingapi vya watu duniani vinachunguzwagwa baada ya miaka mingi kupita? Tunapoulizana yahusuyo kifo cha sokoine wewe hutaki yaongelewe, kwa sababu gani?
Sasa nani anachafuliwa hapa na nani anamchafua? Nimekuambia nani alimuua sokoine ama umenisikia nimesema alikufa kifo cha namna gani?
Acha watu wajadiliane. Hakuna ubaya katika hilo. Lakini ukweli utasemwa siku zote kwamba sokoine hakupimwa morogoro hospital kujua kama alifika pale ameshakufa ama alikuwa hai!.
Hili ninalijua. Maswali mengine bwana. Unataka nisemeje? Wenye ufahamu wameshaelewa. Unajuaje kama sikuwepo morogoro wakati dr. Materu anaambiwa hana sababu ya kupima?
Jifunze kuwa msikivu kuliko kubisha masual usiyoyajua!.
Mkuu asante kwa kunijibia hata mimi nilitaka kumuuliza hayo uliyomuuliza Sokoinekafa miaka kibao leo hii baada ya Mzee wa watu kumsema baba Fred jamaa ndio anamkumbuka Moringe,tena akamsaidie huyo Fred kunywa viroba.
Swali km lako,Lowassa hajaanza kutoa Hela leo,Je!leo mwaka wa uchaguzi ndio C.Msuya anauona huo uovu wa Lowassa?
Simtetei Msuya katika uzi huu, lakini inabidi Lowassa atuonyeshe kiwanda chake cha manoti ili tukachukue huko huko, tumechoka kupewa na yeye.yap...hii mihela kaanza kuitoa mida tu sasa jamaa kaona huu mwaka ndio wa kusemea....
Ndugu zake Sokoine kina nani waliombeba Prof Shaba kutoka New Arusha Hotel?
Mimi ninajua Sokoine hakuwa na ndugu wa kwenda kustarehe New Africa Hotel. Wote walikuwa pale msibani including watoto wake, Joseph and Lazaro, na ukoo wote. Hadi yule ngombe mwusi anachinjwa, wanapaka mafuta yake mwili yake, hatukuwa na ndugu yake anakaa New Africa anaitwa Profesa Shaba 1984.
Nilikaa pale Munduli juu Mwezi mzima baada ya mazishi kabla sijaenda Munduli jeshini.
Naomba kama kuna point sijakupata nielewshe.
Oktoba usije haraka tuone mambo!
Tunapokaribia kuadhimisha miaka 31 tangu kilipotokea kifo kilichojaa utata cha aliyekuwa Waziri Mkuu Ndg.Edward Moringe Sokoine,ni wakati mwafaka sasa kumhoji Mh.Cleopa Msuya juu ya tuhuma za kuhusishwa na kifo cha Mh. Sokoine;kwa sababu Mh. Msuya kwa siku za karibuni amejitokeza kukemea maovu mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa CCM bila shaka pia atakuwa na ujasiri wa kujitokeza na kutolea ufafanuzi wa tuhuma hizi.
Du kama hivo ndivyo ilivyokuwa basi iko kazi....Uanjua watu wanasemaga vitu bila kujua kuna siku vitakuja kuleta maswali.
Kama kuna mtu anasema Sokoine alikuwa akiwa njiani kuelekea Morogoro, nani alithibitisha kifo cha Sokoine? Kulikuwa na Daktari kwenye ile gari aliyempima na kujua alifia njiani wakienda Morogoro?
Nini ilikuwa sababu ya kumpitisha Morogoro Regional Hospital Ikiwa walikuwa wanajua alifilia njiani hata kabla hajafika Morogoro?
Ni vizuri wakanyoosha maelezo.
Ninachokifahamu mimi, waliompeleka Hospital ya Morogoro walikataa asipimwe kwamba alishakufa. Ni jambo dogo lakini ni vizuri kuliangalia kwa upana. Pale Morogoro hakuna Daktari alimpima Sokoine kuthibitisha amekufa ama la. Dr. Materu, aliyekuwa zamu pale, aliye wapokea hakuruhusiwa ampime.
Kama ni report iliandikwa ilikuwa ni kwa formalities na kutokana na maelezo waliyokuwa wanayapata.
Ninaogopa kusema zaidi kwa hofu ya kuambiwa naandika uchochezi.
Imetosha.