Gama
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 13,264
- 4,740
Hii sayansi ngumu. ..
Kuna yule dada aliyetolewa kwenye shimo wakisema ni msukule angepatikana angeweza kutusaidia. ..
Otherwise mshana jr na MziziMkavu wanaweza kutusaidia zaidi
Hii sayansi ngumu. ..
Kuna yule dada aliyetolewa kwenye shimo wakisema ni msukule angepatikana angeweza kutusaidia. ..
Otherwise mshana jr na MziziMkavu wanaweza kutusaidia zaidi
we kiboko,kwa maelezo haya nimekuaminiaJE MSUKULE NI NINI?
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.
Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.
Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.
Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.
Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.
Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.
Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.
Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.
Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.
Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)
Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia “Mortoo tombo Mivi” maana yake ni kwamba “aliye ndani ya kaburi ni wangu”
Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.
Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.
Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.
Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.
Kwa hiyo Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.
Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo DRC na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia.
Na hapaTanzania WAPO kAA CHONJO...
Ukiwa na Shida yoyote ile unaweza kunitafuta Kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
Tungempata Gwajima angeweza kutupa somo la kutosha... Hivi hayumo JF?
Majimoto nasikia ipo na ingine ya kupotea tu, mtu anajipeleka mwenyewe kwa mchawiZipo aina nyingi za kuchukua watu misukule, aina iliyozoeleka sana ni mtu kufa kisha mwili wake ukazikwa, aina ya pili ni wachawi kuondoa nafsi ya mtu akiwa hai na kuingiziwa pepo na akaendelea kuishi, aina ya tatu ni wachawi kuchukua nyota ya mtu na kuuziwa mtu mwingine.
Fasta ngoja niende kwa Eve napajua abapoishiUkitaka kumwona msukule live, kutana na team Wema.
Cc: Evelyn Salt
Ha ha haFasta ngoja niende kwa Eve napajua abapoishi
Hasa team leader ndio original kabisaHa ha ha
Hakyanani, ile team ni Misukule inayoishi.
Mkuu nina swali la kukuuliza!Binadamu ana mwili na ndani ya mwili kuna roho, roho ya mtoto, roho ya kijana na roho ya mzee zote ziko sawa, tofauti ipo kwenye mwili uliovalishwa hiyo roho. Kwa taarifa yako watoto ndio wanaotumiwa sana kwenye ulozi kuliko vijana na wazee.
aisee!! kwahiyo ndugu wasipolia kabisa huyo ndugu yao anaweza kurudi/kufufuka au?!Wapo watu huwa wanatafuta watu wa kumfanyia kazi zake bila ya malipo, watu kama hao huwaendea wachawi na kumwomba amtafutie vijana wenye nguvu kwa ajili ya kazi za shamba au kwa kazi ya kushusha nyavu za uvuvi wa samaki chini ya maji, au kwa kazi ya kwenda kuiba, au kwa kazi za kwenye viwanda n.k
Mchawi akimwona kijana mwenye sifa hizo huandaa uchawi na kuita jini kwa ajili ya kumzibiti, kwa sababu kifo chochote ni lazima kuwepo na sababu, njia wanazotumia sana ni kutumiwa jini na kijana anaumwa sana kichwa mbele ya paji la uso na baada ya muda kijana anafariki, kabila ya kifo chake wanachukuwa kipande cha mgomba, yule jini aliyetumwa anaingia ndani ya ule mgomba na kuvaa sura ya marehemu kabisa wanafana kwa kila kitu. Mchawi aliyepewa kazi ya kutafuta wafanyakazi humshika yule kijana na kumpaka madawa ya kumpumbaza na kumfanya asionekane kwa macho ya kawaida, hubaki naye ndani ya nyumba.
Ndugu mnachukua mgomba wenu na kuanza maandalizi ya mazishi, kwa kawaida vifo vya aina hii huwa vina vituko vingi sana, ndugu kutokuelewana, jambo dogo unazuka ubishi hadi watu wanapigana.
Jambo muhimu sana kwa wachawi hawa kukamilisha shughuli ni kuwafanya ndugu wakubali kuwa ndugu yao amekufa, na mbinu kubwa wanayotumia na kuhakikisha ndugu wanalia sana. Wakiona hakuna mtu anayelia, atatokea mtu hasa mwanamke atakuja analia sana na kujitupa chini kwenye vumbi, ajabu iliyoje ni kuwa huyo mwanamke atakua hajulikani kabisa kwenye hiyo familia.
Ndugu wanapoanza nao kumlilia ndugu yao, basi mjue kilio chenu ndiyo rukhusa ya wachawi kuondoka na ndugu yenu, kama ndugu wakitulia kabisa, ukweli ni kuwa hawa wachawi hawataweza kamwe kumwondoa ndugu yenu ndani ya nyumba yake.
Kama wamefanikiwa kuondoka nae, zipo dawa za kumsafisha asionekane na dawa zingine ananyweshwa ulimi unarudi ndani ya tumbo na hataweza kuongea. Misukule huwa wanalishwa sana pumba za nafaka, damu za watu na nyama za watu waliokufa.
Nini cha kufanya wachawi wasiniibe?Binadamu ana mwili na ndani ya mwili kuna roho, roho ya mtoto, roho ya kijana na roho ya mzee zote ziko sawa, tofauti ipo kwenye mwili uliovalishwa hiyo roho. Kwa taarifa yako watoto ndio wanaotumiwa sana kwenye ulozi kuliko vijana na wazee.