Rose Bud
JF-Expert Member
- Jul 9, 2013
- 252
- 258
UmeuaaaaaaUkitaka kumwona msukule live, kutana na team Wema.
Cc: Evelyn Salt
UmeuaaaaaaUkitaka kumwona msukule live, kutana na team Wema.
Cc: Evelyn Salt
Zipo aina nyingi za kuchukua watu misukule, aina iliyozoeleka sana ni mtu kufa kisha mwili wake ukazikwa, aina ya pili ni wachawi kuondoa nafsi ya mtu akiwa hai na kuingiziwa pepo na akaendelea kuishi, aina ya tatu ni wachawi kuchukua nyota ya mtu na kuuziwa mtu mwingine.
Itakuwa aisee kuna siku nilimwona MTU wa ajabu mno aisee nilishtuka balaaaKariakoo ipo misekule mingi Sana pale
Uzi noma ule niliusoma sikulala siku mbili had nikawa sijielewi nahisi nimezungukwa ña vtu visivo vya kawaida kutetetemeka na baridi juu
mkuu naomba kufahamu kuhusu aina hiyo ya pili na ya tatu namna wanavyochukuliwa na wanavyofanyishwa kaziZipo aina nyingi za kuchukua watu misukule, aina iliyozoeleka sana ni mtu kufa kisha mwili wake ukazikwa, aina ya pili ni wachawi kuondoa nafsi ya mtu akiwa hai na kuingiziwa pepo na akaendelea kuishi, aina ya tatu ni wachawi kuchukua nyota ya mtu na kuuziwa mtu mwingine.
Habari wanajukwaa.
Natambua uwepo wa watu wenye ufahamu na uzoefu katika mambo mbalimbali nami nikaona nipate kufahamishwa jambo hili.
Tangu nikiwa mdogo hadi zama hizi nimesikia na ninaendelea kusikia kuwa mtu fulani hakufa bali amechukuliwa na kufanywa msukule. Hii taaluma ya uchukuaji watu na kuwafanya misukule ipo au ni hadithi tu za kufariji watu? Kama ipo inafanyaje kazi? Nani amewahi kushuhudia msukule na uko katika hali gani?
Mwisho wa msukule (kama upo) ni nini, je atakufa tena kwa mara nyingine au anafanyaje maana hadithi zilizopo ni kuwa lazima mtu afe kwanza kwenye macho ya watu kabla ya kufanywa msukule.
Langu ni hilo tu karibuni sana.
Zipo aina nyingi za kuchukua watu misukule, aina iliyozoeleka sana ni mtu kufa kisha mwili wake ukazikwa, aina ya pili ni wachawi kuondoa nafsi ya mtu akiwa hai na kuingiziwa pepo na akaendelea kuishi, aina ya tatu ni wachawi kuchukua nyota ya mtu na kuuziwa mtu mwingine.
mkuu naomba kufahamu kuhusu aina hiyo ya pili na ya tatu namna wanavyochukuliwa na wanavyofanyishwa kazi
Hakuna formula na mara nyingi haya ni mambo ya vijijini misukule huhifadhiwa vichakani porini na kwenye Mashamba mbali na vijiji
Duuh hii mbona hataree..!!JE MSUKULE NI NINI?
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.
Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.
Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.
Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.
Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.
Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.
Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.
Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.
Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.
Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)
Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia “Mortoo tombo Mivi” maana yake ni kwamba “aliye ndani ya kaburi ni wangu”
Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.
Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.
Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.
Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.
Kwa hiyo Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.
Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo DRC na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia.
Na hapaTanzania WAPO kAA CHONJO...
Ukiwa na Shida yoyote ile unaweza kunitafuta Kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
Nasikia na damu pia ndiyo chakula chao.Ni kweli ?Halafu chakula chao ni unga wa sembe na vitu vingine vikavu kuepusha kwenda maliwatoni kila mara
duu hii ni hatari zaidi yaani kumbe mtu uko mzima unatembea lakini ni msukule na nyota yako inatumiwa na wengine hii hatari sanaKila mtu anayo nyota yake ya mafanikio katika maisha yake, bahati mbaya nyota hizi huwa zinaonekana kwa macho ya wachawi (wanajimu). Wachawi hawa wanao uwezo wa kuchukua nyota za watu na kuziuza kwa watu wengine, watu wanaoadhirika sana na tatizo hili ni wanafunzi, utakuta mtoto wako anafanya vizuri sana kwenye masomo, anashika namba ya kwanza darasani, ndani ya darasa hilo hilo anakuwepo kijana ambaye kimasomo haelewi chochote, wazazi wake wanamchukua kwa mganga, mganga anampa kitu chochote cha kutafuna anamwambia ampe yule kijana anayeongoza darasani, yule kijana atakapokula lile tunda/pipi kichwa kinaanza kumuuma sana, anatibiwa hospitali zote bila ya kupata nafuu yoyote, inafika wakati mtoto anasahau hata chumba chake cha kulala, huku mkihangaika na tiba ya mtoto wenu kijana mwezie atakuwa ndiye anayeongoza darasani. Uwezekano wa kurudisha nyota iliyoibiwa upo sana, na nyota inaporudishwa maisha ya ushindi yanachanua tena. Mtu anakuwa na nyota ya biashara, uongozi, kupendwa, siku wachawi wanapochukua hizi nyota shughuli zako zinadorora biashara inakufa na baadaye kupotea kabisa, ukiwahi kurudisha nyota yako maisha yanarudi kama mwazo na wale waliokuwa wanazitumia wanabaki mazezeta.
Nilishuhudia kiongozi fulani alikuwa anatembelea nyota ya kununua, ikafika siku mwenye nyota yake akaenda mahali nyota yake ikarudishwa yule jamaa hadi leo ni zezeta kabisa.
Umewahi kuona watoto mazezeta hasa katika familia zenye ukwasi wa fedha wa kutosha, kinachofanyika kwa baadhi yao ni kumtoa kafara mtoto wake, wachawi wanahamisha ufahamu wa mtoto na kushushwa kuzimu, mtoto anawekwa eneo la biashara au nyumbani kwa uangalizi wa juu sana, kinachofanyika katika ulimwengu wa roho wa kishetani ni kuwa ule ufahamu wa mtoto kuzimu ndio unaowezesha biashara yako ikuwe na kunawiri, kuna ishara anazofanya yule mtoto zezeta, mwenye mtoto anazijua maana ya hizo ishara, kuna ishara zingine utaona duka linafungwa haraka na kuanza kuchoma ubani. Huyu mtoto kitu chochote atakachokitaka ni lazima kitafutwe kwa gharama yoyote na apewe.
Ipo siku nilifika kwa rafiki yangu tuliyesoma naye, ana biashara kubwa ya malori mengi ya mafuta na mizigo, yeye nae alikuwa na kijana wake zezeta, wakati tukiwa tunaongea, yule kijana akafanya ishara kama anaendesha gari na kubadilisha gia na kupiga honi, mimi niliona kitendo kile kama jambo la kawaida, lakini baba yake alisimama ghafula na kuingia ndani mara nikasikia harufu ya ubani na makokoro mengine yanachomwa, kwa hali ile sikuweza tena kuendelea kukaa pale nikaanga kijana wake wa kazi na kuondoka. Kesho yake tukapata habari kuwa mmoja ya lori lake lililokuwa na mizigo ya kwenda Congo limeanguka na mali yote kupotea.
Siku zote biashara za kichawi huishia kubaya
Hapana misukule hawapewi damuNasikia na damu pia ndiyo chakula chao.Ni kweli ?
uwiiiiiiiiiii mbonaa hiii hatari sasa .......Nasikia hata kula anaweza kuwa anakula na wewe ila hujuwi, jamani hii kitu ipo sana
Sasa tufanyaje?duu hii ni hatari zaidi yaani kumbe mtu uko mzima unatembea lakini ni msukule na nyota yako inatumiwa na wengine hii hatari sana