Mstari gani au verse ya FID Q umekubamba?

Mstari gani au verse ya FID Q umekubamba?

Asiye mpenda ndugu yake anaye mwona hawez mpenda mungu asiyemwona!!!!!! Halafu !!!!! Adui yako unaye mmudu ni vyema kumuombea dua kwa mungu unayemwamini ili aendeleee kumuumbua ! Tisha mbaya mbovu
 
kwenye neno anasema....

Weupe ungekuwa mali basi weusi ungepakwa rangi.
 
Na sitosita kusema asante au kuwasifia mkinisaidia,washkaji baadhi hawana haki ya kuipressure hii medula,wako radhi kukupa pombe na siyo pesa ya kula
[emoji445] [emoji441]
 
Korombwea hayo maisha ya kuungaunga, hiyo shughuli mi naiweza
Hapa utaambulia ushauri ukihitaji msaada wa kifedha
Mi kujiita rasta, wenye chuki tu wanapinga
Wanashangaa na kula nyama, hawajui nyota yangu ni ya simba
Asiye fikiri kabla ya tendo, atatendwa pale akidamka
Na usinidiss kwa kiswahili kama hujui hata kukitamka
Kuongea sio kusema na kufumbua macho sio kuamka
Wasiwasi ukiwanyima raha, mistari itawafanya kuchangamka
Mnapagawa na baadhi ya mambo ambayo nayajua
Pia nna uwezo kufanya mpaka madawa yanaugua
Hii ni I level, sio high level ndio maana hunioni
Waulize wenzako, Fid Q yupo juu zaidi yako homie
Nipo juu, je utanibana kama kizibo cha soda?
Kushuka ngazi tu unahema, je kuzipanda hupati uoga?
Amini usiamini, Fid Q ndiyo sauti ya mtaani
Je, mtafurahi nikishuka chini kama mademu wa marubani
Bora kuogopwa, wakikupenda watakuchukia
Nilipo na nilipo anzia, sipo napo hitaji nibaki pia
Si hofii kupitwa ilimradi muda usiniache
Hii ni kwa wote, popote
Siogopi kuomba mvua najua mnayahofia matope
Mwingine anakurupuka ananiiga, anasema sifai
Naona vibaya kumjibu, sahau kutupa mawe juu ya mayai
Chipukizi chapeni kazi ili mng'atuke mlipokwama
Vumilieni kama nyota mtatoka jua likizama
Ni binadamu sijakamilika, kuandika rhymes sikosei
Japo miluzi ni mingi lakini jibu huwa sipotei
Nitaendelea kuwa mshindi wa juu ka majani na record Bongo
Nakutembea kifua mbele utadhani nimedundwa ngumi ya mgongo
Kila mtu fid q hivi,mara fid qvile
Yaani fd q, fid q,fd q tuuu, ni hayo tu....

Sijui ni na nini nimesahau mengine hehehe
 
Mi ni mbishi muulize hata Nikki hatopinga/hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka LA simba
 
sio ujanja kama wanadada vyuoni
wanasoma mchana kisha wanafanya uchangudoa jioni
then wana act as a virgin in the morn@raykidd
 
Back
Top Bottom