Msisahau

Pole sana dada kwa yaliyo kukuta. Jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa alimuacha mtoto akiwa salama. Kutokana na uzoefu kidogo wa wasichana wa kazi, mimi nawaweka kwenye makundi matatu. Kundi la kwanza ni la wasichana ambao nia yao ni kufanya kazi kwa moyo ili kujisaidia.

Kundi la pili ni la wasichana, wanaokuja mjini kwa mission. Inaweza ni ikawa ni kuiba mume wa mtu au mali za mwajiri wake. Huyo dada naona anafit kwenye kundi hili.

Kundi la tatu, ni wasichana wanaofanya kazi kwa lengo la kutimiza matakwa yao ya kishirikina. Hii ndiyo kundi hatari zaidi, kwani kuna baadhi ya nyumba dada huyu akiingia familia nzima inavurugika, na hata uwezekano wa kudhuru mwana familia ni mkubwa.

Nitajaribu kuandika kwa mtazamo wangu sisi tulioajiri wasichana wa kazi nini tufanye angalau kutusaidia kupunguza kama siyo kumaliza matatizo kama haya. Kila mwajiri angependa kupata msichana aliye kwenye kundi la kwanza hapo juu, jambo la kujua ni kuwa, ni rahisi sana kwa msichana wa kundi la kwanza kuhamia kundi la pili, na sisi kama waajiri tunaweza kuchangia kuwahafanya wakawa hivyo. Si rahisi kundi la pili au tatu kuja kwenye kundi la kwanza.

Jambo la muhimu kwa waajiri ni kujitahidi kuwajua wasichana tulionao. Njia moja wapo ni ya kuuliza maswali yale yale mara kwa mara. Mfano, kabla ya kuja hapa ulifanya kazi wapi? Umewahi kukaa na watoto? Majina ya watoto. Ukiuliza hayo maswali, msichana wa kundi la kwanza maelezo yake yatakuwa consistent. Lakini kundi la pili, kwavile kuna info anataka kuficha, haitachukua muda kugundua kuwa anadanganya. Kwa kundi la tatu, kumtambua ni kwa kuwa na utaratibu wa kuabudu nyumbani kila siku. Hii itasaidia familia kupata ulinzi wa Mungu, na hata huyo msichana hataweza kuendelea na kazi, atatoa visingizio vya kuacha tu.
Maelezo yangu ni ya ujumla sana, lakini wakati mwingine kuna hatua mahsusi mwajiri anapaswa kuchukua kutokana na mazingira halisi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom