Kwa ajili yako Maimuna

paartey

Member
Jun 26, 2023
39
53
KWAAJILI YAKO MAIMUNA

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 01

MAWASILIANO: 0783642467

ANZA NAYO.........

Rehema mwana mama wa miaka 63 aliyejaaliwa watoto wawili wakike na wakiume ambao kwa umri huo wa mama yao tayali walikuwa ni watu wazima na kwakuwa familia yao ilikuwa ya kimasikini sana walisimama kwa pamoja kumsaidia mama yao ambaye yeye pia aliwalea watoto hao kwa shida sana tangu baba yao mzazi alipofariki.

Rajabu na shyna ndio watoto halali wa bi rehema lakini pia kulikuwa na binti aliyekuwa akiitwa maumuna.

Maimuna hakuachana umri mbali na rajabu kwani rajabu ndio alikuwa wa kwanza kuzaliwa kisha akafatia shyna hivyo basi kama maimuna angekuwa ni mtoto wa bi rehema maimuna angekuwa ni mtoto wa pili kuzaliwa....

Maimuna aliokotwa na bi rehema akiwa na umri wa miaka 12, bi rehema alimfanya maimuna kama mtoto wake na kila mtu alimtambulisha kuwa maimuna ni binti yake, lakini bado maimuna alitofautiana vingi sana na watoto wa bi rehema maimuna alikuwa na mwili mkubwa, shape ya kwenda na rangi fulani hivi wale watu wa ovyo wanasemaga karangi ka kuchanganya watu, alikuwa mweupe kiufupi halafu alienda hewani (mrefu ) na umbo lake liliwachanganya wanaume wengi Sana wa pale mtaani kwao uswazi, tofauti nyingine ambayo maimuna alikuwa nayo ukiambatanisha na wenzie maimuna alikuwa mvivu mno yaani kwenye kazi mvivu sana anachojua ni kula kulala lakini pia kuna kile kitu ambacho kinaitwa uchoyo kwa maimuna tunatoa uchoyo tunaweka roho mbaya .

SONGA NAYO......

Bi rehema alikua mgonjwa sana kwa kipindi iko kutokana na umri kwenda ukichanganya na unene aliokuwa nao ndio kabisa presha ndio ugonjwa wake mkubwa hivyo ni alikuwa mtu wa nyumbani na watoto zake ndio walikuwa wakitafuta uku na uku

"Maimuna mama kaniletee maji ya kunywa binti yangu "

"We nawe unachosha sasa aaah kila muda kutuma tu kwani uwezi nyanyuka....."

Alifoka maimuna baada ya bi rehema kumuagiza maji

"Nisaidie tu binti yangu Nisaidie jamani "

"Tusisumbuane...."

Alijibu maimuna na aliona kama anachoshwa aliinuka na kuondoka eneo ilo maimuna alichokuwa anakijua ni kuchezea simu yake tu hakuna kitu kingine anaweza kufanya

"Maimuna....."

Aliita bi rehema na muda huo alikohoa mfululizo na hakupata msaada, alijikaza na kufata maji ya kunywa mwenyewe na baada ya kunywa akajisikia nafuu....

Majila ya jioni alirudi shyna na na beseni lake la mboga mboga na matunda

"Shikamoo mama...."

"Marahaba za utokako ??"

"Aaah uko hali mbaya mama kama uonavyo matunda kama yote Yamebaki lakini pia nashukuru ata mboga zimeisha....."

"Mungu mkubwa pole mwaya na mchoko naona una vumbi hadi usoni mwanangu "

"Mama nawe vumbi kawaida, maimuna yuko wapi ??"

"Eeeh sijui kaenda wapi, kaninunulia vichipsi hapa nimekula naona katokomea "

"Kikubwa amekununulia kitu cha kula, vipi dawa ??"

"Eeeeh nimesahau kunywa mwayaa niletee "

"Ona mama nawe kama mtoto lakini maimuna anajua muda wako wa Dawa "

"Aaah maimuna anachoka na yeye si unaona usafi wa nyumba na kila kitu "

"Lakini ni majukumu yake ye amekataa kubeba beseni la mboga basi nyumbani anatakiwa kitimiza wajibu wake....."

"Mambo madogo hayo...."

"We bibi, maimuna kakununulia chipsi saa ngapi ?? Me si ndo nimekupa miogo hapo na kukufanyia usafi ??"

Alidakia mama rukia ambaye alikuwa ni jilani yao wa karibu sana na kuishi nao vizuri wakawa kama ndugu muda mwingi alikuwa karibu kumtazama bi rehema pale tu watoto zake wanapokuwa wameenda kutafuta

"Aaah jilani utani gani bhana
..."

"Mama ebu kaa kimya umesema usafi umefanya wewe ?? Maimuna alikuwa anafanya nini ??"

"Yuko bize na simu yake "

Shyna alichukia sana na kumuangalia mama yake kwa hasira lakini hakumlaumu wala kumfokea kwani ni mkubwa wake na hakutaka kumkosea mama yake alibaki na hasira zake.

Alitoa mboga za majani na kuanza kuandaa, lakini alionesha wazi kabisa kuwa alikuwa na hasira na muda mfupi tu akaingia maimuna yaani muda wote na simu yake alipomuona shyna akaweka simu yake mfukoni haraka

"Eeeh umerudi ngoja nikusaidie kupika...."

Shyna alimtazama tu kisha akatabasamu

"Pumzika umechoka sana kufanya usafi lakini pia kupika mchana na kila kitu nitapika "

"Jamani we ndo unachoka sana mdogo wangu Sawa nitafanya umetembea Juani siku nzima...."

Yaani hapo shyna hasira ndio ilikuwa ikiongezeka lakini mwisho wa siku shyna ndio alipika maimuna alifurahia hiyo ofa....

Majila ya saa 6 usiku rajabu ndio aliwasili nyumbani akiwa amechoka sana kwakuwa nyumba yao ilikuaa tu ya nje akatoa fungo yake na kufungua mlango kisha kuingia ndani muda mfupi hodi ikasikika mlangoni mwake

"Atakuwa nani usiku huu "

Alijiuliza rajabu lakini ni kama mtu wa nje alisikia hivi akaitika

"Ni mimi shyna fungua...."

Aliposikiwa kuwa ni dada yake haraka akatoka nje mawazo yake walimpeleka mbali sana aliamini uenda mama amezidiwa, maana shynaa na maimuna ndio walikuwa wakilala na bi rehema ...

"Mbona saa hizi kuna shida ??"

Aliuliza rajabu baada ya kufungua mlango

"Ndio ...."

"Shida gani mama anaendeleaje yuko sawa....??"

"Achana na mama yuko sawa na amepumzika, ni kuhusu maimuna tabia zake zinazidi kunikela kila siku "

"Lakini kuhusu yeye si ulinipigia tukaongea jamani au kuna kingine ??"

"Ilo ilo we unaona ni dogo yaani afanyi chochote sasa fikilia isingekuwa mama rukia mama angekula nini leo ?? Halafu mambo ya kuniambia nimuache kwakuwa ni mkubwa kwangu sitaki yaani ni mkubwa sawa lakini ukubwa wake wa kijinga mno...."

"Nitazungumza nae kesho niko ofu "

"Eeeh kwa mara ya kwanza umepata ofu "

"Yaaah wameongezeka wahudumu wawili si unajua upande wa wahudumu wa bar tulikuwa wawili tu sasa yupo wanne...."

"Kwakweli kesho upate usingizi mzuri kaka yangu "

"Nitalala nikirudi mtaani maana nitaingia kuuza matunda "

Nyie hii familia hata kama ndio masikini ila ilibarikiwa umoja na akili ya utafutaji yaani kwa uzuri wa rajabu kwa watu ninaowajua mimi hakuna mtu angeweza kubeba beseni la matunda na kutembea nalo.

Basi dada na kaka walimaliza mazungumzo yao na kila mtu akaingia chumbani na kulala....

Asubuhi kama kawaida walisaidiana kuchota maji na kufanya usafi mwingine ilikuwa ni asubuhi sana na majila ya saa 1 asubuhi maimuna akabeba beseni la mboga na rajabu akabeba beseni la matunda wakaingia mtaani....

Majila ya saa 7 maimuna akarudi na beseni la mboga likiwa vilevile yaani aliuza mafungu mawili tu

"Eeeh nimechoka jamani...."

Alizungumza baada tu ya kushusha beseni la mboga

"Weeeeh mboga zote hizi na umerudi nyumbani....??"

Aliuliza shyna maana alishangazwa na kitendo cha maimuna kuwao kurudi akiwa na mboga nyingi sana....

"Wateja wamekuwa shida sana"

"Ndio maana nilitaka kwenda mimi uko mtaani "

Alizungumza shyna kwa hasira akaingia ndani na kumuaga mama yake kisha akabeba beseni na kuingia tena mtaani

"Na rangi hii nipigwe na jua mie...."

Muda huo huo alilambwa Kofi moja zito la mgongoni
...


"Mama.....🥹"

Alishtuka na kuita mama

"Maimuna wewe huoni umuhimu wa hii kazi sio ?? Unajali rangi yako tu si ndio ??"

Alifoka bi rehema na aliamua kusimama sasa kama mama na siku hiyo alikuwa na afueni...

"We nawe usinisumbue unanifananisha me na vipanya vyako
......"

Yaani maimuna alikuwa na dharau ya waziwazi kwa bi rehema akiamini kuwa hakuna kitu anaweza akamfanya, lakini kwa rajabu na shyna alikuwa akiwaigizia na kujifanya mtoto mwema...

Bi rehema aliendelea kulalamika maimuna akamsukuma bi rehema ambaye alianguka kama mzigo kisha yeye akaingia ndani

"Maimuna unaniua mtoto wewe...."

Alilia bi rehema...

"Tena koma me sio binti yako
...."

Alizungumza maimuna uku akitokomea mtaani kwenda kuzulula....

ITAENDELEA
MAIMUNA.jpg
 
KWAAJILI YAKO MAIMUNA

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 03

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO.....

NB: HII SIMULIZI HAIUZWI NI OFA KWA FANS WANGU OGOPA MATAPELI HAKUNA KUNUNUA NI BURE ILA USIJE INBOX UTAIPATA POLEPOLE NIKIPOST........

TUENDELEE........

Mdada yule aliyejulikana kwa jina na Nagma alionekana kuvutiwa sana na Rajabu muda wote alikuwa akimtazama kwa jicho fulani hivi mpaka rajabu akawa anamuonea aibu, kwa siku hiyo rajabu alifanya kazi pasi na kupumzika....

Muda wa kufunga ulifika marafiki wa nagma walikuja kuchukuliwa na wanaume zao isipokuwa nagma ambaye alikaa pale na alikuwa amelewa, sana bar ilifungwa na mlinzi alikuwa akimfukuza nagma Rajabu hakuona sawa kumuacha nagma ambaye mpaka muda huo alikuwa akipiga simu ya mpenzi wake ambayo haikupokelewa muda wote

"Dada twende......"

"Unataka unipeleke wapi ?? Siendi kokote mume wangu kaniambia nikilewa nisiendeshe gari siendi sehemu...."

Alilalama Nagma na pombe zake muda huo simu yake aliweka pembeni pochi yake ilikuwa na pesa nyingi sana na ilikuwa wazi rajabu aliiangalia sana akaichukua akaweka na ile simu akambeba binti nagma na kuondoka nae mpaka kwenye parking kwakuwa gari iliyobaki ni moja ilikuwa rahisi rajabu kugundua kuwa ilo gari ni la Nagma alichokifanya ni kuifunga vizuri muda huo nagma hakuwa akijielewa alikuwa akitukana tu na kutoa maneno ya ovyo juu ya mume wake ambaye hakupokea simu yake wala kumfata kule bar.

Rajabu aliita tax ambayo moja kwa moja iliwapeleka nyumbani kwao kule uswazi

"Eeeh jamani huyu nani tena ??"

Aliuliza maimuna ambaye kwa muda huo yeye ndio alikuwa macho akichezea simu

"Acha kuuliza na usogee hapo nipite...

Ilikuaa ni usiku na upepo ulikuwa kama wote lakini sasa kwa shida aliyoipata rajabu kwa kumbeba huyo mwanadada alikuwa akitokwa na jasho jingi sana

"Huyu nani kwani ??"

Maimuna akuchoka akaendelea kuuliza

"Ni mgeni wangu sizani kama kuna kitu kingine unataka kujua, siwezi ingia chumbani kwenu kamuite shyna aje mumshike kumpeleka chumbani "

"Yaani na mapombe yake aje kulala ndani kwetu ?? Hapana kwakweli me siwezi lala na mtu ananuka mapombe kiasi iko....."

Muda huo rajabu alikuwa ameshamlaza Nagma kwenye kochi na alikuwa ameshikilia pochi yake tu, maimuna kweli alizamilia aliingia chumbani kwao akazima taa na kufunga mlango kabisa, rajabu hakuwa na budi zaidi ya kumpeleka Nagma chumbani kwake kwani sebuleni kulikuwa na mbu sana lakini pia hakuweza kumuacha pale ikiwa yeye ni mgeni Wao....


Asubuhi wakwanza kuamka alikuwa ni Nagma alishtuka sana kujikuta kwenye nyumba kuu kuu ambayo tandabui ndio walikuwa mapambo makuu ya chumba iko lakini bado vitobo vidogovidogo vya bati ilo pia ndio vilikuwa vikipitisha mwanga kwenye chumba iko.

Nagma alibaki akitalii chumba kizima na kujiangalia na alikuwa na uchovu sana kutokana na pombe nyingi alizokunywa ndani ya usiku uliopita, katika kutaka kushuka ili atoke nje na kujua yuko wapi alishtuka baada ya kumkanyaga mtu

"Yaaalaaaah"

Alishtuka rajabu ambaye usiku kucha alilala chini kabisa tena kwa kutandika kiloba baada ya kumuacha Nagma kulala kitandani

"Ooooh am so sorry daaah, nisamehe umeumia....??

Aliuliza Nagma kwa haraka sana baada ya kuhisi kuwa rajabu atakuwa ameumia

"Amna niko sawa...."

"Ooooh rajabu sio ??"

Nagma alionekana kumkumbuka vizuri sana rajabu

"Ni mimi...."

"Hope sikukusumbua jana, lakini naomba kuuliza nilifikaje hapa na ni wapi ??"

"Aaah hapa ni nyumbani kwetu sisi na mimi ndio nilikuleta ulikuwa mwenyewe baada ya wenzio kuondoka, lakini pia bar ilifungwa sikuwa napajua kwako na nisingeweza kukuacha peke yako pale maana dunia imeharibika sana "

"Ooooh so sweet jamani, asante sana Mungu akubariki "

"Usijali aaah njoo...."

Rajabu akamshika mkono Nagma na kumtoa nje hapo alimkuta shyna akifanya usafi yaani alikuwa akifagia uwanja na maimuna alikuwa amelala tu

"Oooh karibu....."

Alikaribisha shyna kwa heshima zote uku akicheka cheka tu

"Aaah muwekee maji na umpatie gauni yako moja avae...."

Na kweli alitakiwa kubadili nguo maana mavazi yake yalikuwa mafupi mno na kufuani sehemu kubwa ya mwili wake ulikuwa wazi....

"Sawa....."

"Ngoja nikamuangalizie supu...."

Alizungumza rajabu na kuondoka shyna akaingia ndani akatoka na kitenge kimoja kisha kumpatia Nagma, haraka akamuwekea maji na kwenda kuoga...

Baada ya dakika kadhaa rajabu alirudi akiwa na kontena la supu zile za mtaani yaani bandama na mapupu supu yangu pendwa

"Sijui kama unakulaga supu yetu ya bei rahisi...."

Alizungumza rajabu uku akikabizi contena ya supu kwa Nagma ambaye muda mwingi alikuwa akimtazama rajabu usoni na kutabasamu

"Weeeh kwahiyo huyu ndo wifi yangu ??"

"Shika adabu yako wewe ? Yaani nilete mwanamke kipindi hiki ?? Thubutu kwanza sina mwanamke "

"Mmmmh sema kweli sema mzuri huyo na kapendeza hatari "

"Kapendeza na nini.?? Yale mavazi ya nusu utupu au ? Ila sijui wanawake mna nini nyie kama uzuri unao utaonekana tu sio mpaka uvae mavazi ya wazi "

"Sawa ba mchungaji, tuachane na hayo sasa kama sio wifi mbona katokea chumbani kwako na mmependezana "

Rajabu alikuwa mtu muwazi sana kwa dada yake alitumia muda huo kumuelezea kwani walikuwa nje wakichota maji na Nagma alikuwa ndani akinywa supu si unajua ugenini lazima ule polepole


"Huyu maimuna sasa anatupanda kichwani yaani anaonesha chuki za waziwazi kwahiyo kagoma kabisa huyu mdada kulala ndani kwetu ??"

"Ndo hivyo....."

"Subili nimfate"

"We nawe fliji lako lilivyokuwa aligandishi kumbuka mama alisema kuwa tusije tukafanya mambo ambayo yatamfanya maimuna ajione mpweke.."

"Hapo ndo unanikelaga tena usiwe unamtajaga mama kwenye magoda ya mai....."

Shyna alionekana kuchukia sana akabeba ndoo yake ya maji na kurudi ndani

"Asanteni sana nimeshiba "

Ile kuingia tu Nagma aliwashukuru kwa supu

"Aaah nisiendelee kupoteza muda naomba niwaache na kuhusu gauni yako nafikili nitailejesha leo jioni hapa au kazini kule "

Alizungumza Nagma kwani kwa wakati huo alikuaa amevalia gauni ya shyna

"Haina haja unaweza ukabaki nalo "

"Kweli.....??"

Aliuliza Nagma akionesha kuwa ametokea kulipenda sana gauni la shyna

"Ndio "

"Asante sana nitakuletea zawadi sasa rajabu wacha nikuache mie niwai maana na muda wa kazini umefika nitapitiliza "

Basi rajabu akakabizi pochi ya Nagma na kumsindikiza kidogo mpaka barabara kubwa, Nagma alifurahishwa sana na familia ya kina rajabu na hakuwa amemuona maimuna kwa siku hiyo kwani alikuwa bado amelala.

Rajabu baada ya kumsindikiza Nagma akarudi nyumbani lakini alishtuka baada ya kuona watu wakiwa wamejaa pale nje kwao aliwai na kitaka kujua nini kinaendelea alishangaa sana baada ya kukuta shyna akiwa anapigana na maimuna tena adhalani na hakuna jilani ambaye alikuwa akiwaamulia zaidi ya mama rukia haraka rajabu akadandia tawi la mti wa mwarobaini na kuanza kuwatandika kama watoto kila mtu alikimbilia ndani wakabaki wakitumpiana maneno uku na uku....

ITAENDELEA.....
 
KWAAJILI YAKO MAIMUNA

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 04

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO......

"Nimesema kimya wote kimya, msinifanye mtoto mdogo hapa naongea na nyie mnaongea "

Alifoka Rajabu baada ya kuona maneno yamekuwa mengi

"Mwambie huyo mdogo wako sijui shyna amekuwa na shida gani na mimi amekuwa akinifokea kama mdogo wake anaongea maneno machafu juu yangu anaongea kila aina ya maneno ya ovyo juu yangu yaani mimi umu ndani sitakiwi kufanya maamuzi kwasababu sio kwetu si ndio ?!

Alizungumza maimuna akilia sana na hayo mazingira amekuwa akiyatengeneza kila siku yaani kila akifanya kosa anatengezeza mazingira ya kuonekana kuwa ananyanyasika....

"Maimuna kaa kimya sijui mnagombania nini lakini pia sitaki kujua nachotaka mnyamaze nataka kuzungumza kitu....."

Kila mtu akakaa kimya

"Mmeangaliwa kuwa saa hizi ni saa ngapi ?? Mmeangalia majilani kiasi gani wamejaa hapo nje wakiwatazama ninyi ?? Mmewaona majilani wanavyowacheka ? Hakuna ata mmoja alijitokeza kuwaamua isipokuwa mama rukia ambaye ata yeye amechoka sio ndugu anaweza akatuchoka muda wowote na saa yoyote ile sijui kama mnanielewa jaribuni kuwa watu wazima mnaojielewa tazama kama wewe mai unapigana na vazi lako ilo angalia nyonyo lote nje majilani wanaangalia tu, na sasa hivi dunia mkononi si ajabu ukaja kujikuta uko mitandani kwenye page za udaku please msinitie aibu....."

"Lakini ka......."

"Usizungumze shyna nimesema mimi ndio naongea sitaki maoni wala ushauri "

"Ujawai kunipa nafasi ya kuongea, ulivyoondoka tu nikawa natoa vyombo alivyolia da nagma "

"We kila mtu dada yako ?

Alidakia maimuna alionekana kuwa ni binti mkorofi sana

"Unamuona sasa ata kuongea sijamaliza anadakia "

"Naitaji kulala kabla muda wangu wa kazini haujafika sawa ?? Siitaji hizi kelele kila mtu aendelee na shughuli zake na wewe maimuna usitake nikuoneshe hasira zangu hakuna kutoka kwenda kokote leo yaani utulize komwe lako hapo toa hizo futi zako uone kama sijakuvunja miguu "

Alifoka rajabu

"Bora umemwambi anazurula kama kuku mwenye njaa "

"Weeh nawe kaa kimya wigi kama manyoya ya tausi "

Eeeh si wakaanza kutupiana maneno tena mwisho kila mtu akashika njia yake na rajabu akapata muda wa kupumzika....

Kama kawaida muda wa saa 10 rajabu alijiandaa na kufika ofisini....

"Rajabu kuna mzigo wako hapa ameacha msichana fulani hivi alisema kuwa anaitwa Nagma "

"Oooh sawa, asante "

Rajabu alipokea mzigo ule ambao ulikuwa kwenye mfuko mweusi hakufungua kwani ulikuwa ni muda wa kazi akaweka sehemu tulivu na kuendelea na Mishe zake za hapa na pale....

"Shyna mwenyewe iki kibanda mlichoachiwa na mama yenu unaona kama ghorofa sio ??"

"Kwani maimuna mama yangu me sio mama yako ??"

"Unajisahaulisha au .? Me kwani ndugu yenu ? Japo simfahamu mama yangu lakini awezi kuwa kama bi rehema kweli amenilea lakini hakuwa na hadhi ya kuwa mama yangu "

Alizungumza maimuna maneno makali sana ambayo yalimuumiza mno shyna aliangua kilio

"Eeeh msiba mwingine uku "

Alizungumza maimuna na kuondoka uku akimuacha shyna akilia.....

Majila ya usiku kama kawaida rajabu alirudi akiwa amechoka sana alishangaa muda huo kumkuta maimuna akiwa amekaa nje ikiwa ni usiku sana

"Mbona nje muda huu ??"

" shyna amenambia asinione nyumbani kwa mama yake nikatafute mama yangu aliko....."

Alidanganya maimuna ambaye kwa muda huo hatukujua alikuwa na lengo gani maana huyu binti naye ni pasua kichwa

"Kisa nini ?

"Ni ule ugomvi wa asubuhi nikajua tumesahau kila kitu na tunaendelea na mambo mengine lakini mwenzangu amechukulia hasira ameongea maneno machafu sana juu yangu najua mimi sio ndug......."

Rajabu akawai na kumziba maimuna mdomo....

"Usije ukazungumza hivyo Wewe ni ndugu kwetu lakini pia ni mkubwa kwa shyna haya mambo yanazungumzika, lakini kwa sasa hivi wacha nimnyooshe......"

Alichukia rajabu na kutaka kumfata shyna lakini maimuna alimuwai

"Muache haujui na yeye anayapi anayapitia nafikili mpaka asubuhi atakuwa Sawa "

"Sasa utalala wapi ? Lazima tugonge afungue mlango ulale "

"Nitakaa hapa nje ata hivyo sina usingizi "

Unawazimu wewe.."

Alijibu rajabu na kumshika mkono kisha wakaingia chumbani kwa rajabu

"Panda kitandani ulale kwanza umekula ??"

"Ndio....."

Alijibu maimuna kisha akapanda kitandani rajabu alilala chini akiwa na mavazi yake, kulikuwa na joto sana usingizi ulikuwa wa shida sana lakini hakuweza kupunguza mavazi yake akiamini kuwa alikuwa amelala na dada yake baada ya muda kidogo

"Maimuna ni nini lala juu kule......"

"Yaani me nilale juu kaka yangu ulale chini siwezi kabisa bora tuteseke sote apa chini "

"Acha mambo yako basi sawa ?? Acha kabisa "

"Nitalala hapa "

Maimuna alikuwa mkaidi sana na kwa muda huo rajabu alikosa ujanja zaidi ya yeye kuinuka na kukubali kulala kitandani ili na maimuna alale kitandan kwani chini kulikuwa kukiumiza sana..

"Haya sasa ulale "

"Hapa sasa nitalala kwa amani kwani kaka yangu pia amelala sehemu nzuri "

Wakacheka kwa pamoja ila maimuna jamani ni muigizaji mzuri sana .

Baada ya Muda tena maimuna alianza kuangaika na kumshika shika rajabu wa watu mwaya

"Maimuna ni nini.......??"

Aliuliz rajabu lakini pia maimuna hakujibu aliendelea na kazi yake na kwakuwa rajabu na yeye yuko vizuri kama mwanaume hakuacha nafasi ipite hivi hivi bhana na usiku ulikuwa Murua kabisa....

ME SIMO JAMANI NI KAKA JA DADA HAO ila awajashea mama wala baba wala awana undugu wa mbali.

ITAENDELEAKWAAJILI YAKO MAIMUNA 🥹

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 05

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO......

Asubuhi na mapema maimuna aliamka na kwenda kugonga chumbani kwao kule alikokuwa akilala kila siku na shyna

"Yaani ndo unarudi saa hizi kweli ??"

Aliuliza shyna baada ya kumuona maimuna aliamini kua ndio amerudi asubuhi

"Uoni aibu unaweza ukaniambia ulilala wapi wewe ? Me sio mkubwa kwako na sina haki ya kukuuliza hayo maswali lakini kuwa na heshima kidogo fikilia kama ungepata matatizo uko uliko "

"Nipishe mie "

Maimuna alimsukuma shyna kwa dharau sana kisha akaingia ndani

"Hii sasa ni too much aiseeh....."

Alilalamika shyna na kugeuka kutaka kuingia ndani lakini mkono wake ulidakwa na rajabu

"Sasa naona ushakuwa mama mwenye nyumba sio ??"

"Shikamoo kaka "

"Sina haja na hiyo salamu, hivi shyna uko na shida gani ?? Yaani kwanini unampa mwenzio maneno machafu ya kumfanya ajione kuwa yeye sio mmoja wa familia ?? Eeeh sijakuzoea hivyo na sipendezwi na unachokifanya sawa ?? Najua we ni muelewa ukiachana na iko kwanini umkataze mwenzio kulala ndani ??"

"Sio kweli sikufunga mlango kwamba asije kulala nilifunga kwakuwa amechelewa kurudi alipaswa kunigongea kama kweli alirudi jana usiku "

"Ona sasa unaongea ata maneno hayaeleweki, shyna me sijakuzoea hivyo nakujua uko na huruma na uvumilivu kama mama......"

Aiseeh Rajabu alionekana akishika upande wa maimuna moja kwa moja yaani aliona dada yake ndiye mwenye makosa ilo jambo lilimchukiza sana maimuna aliingia ndani akiwa ana lia sana yaani...

Siku hiyo ilikuwa ni ofu ya rajabu hivyo alibaki nyumbani na familia yake lakini pia shyna sio mtu wa kukaa na hasira baada ya masaa kadhaa tu akawa anapiga story na kaka yake wakiwa wamefurahi sana yaani.....

Wakiwa bize na mambo yao wenyewe story zimenoga mara ulisikika mlio wa gari nje kwao na muda huo huo mlango wao uligongwa.....

"Karibu....."

Aliitikia shyna na kwenda kufungua mlango

"Oooh jamani karibu dada "

Alikaribisha kwa furaha sana baada ya kujua kuwa aaliyekuwa anagonga mlango ni Nagma

"Aha Asante mdogo wangu ( alijibu na kuingia ndani ) oooh kumbe leo haupo kazini ??"

Aliuliza nagma baada ya kumuona rajabu

"Ni ofu yangu bhana si unajua tena karibu sana...."

"Asante me sio mkaaji lakini nimelejesha ule mzigo wetu....."

"Oooh jamani me nilikuambia ubaki nao dada lakini kama umerudisha pia sio mbaya Asante sana "

"Sawa ngoja niwaache "

"Sawa jicho uliumia au ??"

"Yaani kuna kitu kilinigonga....."

Basi nagma akatoka nje na rajabu alimfata

"Umejipa kazi na kuchoma mafuta yako bure kabisa ungebaki nalo "

"Amna bhana...."

Rajabu alimsogelea Nagma na kumshika usoni,
" umefanya nini maana ukiachana na jicho uko na alama nyingi uku "

"We acha tu ni kipigo iko siku ile ambayo sikurudi nyumbani "

"Unaongelea juzi ambapo ulilala kwangu au ??"

"Ndio yaani acha tu lakini ndo mambo ya mahusiano na ndoa "

"Samahani kama nitakuwa naingilia ndoa yako au mambo yako lakini nataka kujua kitu siku ile si ulikuwa ukimtafuta ili akufate ??"

"Ndio amesema kuwa alilala na alitaka nirudi mwenyewe "

"Lakini si ulisema kuwa amesema usiwe unaendesha ukiwa umelewa ??"

"Ndo hivyo na aliniaidi kunifata lakini ndio mambo ya ndoa hayo hakuna namna "
"Mambo ya ndoa ?? Ndoa lazima iwe na amani na maelewano lakini sio kupigana kama hivyo "

"Rajabu bhana ata hivyo kuna sehemu nawai tutaonana baadae "

Nagma alionekana kutotaka kuongelea mambo yake ya mahusiano hivyo haraka akaaaga na kuondoka rajabu alibaki akimuangalia nagma anavyooanda kwenye gari mpaka anavyoondoka na kutokomea kwenye barabara kubwa

".mmmmh umempenda eti ??"

Alishtushwa na sauti ya shyna ambaye alikuja nyuma ya kaka yake

"Tutauwana ndo mambo gani hayo ??


"Ila mnapendezana tofauti yenu mwenzio ako na pesa halafu wewe uko hapa unateseka "

"Shyna kwani una nini jamani ?? Sasa hivi umekuwa mkorofi mno ingekuwa enzi zile za utoto nishakutwanga vibao...."

"Ahahq kwani miguu ya kukimbia sina au ??"

"Ni a usingizi naomba nikapumzike kwanza "

Rajabu alitembea kwa mwendo wa taratibu na kuingia chumbani kwake....

"Jamani nimi tunasumbuana....."

Aliongea rajabu akiwa usingizini kwani alihisi kuguswa, lakini hali hiyo iliendelea na kuwa ya kasi zaidia akakurupuka na kukaa wima

"Aaah jamani maimuna nini tena uku ?"

"Kwani dhambi me kuja chumbani kwako ??"

"Yaani unataka nini uku na nimepumzika nimechoka mno "

"Lakini......"

"Lakini nini ?? Toka nje "

Rajabu alichukia na kumfokea maimuna

"Hivi rajabu unanifokea mimi kwaajili ya yule mjinga wako mwenye gari ??"

Kwanza kwa mara ya kwanza maimuna alimuita rajabu kwa jina yake mara nyingi amekuwa akimuita kaka na kama ataita rajabu lazima aseme kaka rajabu

"Umeniita nani ??"

"Si rajabu au unataka nikuite jina gani haya mpenzi....."

"Maimuna we una akili kweli ??"

"Nilikuwa nazo ila kwa sasa hivi sina kwaajili yako "

"Toka nje nimesema "

"Kwani yule amekichanganya na gari au ?? Nambie na mimi nijue nakuchanganya na nini, nimetembea na watu wengi ila we kiboko "

Alizungumza maneno mazito sana ambayo yalimfanya rajabu abaki akimshangaa tu na kumtolea Macho hakuamini kabisa kama maimuna anaeza kuzungumza maneno ya hovyo mbele yake

"Sina mwanamke sina mchumba na sitalajii kuwa naye kwa sasa, na kuhusu wewe ni ujinga wako ulisababisha yote na haya yaishie hapa Mimi na wewe ni kaka na dada toka nje....."

"Unanifukuza sio ?? Haya ngoja nitoke niseme kaka angu kanibaka "

"Unasemaje ??"

Aliuliza rajabu kwashangao sana na muda huo maimuna alifungua mlango na kuanza kupiga kelele lakini kabla ya yote rajabu alimuwai na kumziba mdomo kisha kumrudisha ndani

"Unataka jamii ituonaje ??"

"Wajue ukweli "

"We umekuwaje ? Ebu kaa chini "

"Sikai ila kuna kitu nataka...."

Alizungumza maimuna na kuanza kumsogelea rajabu wa watu mwaya 🥹.

ITAENDELEA
 
KWAAJILI YAKO MAIMUNA

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 06

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO.......

Rajabu alibaki akiwa ameganda na kumshangaa maimuna maana tabia zake zimebadilika sana zinamchanganya rajabu ambaye mtaa mzima walikuwa wakijua kuwa hao ni ndugu yaani baba mmoja mama mmoja.

"Maimuna....."

Aliita rajabu lakini hiyo haikusaidia kabisa maimuna alionekana kuzamilia jambo lake hapo ndipo rajabu alipoamua kusimama kiume

"Nitakuchapa mabao hapa adharani na hautakuja kuamini kitakachotokea ondoka "

Alifoka rajabu lakini pia haikusaidia yaani maimuna ni kama pepo hivi , hapo rajabu aliiinuka na kumshika mkono maimuna alitumia nguvu kumvuta mpaka nje, lakini katika kuvutana maimuna aligonga tumbo lake kwenye mlango na alionekana kuumia sana kwani alipiga ukunga wa hali ya juu uliomshtua kila aliyebahatika kuusikia

"Kuna nini jamani.....??"

Alikuwa ni shyna ambaye alitoka nje haraka baada ya kusikia kilio cha maimuna

"Rajabu unaniua....."

Alilalamika maimuna na ilionesha wazi kuwa alikuwa kwenye maumivu makali mno, lakini rajabu akuelewa kabisa kilichokuwa kinaendelea na kwakuwa alikuwa na hasira sana

"Shyna mchukue huyu mjinga mfungie umo ndani nitakuja kumuua mimi...."

Alifoka rajabu na muda huo majilani walijaa wakiangalia show ile ya bure iliyokuwa ikiendelea kwenyw eneo ilo

"Rajabu mwanangu kuna nini jamani ?? Mbona unampiga dada yako ??"

Aliuliza mama rukia ambaye kwa wakati huo yeye ndio alikuwa mtu wa karibu sana na familia hiyo aliwajali kama watoto wake kiukweli mama rukia alikuwa na moyo wake, lakini muda huo mama rukia aliweza kuona ni kiasi gani damu zilikuwa zikimtoka maimuna hii yote ni baada ya kujigonga tumboni....

"Rajabu nipishe....."

Alizungumza mama rukia kisha akamsogelea maimuna

"Wewe ni mjamzito ??"

"Sijui....."

Alijibu maimuna kuwa hajui kama ni mjamzito au laah

"Mama rukia alisaidiana na shyna moja kwa moja wakamuingiza maimuna ndani akamsafisha kisha wakampeleka hospital

"Me msinipeleke kwenye hii hospital "

Alizungumza maimuna na muda huo walikuwa nje ya hospital

"Yaani tumefika hospital unaanza kukataa una shida gani wewe tunaangaikia afya yako
...."

Alifoka shyna ambaye kwa namna moja alishachoshwa na maimuna

"We nawe usinifokee ndo sitaki kwenda umu tafuteni hosting nyingine, hii hospital inanikumbusha sana kuhusu mama "

Ila nyie maimuna ni muigizani mzuri sana daaah yaani ni kadada fulani hivi kajinga hovyo kabisa.

"Ooooh maimuna karibu "

Ilisikika sauti ua dokta ambaye alikuwa ni mwenyeji sana kwenye hospital hiyo na alionekana kuzoeana na maimuna, yaani kitendo cha daktari kuzungumza na maimuna ndicho kilirahisha kazi ya mama rukia na shyna kwa urahisi kabisa wakaingia hospital na taratibu zilifatwa....

"Dokta huyu ni binti yangu mimi achana na kila kitu kwanza nataka apimwe ujauzito....."

Alizungumza mama rukia,

"We nawe dokta fanya kazi yako ata hivyo me siumwi...."

"Mnanichanganya kimewaleta nini aswah ??"

"Baba angu sikia huyu binti leo ameanguka bahati mbaya "

"Nimeanguka wapi wakati tajabu kanisukuma "

"Kaaah kimya kima wewe, dokta sikia huyu leo ameanguka akaangukia tumbo cha ajabu alianza kutokwa na damu nyingi na mpaka mda huu hapo......"

Maimuna alichukua mkono wake na kumziba mdomo mama rukia, muda wote huo shyna alikuwa nje akiwasubili

"Maimuna ebu njoo hapa kwa hali aliyonielezea mama yake napata wasiwasi juu ya ujauzito wako"

Alizungumza dokta maneno ambayo moja kwa moja alinfungua mama rukia ambaye ni mtu mzima hivyo ilikuwa rahisi kuelewa kuwa maimuna alikuwa mjamzito, basi maimuna hakuwa na jinsi zaidi kufata kile ambacho dokta alikuwa amekigiza.

Baada ya vipimo vya muda wakarudi tena kwenye chumba cha daktari....

"Nafikili maimuna mngemuacha leo alale hapa, kwanza niwapongeze aliyemsaidia mwanzo alifanya vizuri sana, na maimuna yuko sawa yeye na mtoto wake...."

"Unamaanisha nini yeye na mtoto wake ??"

Kwa wakati huo shyna aliweza kuingia pamoja nao na yeye ndiye aliyeuliza swali ilo...

"Maimuna kwani ukumwambia mama ?? Ni jambo la kheri hakuna haja ya kuficha kabisa, ni hivi najua sio sehemu sahihi lakini lazima ujue ili, maimuna ana ujauzito wa miezi mitatu inaenda minne mi vile tumbo alijakua na mimi ndio muhusika nisamehe mama "

Dokta huyo alionekana kuwa mtu powa sana yaani alikuwa mtulivu na muelewa

"Jamani....."

Ma rukia alikosa ata maneno ya kuongea

"Sasa tumuache kwajili ya nini ??"

"Aaah au basi kuna dawa nitamuandikia hapa atapasa kutumia mtapitia pale dirishani bill ni juu yangu wakimuona wanajua "

Dokta huyo aliongea kwa kujiachia sana na alikuwa akimpenda sanaa maimuna na hakuweza kuficha hisia zake, yaani mama rukia na shyna walikuwa kimya wakisikiliza.....

Majila ya jioni waliwasili nyumbani walikuta rajabu akiwa na mawazo sana yaani

"We nawe mbona ulikuwa unapiga simu kama natembea na Figo Zako ??"

Aliuliza shyna baada tu ya kufika nyumbani, maimuna alimpita rajabu chap na kuingia ndani....

"Haya jamani wacha nikaangaliwa wanangu kwanza "

Alizungumza mama rukia na kwenda nyumbani kwake

"Kimejili nini uko ??"

Aliuliza rajabu

"Uwe unashikilia hasira zako ulikuwa unaenda kuua kiumbe cha watu "

Alizungumza shyna na kumfanya rajabu aogope na kutetemeka sana maana akifikilia usiku uliopita alipita na maimuna akahisi eeeh tayali

"Unamaanisha maimuna ni mjamzito ??"

"Ndio "

"Sema kweli "

"Ndo hivyo ni wa miezi mitatu, ashukuliwe Mungu baba wa mtoto anajali sana "

Alizungumza shyna na kumfanya rajabu amsikilize kwa makini sana, shyna hakuwa na sababu ya kuficha chochote kwa dada yake alimsimulia kila kilichotokea hospital

"Daaah Mungu mkubwa kwamba mtoto yuko sawa nilikuwa nikiogopa sana "

"Nikuulize kwanini ulikuwa unampiga da maimuna sio kawaida yako ??"

Aliuliza shyna

"Weeh acha tu ni mambo ya aibu siwezi nikazungumziq hapa muda huu "

Alizungumza rajabu, nauda huo honi ya gari ilisikika

"Oooh nilisahau natoka nitachelewa kurudi hakikisha maimuna anakuwa sawa....."

"Wapi tena ??"

"Nagma huyo na mume wake tunatoka out "

"Kwani da nagma ana mume ??"

"Umbea tu naomba andaa chakula mle hakikisha atoki, na dawa anakunywa nitaongea nae kesho nahisi nitachelewa kurudi....."

Basi rajabu akatoka nje mwenyewe na kwenda karibu na gari ya nagma

"Mmmh shemeji yuko wapi ??"

"Tutamkuta uko uko"

Alijibu nagma kisha akawasha gari safari ikaanza....

ITAENDELEA
 
KWAJILI YAKO MAIMUNA

MTUNZI: PATRICIA ANTONY

SEHEMU YA: 07

MAWASILIANO: 0783642467

SONGA NAYO.......

basi safari ya nagma na rajabu haikuwa ndefu sana ukizingatia ni usiku lakini pia walikuwa na usafiri wao binafsi....

"Karibu sana
...."

Alizungumza nagma muda huo gari ilikuwa imesimamq nje geti kubwa sana na alikuwa akiendelea kupiga honi....

"Uku ni wapi ?"

"Ni nyumbani kwangu naomba kwanza niingize gari ndani halafu mimi na mume wangu kwanini tumekuita umu nyumbani kwetu "

"Nagma, ebu kwanza kabla ujaingiza gari ndani naomba tu unishushe mpaka sasa hivi umeshanidanganya vya kutosha, kwanza ulisema tunatoka out na mume wako mtanifata, ukaja mwenyewe, bado ukasema kwamba mumeo ametangulia sehemu husika sasa hivi unanileta nyumbani kwako nashindwa kukuelewa kabisa....."


"Wasiwasi wako ni nini ? Au hauniamini ?? Me si rafiki yako jisikie amani uko sehemu salama "

"Nishushe bhana usiniletee ujinga mimi...."

"Eeeh sawa ingawa ilibidi kuwa surprise inabidi nikuambie ila ukifika kwa mume wangu usije ukasema kuwa unajua "

"Ni nini ??"

"Niliongea na mume wangu na tukapanga kwamba tukupe kazi ya kulinda bustani yetu tu ni asubuhi tu unayahudumia na jioni kisha unarudi nyumbani, nimefanya hivyo baada ya kuona siku ile boss wako akiwa anakufokea sana , nikaona cha haraka haraka ni hiki kukupa kazi hii lakini sitaishia hapo nitaendelea kukutafutia kazi nzuri....."

Hapo kidogo wasiwasi wa rajabu ulipungua na wakaingia ndani

"Una nyumba nzuri sana da nagma....."

Alizungumza rajabu

"Asante ipo siku na wewe juhudi zako zitakuleta hapa tena zaidi ya hapa '

Walishuka kwenye gari na kuongozana kuelekea ndani ile wanafungua tu mlango nagma hakuamini kumuona mume wake akiwa nawanamke mwingine tena wakiwa watupu kabisa 🥹 nguvu zilimuisha....

"Baby i can explain "

Alianza kujitetea mume wa nagma lakini kwa wakati huo nagma alikuwa na hali mbaya mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kasi sana kwani wote alikuwa anawajua yaani mume wake na mwanamke aliyekuwa naye alikuwa ni rafiki wa nagma ambaye ni wale ambao walikuwa wakiiitana best friend

"Nagka shoga angu nilikuja kuongea na wewe, sijui nini kimetokea"

Alizungumza msichana huyo rajabu alielewa nagma anajisikiaje kwa wakati huo akamshika mkono nagma na kutoka nae nje, akampakia kwenye gari

"Braza naomba nifungulie geti....."

Alizungimza rajabu akimuomba mlinzi ambaye moja kwa moja alijua nini kimetokea kuweni na urafiki na walinzi wenu wanajua mengi sana hawa watu......

Rajabu aliwasha gari na safari ilienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwao ata shyna Alishangaa mbona hawa watu wamewai kurudi kulikoni lakini hakuuliza kwani kwa muda huo nagma alikuwa akilia sana.

"Mpeleke chumbani akalale...."

Alizungumza rajabu na shyna akafanya kama ambavyo kaka yake alimuagiza.

"Umemleta tena ??"

Maimuna akaanza mambo yake kwakuwa walikuwa sebuleni rajabu aliofia kuwa maimuna anaweza akalopoka kitu na dada yake akasikia halafu ikaleta ishi nyingine alitoka nje ambapo aliamini kabisa kuwa maimuna angeweza kumfata na kweli maimuna alimfata rajabu

"Naongea na wewe halafu unatoka nje sio ??"

"Shida yako nini mai ??"

"Shida yangu ni huyu changu wako kumleta umu ndani ikiwa mwanamke wako nipo "

"Mwanamke gani ? "

",unajizima data sio ?? Sasa kama shyna hajakupa taarifa wacha nikupez unatarajia kuitwa baba nina unauzito wako "

"Ooooh hongera binti "

Yaani fanya vyote ila usije kuomba kukutana na dharau za rajabu kaka akiamua kumdharau mtu anamdharau mazima kabisa ndicho kilichomkuta shoga yetu maimuna yaani shwaaaah kajilahisisha halafu hakuna kitu anafanyiwa

"Rajabu huyu mtoto anatuitaji wazazi wake "

"Ukimaliza kutamba mashahiri ingia ndani ukapumzishe fuvu lako "

Maimuna alichukia sana na kunyanyua mkono wake kutaka kumchapa kibao rajabu lakini rajabu aliwai kwa kumdaka mkono

"Usije ukajaribu kunigusa na huu mkono wako mchafu, sawa ?? Nilikuaa nakuheshimu kama dada yangu lakini sasa sina cha zaidi juu yako' sina cha kufanya kwako uwezi kuwa dada yangu najivunia kuwa na dada anayeitwa shyna a sio wewe...."

Alizungumza rajabu kwa hasira kisha akamuachia mkono maimuna kwa hasira sana na kuondoka chumbani kwake....

Sasa bhana show ikaanza asubuhi subuhi ambapo watu walikuwa bize na kujiandaa kwenda maofisini na wanafunzi shuleni maimuna alisimama nje ya uwanja wao na kuanza kupiga kelele na kuita majilani ma kweli mitaa ya uswazi tena kwa ushambenga kelele moja tu watu wakajaa nyie hadi watoto, shyna alitoka nje akiwa na nagma na rajabu pia alitoka nje lakini hakuonesha kushtuka wala kushangaa kabisa ndio kwanza akakaa makini kusikiliz maimuna anajipya gani....

"Najua hakuna mtu anajua kuhusu mimi ila leo naomba mjue, nataka watu wangu wa karibu mjue, kwanza kabisa naomba mjue kuwa mimi sio mtoto wa bi rehema 🥹......"

Shyna alishtuka sana maana mama yao tu alishawai kuwaambia kuwa hii siri ibaki kati yao lakini leo maimuna anaiweka wazi....

"Unafanya nini wewe ??"

Aliuliza shyna uku akijaribu kumzuia maimuna asizungumze

"Tena huyu ambaye anajifanya kunizuia ataki watu wajue kuwa hakuwai kunipenda tangu siku niliyoletwa hapa, siku ambayo bi rehema aliniokota....."

Hapo sasa ndio majilani walianza kujua kuwa maimuna sio mtoto wa bi rehema ndio maana yulo tofauti na wenzie ata rangi ya ngozi zao
....

"Kaka mzuie maimuna "

Alizungumza shyna ambaye hakupendezwa kabisa....

"Muache aongee muache atoe dukuduku lake maimuna mama nikupe na kipaza sauti au sauti yako inatosha ??"

Yaani rajabu alishamzarau maimuna mpaka mwisho....

"Kaa kimya rajabu, kaah kimya bora bi rehema angekuwepo angenisaidia yaani, majilani zangu nataka mjue kua mimi ni mjamzito na niliupata baada ya kubakwa na kaka rajabu......"

Kila mtu alistuka walahi, hata rajabu ambaye alikuwa amekaa chini lakini aliinuka chapu hakutarajia kuwa maimuna anaweza akaongea kitu cha kipuuzi kiasi iko.....

RAJABU aka....

ITAENDELEA
 
Sasa hivi unatupia mwendelezo within few hours, uzi ukipata viewers wengi unaanza nyodo na kuturusha ooh, mara kazi Ni nyingi, mara hamnilipi, mara hamna shukrani, mara njooni WhatsApp kupata mwendelezo n.k.
Kwahiyo mi sitasoma Ila nitaendelea kufatilia hadi pale nitakapoona umefika episode ya mwisho ndo naanza kusoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom