Simulizi: Shemeji

Yellow donaty

Senior Member
Jan 16, 2023
113
271

Kwa wale ambao wamebahatika kuwa na wadogo wa kike. Kwanza ni furaha na inapendeza sana kuona ndugu wakipendana na kusaidiana katika mambo mbalimbali. Embu soma mkasa huu.

Rabia alikuwa akiishi Singida lakini baadaye alihamia na kuishi Dar es salaam ambapo aliolewa na mwanaume mmoja ambaye ni mfanyabiashara jijini Dar es salaam, Kijana huyu alikuwa na uwezo mkubwa kifedha na hivyo alikuwa akimsaidia sana Rabia kwa kila alichokuwa anakihitaji.

Baada ya miezi michache Rabia aliamua kumchukua mdogo wake wa kike na kuja kuishi naye jijini Dar es salaam, Mdogo wake alikuwa amemaliza kidato cha nne kwa wakati huo. Maisha waliyokuwa wanaishi pale nyumbani Rabia alikuwa hapendi sana kutoka na kwenda katika sehemu ambazo ni za starehe lakini mume wake alikuwa akipendelea sana, hivyo Rabia alimtaka mdogo wake awe anaongozana na shemeji yake. Mdogo wake Rabia alikuwa ni binti mrembo sana, mwenye umbo na sura nzuri ya kuvutia, na alikuwa akipendeza kwa kila aina ya vazi alilokuwa akivaa.

Maisha yaliendelea huku Rabia akiwa anamuweka karibu sana mdogo wake katika kila jambo ilifikia kipindi mume wake alimzoea sana mdogo wake na Rabia hadi akawa anamuita mke mdogo, lakini Rabia hakujali na kuona ni kawaida kwa jinsi alivyokuwa anampenda mdogo wake na siku zote aliamini kuwa mdogo wake hawezi kumsaliti kwa kujihusisha kimapenzi na mume wake.

Pale nyumbani mdogo mtu alikuwa yupo huru sana. Siku moja Rabia alisafiri na kwenda Singida peke yake huku akimwacha mdogo wake na shemeji yake. Baada ya kuondoka kesho yake kama kawaida shemeji alimtaka mdogo wake na Rabia ajiandae watoke pamoja kwenda disko.

Walipofika huko walicheza na kunywa sana. Wakati wakiwa wanaondoka kuelekea nyumbani waliingia ndani ya gari huku wakiwa wamekumbatiana na kuanza kupeana mabusu motomoto bila ya kujali kitu chochote. Huku maneno ya kimahaba yakiwatoka kwa sauti ya chini "Unajua shemeji wewe ni mzuri sana kuliko hata dada yako" Mdogo mtu akawa anajichekesha na kusema "Asante shemeji, yaani mimi nimekuzoea laiti tungeonana mapema kabla haujamuoa dada yangu".

Walipofika nyumbani mchezo ule uliendelea kama kawaida hadi aliporudi Rabia na kukuta mabadiliko. Mwanaume alikuwa akionyesha wazi kwa kiasi gani anampenda shemeji yake mara nyingi alikuwa akitaka chakula apikiwe na shemeji na kila inapofika jumamosi alikuwa akitoka na shemeji yake. Kutokana na mabadiliko hayo Rabia alianza kupata wasiwasi "Hivi mbona sikuhizi simuelewi mume wangu, mmmh au kuna kitu kinaendelea kati yake na mdogo wangu, Lakini haiwezekani jamani, mdogo wangu akatoka kimapenzi na shemeji yake" Aliwaza na kujiuliza maswali mengi sana bila ya kupata majibu.Siku moja usiku wakiwa wamelala Mume wake Rabia kutokana na uchovu alikuwa amelala usingizi wa pono.

Ndipo Rabia alichukua simu ya mume wake na kuanza kusoma ujumbe "Nakutamani sana tunda la moyo wangu, huyu dada yako namuona kama mzigo, yaani sijui nimwambie asafiri tena, nalikosa sana penzi lako, asali wa moyo wangu" Ulikuwa ni ujumbe umeandikwa na Mume wake Rabia aliokuwa anamtumia shemeji yake.

Baada ya Rabia kusoma ule ujumbe, alishindwa kujizuia na kujikuta akilia kwa sauti kali iliyojaa kigugumizi. Ndipo Mume wake alishtuka kutoka usingizini na kusema "Vipi wewe una matatizo gani? Unaumwa? Kuna nini kimetokea? " Kwa sauti ya unyonge Rabia akasema " Siamini mume wangu kama umeweza kunisaliti kwa mdogo wangu wa damu, yaani wewe kweli ni wakunifanyia hivi".

Huku akiwa anampa ule ujumbe kwenye simu. Mwazoni alijitahidi kujitetea lakini baada ya kuona mke wake amemzidi akawa mkali na kusema "Basi amini unavyohisi wewe, na pia jichunguze wewe unakasoro gani ambazo zinanifanya mimi nimpende mdogo wako" Rabia alikuwa kama amechanganyikiwa alikosa amani kabisha na hata aliponyanyuka na kwenda chumbani kwa mdogo wake huku akionekana kuwa na jazba mume wake almfuata na kumzuia asimpige mdogo wake.

Purukushani ziliendelea hadi asubuhi ambapo Rabia aliamua kukusanya vitu vyake na kutaka kuondoka. Mdogo wake alipoona hivyo alianza kuomba msamaha na kulia kwa uchungu "Dada nisamehe, shetani alinipitia, naomba ubaki na mume wako mimi nitaondoka." Lakini Rabia hakutaka kumsikiliza na kuamua kuondoka kurudi nyumbani kwao Singida.

JE UNAFIKIRI NANI WA KULAUMIWA KATIKA SIMULIZI HII
 
Inamaana imeisha? Endelea mkuu maana naamini siku zote carma haiwezi kumuacha salama mdogo mtu.

Ila wakulaumiwa ni huyo mume wa Rabia kwani alishindwa kujizuia na kulinda heshima ya mkewe. Anyway majaribu ni mtaji
 
Back
Top Bottom