Msimu huu wa Sikukuu ni vema ukatoa misaada kwa watu!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Ni vema kipindi hiki cha Msimu wa Sikukuu za Mwisho na Mwanzo wa Mwaka ukajitolea kusaidia watu kwa kiasi cha Pesa!.

Haujakatazwa kufanya starehe lakini angalau tenga kiasi kidogo ambacho kitawagusa wengine ili nao wajihisi ni sehemu ya wanadamu!.

Unapita sehemu unamkuta mama anachoma mahindi kabeba mwanaye mgongoni huku kimuonekano akiwa anaonekana kabisa anapitia mambo magumu,hebu msaidie tu hata elfu 20 atakushukuru sana!.

Umepita sehemu ukakuta mwanamke amekaa kwenye kigoda anauza karanga na vikorosho kwenye sinia,hebu msaidie hata elfu 10 tu ili umtie moyo maana pia ni watanzania wenzetu!.

Hata kama unaishi na majirani ambao unatambua kabisa hali yao ya kiuchumi si nzuri,hebu kanunue angalau vyakula kidogo utenge na kiasi kidogo cha pesa uwapelekee,watafarijika sana hawa watu na hutapungukiwa na chochote!.

Kipindi hiki si cha kujikweza kwa mali ulizochuma mwaka mzima,bali mshukuru Mungu nawe pia utoe kwa wenzio!.

Usipende kwenda Kunywa Pombe za gharama na marafiki zako wakati huo jirani yako akiwa anapitia changamoto za chakula!,Hao marafiki unaowanunulia pombe ukiondoka kwenda Chooni watabaki wanakujadili na kukusonya lakini jirani atakuombea!


Jifunze kusaidia watanzania wenzio!
 
Kusaidia ni kulipa kodi za serikali na serikali ndio inajua walipo wahitaji.
Wagogo waliopo Dar toka mwanzoni mwa miaka 1980 mpaka leo wanaomnba tu, haijulikani wanapopeleka fedha.

Roho ya ombaomba Mungu hapendi na mkono wa kutaka kupokea kila siku haubarikiwi.
 
Back
Top Bottom