Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

La Lowassa ni tukio moja ambalo lilipita lakini hii ya kuwafananisha watu na mbwa imekuwa ni kejeli inayojirudia kila siku.

Hata hili litapita, labda kama ww ndio Lowassa useme limepita. Unasema kuwafananisha watu na mbwa linajirudia, ni lini tena lilisemwa ili tuwe na uhakika na usemacho?
 
Shambulia hoja badala ya watu
Hoja ya ukabila umeiibua wewe
Bavicha mnaua chama kwa kuendekeza upambe,huna,hadhi,uwezo wala nguvu ya kumshambulia Mzee Mwanakijini,inahitajika tafakuri pana ili kupangua hoja zake,Hizo sio size yako
 
Fafanua tafadhali
Mifano ya nchi ulizotumia kufikia conclusion hazina mazingira ya kisiasa, kiuchumi, kiuelewa miongoni mwa wananchi, yanayofanana na Tanzania. Katika nchi hizo sidhani kama polisi hubeba masanduku yenye kura na kukimbilia uchochoroni, na leo tumlaumu Mbowe tumshinikiza kung'oka eti kwa sababu chama anachokiongoza kimeshindwa kuchukua dola katikati ya hujuma za wazi wazi, ambazo zingine zinapaswa kukataliwa na wananchi bila kujali ni wanachama au wapenzi wa vyama gani. Kumnyoshea kidole Mbowe kutaka ang'oke katika uongozi wa Chadema huku wanachama na wananchi wakishuhudia vituko vya akina Mwambe, huku wakishuhudia nguvu ya dola na CCM kutaka ang'oke ni kuwafanyia dhihaka watu hao....sumu haionjwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Nisahihi mbowe akubali kwamba hali ya chama chini ya misingi anayoisimamia ni mbaya hivyo apishe fikra nyingine hii pia itaonesha demokrasia ndani ya chama kwakuwa ndiyo wanayoihubiri kilasiku, pengine ajaye ataleta maendeleo kwani mbowe sasa hasaidii chama kuwa na demokrasia na maendeleo Bali ubabe na msambaratiko. Tuwe wepesi kupokea mabadiliko hats kwa kushawishi watu wampokee Lowassa na kumpa hadhi kubwa (kumkabidhi nafasi kuu) huku haaminiki ilikuwa ni sababu tosha yayeye kujiuzulu kiheshma pasi na kusubiri watu wamchoke.
 
Mbona sijawahi kukusikia ukitoa msimamo Mrema, Cheyo, Doutwa, Lipumba au Magufuli wajiuzulu?
 
Mbona siku nyingi tu tuliwaambia Chadema ni chama chake yeye binafsi Mbowe kwa maslahi ya ukoo wa Mbowe, msipate shida kulielewa hilo.

Kama Watanzania wengine ambao hawakuelewa kwa nini Dr. Slaa alinyimwa haki yake kugombea pale aliponyang'anywa tonge mdomoni. Mna wakati mgumu kumwelewa Mbowe na kampuni yake binafsi.
 
Mbowe hapo alipo anacheeka...

Nothing so far has seemed to work for them...kama aliondoka bwana yule na bado hiki chama kikabaki strong, bwana huyu ana lipi hasa? Labda useme kaondoka na taarifa za mipango, mbinu au siri chafu... Madhara yapo japo si makubwa kama ambavyo akina fulani wanavyoaminisha watu huko twittani na instagramuni!
 
Nahisi hujanielewa..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusidanganyane hapa. Hakuna chama cha siasa kinachofurahia kuondokea na wanachama wake tena viongozi wa juu. Hawa viongozi wanavyoondoka kila kukicha ni dhahiri wanapunguza pia imani kubwa kwa wanachama wa chini. Infact, Chadema inapuputika taratibu.

Chadema ikiendelea kulifumbia macho tatizo hili na kuona kila anaendoka hana athari yoyote atakuja kubaki mbowe na mtei ambao ndo wenye maslahi yao kwenye hicho chama.


Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Wote waliotaka kugombea nae wamerudi nyumbani kwa waliowatuma maana ngoma imedunda. Hizo mbinu mpya unazozitaja ni za kuendeleza chama ama kukiuza kama wengine walivyouza ubunge/udiwani wao?
Tatizo cdm hawaandai viongozi, na inakuwaje ukubwa wote huu wa chama hakuna viongozi walio andaliwa kushika hatamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…