Mahaba dhidi ya Magufuli yamekufunika, Acha kutuinjoi hapa! Lowassa ndiye Rais wako, Watanzania walio wengi wameshaamua badala yako, maana hukujaliwa busara ya kujua jema na baya![/QUOwTE]
Wewe Musa tambua kuwa wingi si hoja na pia elewa WaTZ wengi upeo bado mdogo sana wa kuchambua mambo. Leo hii unasahau kuwa Cdm ndo walikuwa mstari wa mbele kuwaeleza kwamba ENL ni fisadi lililokubuhu tena walimtaja pale mwembe Simba kuwa ni miongoni mwa mafisadi PAPA 11 walioifilisi nchi, na mlishangilia kweli. Kama haitoshi Cdm wakasema wana ushahidi na anayeona kaonewa aende mahakamani kwani ENL alienda kushtaki au hata kukanusha??? Leo watu haohao wanasema ENL ni msafi na nyie nyumbu bado mnashangilia tu. Tafakari kijana acha kupelekwa kama bendera fuata upepo. Ishughulishe akili yako