Msimamo binafsi: Mabadiliko (Yes) Lowasa (Big No)

Msimamo binafsi: Mabadiliko (Yes) Lowasa (Big No)

Huu ni msimamo wangu binafsi simlazimishi mtu yoyote kuufuata maana waswahili wanasema" Wengi wape".
MUNGU akipenda tarehe 25/10/2015 siku ya uchaguzi nitafanya ifuatavyo.
1. Ubunge: Nitampigia kura ya ndiyo mbunge toka UPINZANI.

2. Udiwani: Nitampigia kura ya ndiyo diwani toka UPINZANI.

3. URAIS: Kura itaharibika maana Lowasa simkubali hata kidogo. Siwezi shiriki dhambi ya kumkabidhi nchi hii Edward N. Lowasa.
Hata ikitokea ENL akashinda binafsi sitamtambua kama Rais wangu (atakuwa rais wa hao waliompitisha).
HUU NDIYO MSIMAMO WANGU MIMI. Naomba msimamo wangu uheshimiwe

naona umekurupuka. Unaonekana kwenye ubunge unachagua chama kitu ambacho pia si sahihi ' chagua kiongozi bora bila kujali anatoka chama gani.
Kama vile ulivyoona kuwa lowassa sio kiongozi bora huwezi kumchagua.
 
Hapa nilipo mbunge na diwani kutoka Upinzani wapo vizuri sana.
 
Vyama vinavyoshiriki uchaguzi vipo zaidi ya 10 ikiwa unapenda mabadiliko na humpendi Lowasa iweje uharibu kura ya urais wakati kuna wapinzani kibao wanagombea?.Lkn pia lazima tukubali kuwa Dr Slaa ni mwanamapinduzi lkn hana ubavu wa kushindana na Magufuli hivyo kumpata m2 km Lowasa anaekubalika kuliko mwanasiasa yeyote tz ni fursa.Cha msingi tumtoe adui(ccm) mengine tutarekebisha coz huwezi juwa km hivi vyama vikubwa km vitakuja pata fursa km hii ya kuungana na kuwa ki2 kimoja
Wanamabadiliko mda ni sasa wanafiki wakae pembeni tusikatishwe tamaa ni vimisimamo vya kinafiki km vya ACT eti watapiga kampeni kumpinga Magufuli na Lowasa ilihali hawajasimamisha mgombea wao sasa ndo nn
 
Mpigie kura kiongozi unayedhani anakufaa.

Good, then sioni mantiki ya uzi wako. Ulitaka kubishana maana kama msimamo kila mtu anao, au ulitaka kushawishi lkn pia hukuwa specific ili tujue hasa wataka nini.
Anyway have a blessed day
 
Vyama vinavyoshiriki uchaguzi vipo zaidi ya 10 ikiwa unapenda mabadiliko na humpendi Lowasa iweje uharibu kura ya urais wakati kuna wapinzani kibao wanagombea?.Lkn pia lazima tukubali kuwa Dr Slaa ni mwanamapinduzi lkn hana ubavu wa kushindana na Magufuli hivyo kumpata m2 km Lowasa anaekubalika kuliko mwanasiasa yeyote tz ni fursa.Cha msingi tumtoe adui(ccm) mengine tutarekebisha coz huwezi juwa km hivi vyama vikubwa km vitakuja pata fursa km hii ya kuungana na kuwa ki2 kimoja
Wanamabadiliko mda ni sasa wanafiki wakae pembeni tusikatishwe tamaa ni vimisimamo vya kinafiki km vya ACT eti watapiga kampeni kumpinga Magufuli na Lowasa ilihali hawajasimamisha mgombea wao sasa ndo nn
Umeona eeh, sidhani kama hayajui hayo huenda ana mood ya debate kama kweli ni ukawa huyu mtu.
Muda wa kunyoosheana vidole haupo ndio maana namkubali sana Dr Slaa kuliko Lipumba. Slaa anataka mabadiliko na amefight kweli, ametofautiana kimaamuzi amekaa kimya maana anajua akiongea atarudisha nyuma hatua kubwa zilizofikiwa tayari unlike Lipumba ambaye moja kwa moja anaonekana kutumika kurudisha nyuma maendeleo thank God hana impact kama Slaa.

So mleta mada wetu hakupaswa kuandika hapa 'msimamo' wake; maana to me inaonekana bado hana msimamo anajicomvice zaidi kuliko kuwacomvice wengine.
 
Ni hajabu sana kuona mtu anaipenda ccm, lakini ni mshangao mkubwa kuona kundi la mafisadi linasafishwa ili lipewe ikulu.
 
Kura yangu ilikuwa inamsubiri Jemedari Wilbroad Slaa; sasa ndiyo hivyo tena. Genge la wanyang'anyi kutoka CCM limevamia CDM. Siwezi mpa kura yangu kiongozi mkuu wa MAFISADI.

MCHAWI mpe mtoto akulelee na pia unatakiwa utambue kuwa tunamtaka mgombea atakayeweza kuiondoa CCM madarakani. Akishakuwa raisi mafisadi wa CCM kuanzia ngazi ya vitongoji mpaka mawaziri watafyekwa. Viongozi watakuwa wapya kutoka ukawa. Hivyo basi tutapumua kuna vijana makini sana wana mapinduzi kutoka ukawa. Usidhani RAIS ni kama baba wa nyumba. KIKWETE hata kama ni fisadi sio kama watendaji wake hao ndio hatuwataki.Ili tuwaondoe inabidi CCM ichinjwe mpaka ife.
 
LOWASA mpinzani???? Hii ni kali ya karne. Wewe mchague ila mimi ni big NO.

he deserve to be our president pls choose YES EL. tatizo ccm haiaminiki mambo ya serkali yake hayafuati sheria, katiba hawaijari mpaka litoke tatizo, haki za msingi zinaminywa, bora wakae pembeni wajisahihishe, tunawapanda lkn hawapendeki 50yrs
 
MCHAWI mpe mtoto akulelee na pia unatakiwa utambue kuwa tunamtaka mgombea atakayeweza kuiondoa CCM madarakani. Akishakuwa raisi mafisadi wa CCM kuanzia ngazi ya vitongoji mpaka mawaziri watafyekwa. Viongozi watakuwa wapya kutoka ukawa. Hivyo basi tutapumua kuna vijana makini sana wana mapinduzi kutoka ukawa. Usidhani RAIS ni kama baba wa nyumba. KIKWETE hata kama ni fisadi sio kama watendaji wake hao ndio hatuwataki.Ili tuwaondoe inabidi CCM ichinjwe mpaka ife.

Napenda watu wenye critical thinking kama wewe. Wengine ni kama manyumbu tu hawajui wanashabikia nini.
 
Hakuna mabadiliko bila kuitoa CCM na ili ccm ccm ivunjikr ni lazima ivunjwe na mwanaccm
nikuulize swali do go kama Una ufahamu wa biblia..... hivi kama kama waisraeli wangemkataa Musa kwa Sababu tu alikulia na kuishi kwa farao wangeokolewa kweli???
tunakubali kuwa Lowasa kama binadamu yoyote anamapungufu yake lakini Ana mvuto Ana mtaji mkubwa wa watu utajiri wa kisiasa si pesa ni watu
kama ubalipenda boga penda na maua yake

Sio kila mabadiliko unayahitaji, kuna mabadiliko chanya na mabadiliko hasi, sasa kama lengo ni mabadiliko hata kama ni mabadiliko hasi siwezi poteza kura yangu
 
Angalia makundi yanayompigia debe utajua mentality ya watu wanaofikiria wataletewa maendeleo. Especially na huyu mtu anaitwa Lowassa. Ndo utajua kuna minyumbu mingi sana nchi hii, hayataki shule wala kazi yanataka vitu kirahisi rahisi tu ndo maana yana mda wa kuandamana kila kona. Msipobadili fikra zenu hata mpewe Yesu na Mtume kwa pamoja kuwaongoza mtabaki mlipo. Mkuu una point, kura zangu za ubunge na udiwani zinaenda upinzani uraisi Lowassa hapati kura yangu niko radhi nisipige kura.
 
Huu ni msimamo wangu binafsi simlazimishi mtu yoyote kuufuata maana waswahili wanasema" Wengi wape".
MUNGU akipenda tarehe 25/10/2015 siku ya uchaguzi nitafanya ifuatavyo.
1. Ubunge: Nitampigia kura ya ndiyo mbunge toka UPINZANI.

2. Udiwani: Nitampigia kura ya ndiyo diwani toka UPINZANI.

3. URAIS: Kura itaharibika maana Lowasa simkubali hata kidogo. Siwezi shiriki dhambi ya kumkabidhi nchi hii Edward N. Lowasa.
Hata ikitokea ENL akashinda binafsi sitamtambua kama Rais wangu (atakuwa rais wa hao waliompitisha).
HUU NDIYO MSIMAMO WANGU MIMI. Naomba msimamo wangu uheshimiwe

Safi sana sanaaaa mwenye kujitambua hawezi kumpa kura JIZI LA MAJIZI
 
Angalia makundi yanayompigia debe utajua mentality ya watu wanaofikiria wataletewa maendeleo. Especially na huyu mtu anaitwa Lowassa. Ndo utajua kuna minyumbu mingi sana nchi hii, hayataki shule wala kazi yanataka vitu kirahisi rahisi tu ndo maana yana mda wa kuandamana kila kona. Msipobadili fikra zenu hata mpewe Yesu na Mtume kwa pamoja kuwaongoza mtabaki mlipo. Mkuu una point, kura zangu za ubunge na udiwani zinaenda upinzani uraisi Lowassa hapati kura yangu niko radhi nisipige kura.

Nisaidie kuyaeleza MISUKULE ya Taifa hili
 
naona umekurupuka. Unaonekana kwenye ubunge unachagua chama kitu ambacho pia si sahihi ' chagua kiongozi bora bila kujali anatoka chama gani.
Kama vile ulivyoona kuwa lowassa sio kiongozi bora huwezi kumchagua.

Alicho kiona yy nisahihi kuliko kuwa FUATA UPEPO
 
Mag3 sio wewe bali na mahaba yako ndiyo yamekusukuma kuchakachua na kuhakikisha unaleta list yako mpya ambayo Dr Slaa hajawahi kuitoa lengo lako ni utafute tu upenyo wa kuingiza jina la Dr John Magufuli.
Hii si akili salama.

Nakuomba tu mahaba niuwe wako tukimkata sie wananchi tar 25 oct mtulie tuliiii ili watu tuendelee na kuijenga nchi yetu pendwa.

Watu tunataka mabadiriko yasiyoongozwa na jizi la aina yoyote kwa mujibu wa takwimu.
Mr.Mak, watu wapuuzi kama wewe si kawaida yangu kuwajibu na ukiendelea na kukurupuka hovyo nitakuweka kwenye ignore list. Hebu pitia hii taarifa;

Slaa ataja mafisadi wapya - April 2011

WAMO VIGOGO WA CHAMA, WAZIRI MMOJA

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na kada wa chama hicho, Mabere Marando, jana walitaja orodha mpya ya waliyodai kuwa ni mafisadi.Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora, Dk Slaa aliwataja mafisadi hao kwa majina yao (yamehifadhiwa)kuwa ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu mmoja ambaye alimtuhumu kuhusika na wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Mwingine ni Rais mmoja mstaafu na waziri mmoja aliyekuwa Serikali ya awamu ya tatu na sasa yuko katika Serikali ya awamu ya nne kwa tuhuma za kuhusika na kuuza nyumba za Serikali bila kufuata utaratibu.

Wengine ambao wametajwa na Dk Slaa ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ambaye amewahi kushika nyadhifa nyingine serikalini kwa tuhuma za kuhusika na EPA.

Wengine ni wafanyakazi wawili wa kampuni moja inayomilikiwa na kada mkongwe wa CCM ambao wanatuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha kupitia Kampuni ya Kagoda ambao walitajwa na Marando.

Akifafanua tuhuma hizo, Marando alisema aliwafuatilia watuhumiwa hao wa kampuni ya kada huyo wa CCM na kugundua kuwa waliandika majina bandia katika hati za usajili wa Kagoda.

Marando alisema anaishangaa Serikali kutowachukulia hatua watu hao hadi sasa.

Alisema kama Serikali imeshindwa kufanya hivyo yeye ataisaidia kwa kuwa anao ushahidi wote.

"Tulipowataja mafisadi CCM walikanusha, sasa leo wanaibuka na kuwataja mafisadi hao na kuwataka wajiuzulu, huo ni uongo na sidhani kama watajiuzulu kwa kuwa wana urafiki mkubwa," alisema Marando.

Dk Slaa alitaja orodha hiyo katika mkutano huo ambao kabla ya jana ulipangwa kufanyika baada ya maandamano yao yaliyolenga kupinga Muswada wa Marejeo ya Katiba 2011, ambao tayari umeondolewa bungeni.

Dk Slaa alilituhumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuwachukulia hatua yoyote watuhumiwa hao tangu walipotajwa na chama hicho mwaka 2007 na kuongeza kuwa ataendelea kuwataja kwa kuwa haogopi na yuko tayari kufa.

Alisema kauli inayotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba nchi iko katika hali tete, inasababishwa na yeye mwenyewe kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi.

Miaka minne iliyopita,Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembeyanga wilayani, Dk Slaa aliwataja vigogo 11 wanaodaiwa kuwa ni mafisadi.

Awali, msafara wa Dk Slaa ukiongozwa na pikipiki zaidi ya 30 na magari ya polisi uliwasili katika uwanja huo wa mikutano saa 9:47 alasiri, huku ukishangiliwa na mamia ya watu waliofika uwanjani hapo.

Dk Slaa aliongozana na aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Segerea, Fred Mpendazoe, Profesa Abdallah Safari, Mabere Malando, Wilfred Rwakatale na Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge na Halmashauri wa chama hicho, John Mrema.

Katika mkutano huo pamoja na Dk Slaa,wanachama na viongozi mbalimbali walipewa nafasi ya kuzungumza na kwamba Profesa Safari alizungumzia nyumba za serikali zilizouzwa pamoja na udini.
Dr SLAA ATAJA ORODHA MPYA YA MAFISADI, WAFIKIA 17 - April 2011

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaja orodha mpya ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Vigogo hao ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, John Samwel Malecela, aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Philip Mangula, kwa kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu.

Dk. Slaa alitangaza majina hayo jana mjini Tabora alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Chipukizi. Alisema majina hayo ni muendelezo wa yale ya vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi aliyoyataja Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambayo ni 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Katika orodha ya mwaka 2007, Dk. Slaa aliwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), ambaye sasa ni marehemu, Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM) na Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM).

Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, kada wa CCM, Nazir Karamagi, Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM), Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na Rais Jakaya Kikwete...
 
naona umekurupuka. Unaonekana kwenye ubunge unachagua chama kitu ambacho pia si sahihi ' chagua kiongozi bora bila kujali anatoka chama gani.
Kama vile ulivyoona kuwa lowassa sio kiongozi bora huwezi kumchagua.

Kusema amekurupuka si sawa kama tayar ameshawapima wabunge na madiwani jimboni kwake nakutambua kwamba mpinzani ndiye anayefaa kosa lake liko wapi?
 
MIDFIELD, naona unaitaja listi ya mafisadi PAPA 11 lakini sina hakika kama unaijua listi. Ngoja nikumbushe kidogo hiyo listi;

  1. Dr. Daudi T.S. Balali
  2. Andrew J. Chenge
  3. Basil P. Mramba
  4. Gray S. Mgonja
  5. Patrick P. R. Rutabanzibwa
  6. Nazir Karamagi
  7. Nimrod Mkono
  8. Rostamu Aziz
  9. Edward Lowassa
  10. Benjamin W. Mkapa
  11. Jakaya Mrisho Kikwete
Miaka mitano baadaye hii listi iliweza kuongezeka ikijumuisha wafuatao;

  1. Dr. John Pombe Magufuli
  2. John Samwel Malecela
  3. Philip Mangula
  4. Fredrick Sumaye

MIDFIELD, kwa kukufahamisha tu ni kwamba kilichowaunganisha hawa mafisadi papa ni kitu kimoja tu, UCCM wao. Katika orodha zote mbili hakuwahi kutajwa kiongozi yeyote wa upinzani. Lowassa hayupo tena pamoja na hao mafisadi, kalihama kabisa hilo pango la wezi, sasa yuko UKAWA kwa wasio na doa.

Kaenda kwa wasafi kuchafua au siyo. Maana maji masafi ya kunywa yakiwa pipa zima, ukidondoshea kipande kidogo cha mavi mfano wa goroli sidhani kama watu wataona bado yanafaa kunywa. Naamini mtamwaga pipa zima sababu ya hicho kinyesi. Sawasawa na lowasa na chadema/ukawa, Kwa sasa hawawezi wakaongelea ufisafidi wa CCM watu watawashangaa.
Hiyo list yako ya pili uliyoitoa nadhani mmekaa ninyi mkaitengeneza ili kukidhi kile mnachotaka kiwe. Lakini watu wenye akili timamu wakikusikia watashangaa tu na kukuacha ulivyo maana pengine hujui utendalo. Dr Slaa hatujawahi kumsikia akitoa hiyo list. itakuwa list yako hiyo na wenzio mnaofanana
 
Msaada mkubwa utaweza pia kuupata kutoka kwa hawa watu hapa chini

Hao wote uliowaquote ndio wanaomsapoti. Wamekuingiza chaka wewe bado unacheza style ya zamani wenzako wameshabadili style. Siasa haiko static hivyo ndio maana hata sisi CCM tulilipiga chini azimio la Arusha ili kwenda na mahitaji ya wakati.

CCM hii movement na amshaamsha ya wapinzani especially UKAWA sio kwamba hatuioni na kuifeel na wala hatuibezi bali ndio mapenzi yetu kwa chama yaani kiufupi tunakufa na tai shingoni aka kijerumani
 
Back
Top Bottom