kishanshuda
Member
- Feb 25, 2011
- 73
- 11
nimemzidi kisomo mtu ambae ananipenda na kunijali sana na namuona ananifaa kuwa mwenza wangu maishani,mimi nakaribia pata mastesr wakati mwenzangu hata certificate hana. Ila ni mtu ambae tunajuana vizuri na ni kwa muda mrefu sasa, though hatujakuwa karibu kimapenz kwa muda pia.
Jambo hili la ndoa na yeye lilijitokeza kama wiki liyopita hivi tulipo onana ana kwa ana na kuongea mengi likiwemo hili la ndoa, na tulipofikia kuhusu elimu ye akasema anataka aanze soma serious sasa coz umri umeenda na anashindwa fanya mambo mengi ya maendeleo kutokana elimu hiyo.
Na katika maongezi na majadiliano nae tumefikia uamuzi wa yeye aanze degree ambayo itamchukua miaka mitatu hadi amalize na ndipo tuweze oana na hata aweze endelea na elimu yake pia zaidi.
Ila napata utata kidogo katika mambo yafuatayo, kwanza naona miaka mitatu ya kusubiri ni mingi , pia napata wasiwasi kuwa anaweza pata mwingine na kubadili mawazo wakati me nimekaa muda wote namsubiri yeye, sasa hapa nachanganyikiwa na hata sielewi.
Naombeni ushauri wenu wadau walau nijue nifanyaje katika hili
anaweza kujiendeleza mkiwa kwenye ndoa
Hahaha!!! Ruta imenibidi nicheke tukwani yamekuwa mashindano?
Nina jamaa yangu wa karibu mkewe ana PHD hapahapa A-Town......................naye yeye alikuwa kidato cha nne ..........na sifuri tu.........siku hizi anahangzika kupata BBA anasema safari imeanza.........kaacha shughuli zake za maana anahangaika na mambo ambayo wala Muumba hakumwandikia..............................matokeo yake anafeli kazi kununua mitihani ili apate cheti cha kututambia mtaani..........
hana hata certificate then anataka kusoma dgree? au mimi cjaelewa hapa certificate gani unazungumzia?
nashukuru kwa kuweza nielewa elimu ina'matter jaman hasa kwa maisha haya ya sasa hivi ahhh,Mtaanza kinafiki mkidhani mnapendana ila itafika point mtofautiane kiupeo. Elimu ina mata sana usijidanganye lazima mlingane au msitofautiane sana. Kingine kwa jamii zetu za kiafrika ambapo mume ni mbabe ni wazi itabidi uchague kuzika uwelewa wako au umwombe mungu mumeo awe mwelewa sana.
Hahaha!!! Ruta imenibidi nicheke tu
Kwanini unausemea moyo wa mwenzio au haujiamini au umeishaona yeye hajiamini??nashukuru kwa kuweza nielewa elimu ina'matter jaman hasa kwa maisha haya ya sasa hivi ahhh,
, me naweza kubali na tukafanya kila kitu hata tukawa mke na mume, ila yaweza kuwa me nikafanya jambo jema tu kwa mema ila sababu ya hiyo elimu ikawa utata coz it happens na watu yanawakuta hayo, hata ukiamua uamuzi mzuri tu na kwa mema tu itaonekana tu unajidai au unafanya kwa sababu ya elimu yako
Ila napata utata kidogo katika mambo yafuatayo, kwanza naona miaka mitatu ya kusubiri ni mingi , pia napata wasiwasi kuwa anaweza pata mwingine na kubadili mawazo wakati me nimekaa muda wote namsubiri yeye, sasa hapa nachanganyikiwa na hata sielewi.
Kwanini unausemea moyo wa mwenzio au haujiamini au umeishaona yeye hajiamini??
Elimu na ndoa ni vitu viwili tofauti hicho naomba uelewe, elimu doesn't guarantee you that utakuwa na ndoa au familia iliyo bora so kama mmeamua kuoana just go ahead msianze kuweka vikwazo sijui hadi asome awe na degree au masters, afterall anaweza kuendelea kusoma baada ya nyie kuoana
Thread Closed lolMkuu umeongea vyema sana
Sijui anachompendea huyo dada ni elimu yake au anampenda yeye kama yeye without hayo macertificate atakayoenda kutafuta
Eklimu haina mwisho na kama ni mkeo unayependa hata mkishaoana na hicho kisomo alicho nacho ni wajibu wako kumuendeleza na afikie malengo yake
Sidhani kama kuna haja ya wewe kusubiri mpaka apate degree maana wapo waliolewa wengi na wanasoma wakiwa na familia zao
So wewe jipangeni na mpendwa wako muendelee na mipango ya ndoa na then baada ya hapo anaweza kuendelea na kusoma
Kwa hiyo ni polisi kwa sasa?aliishia form 6 akaenda depo CCP
nimemzidi kisomo mtu ambae ananipenda na kunijali sana na namuona ananifaa kuwa mwenza wangu maishani,mimi nakaribia pata mastesr wakati mwenzangu hata certificate hana. Ila ni mtu ambae tunajuana vizuri na ni kwa muda mrefu sasa, though hatujakuwa karibu kimapenz kwa muda pia. Jambo hili la ndoa na yeye lilijitokeza kama wiki liyopita hivi tulipo onana ana kwa ana na kuongea mengi likiwemo hili la ndoa, na tulipofikia kuhusu elimu ye akasema anataka aanze soma serious sasa coz umri umeenda na anashindwa fanya mambo mengi ya maendeleo kutokana elimu hiyo. Na katika maongezi na majadiliano nae tumefikia uamuzi wa yeye aanze degree ambayo itamchukua miaka mitatu hadi amalize na ndipo tuweze oana na hata aweze endelea na elimu yake pia zaidi.
Ila napata utata kidogo katika mambo yafuatayo, kwanza naona miaka mitatu ya kusubiri ni mingi , pia napata wasiwasi kuwa anaweza pata mwingine na kubadili mawazo wakati me nimekaa muda wote namsubiri yeye, sasa hapa nachanganyikiwa na hata sielewi.
Naombeni ushauri wenu wadau walau nijue nifanyaje katika hili